JWTZ: Wasioitakia mema nchi yetu wanahamasisha kufanya vurugu, hatutasita kuchukua hatua

eshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) limewataka wananchi kupuuza wito wowote unaohamasisha vurugu na uvunjifu wa amani, likisisitiza kuwa hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi ya watakaohusika na vitendo hivyo.

Katika taarifa yake kwa umma, JWTZ imesema kuwa ina jukumu la kulinda usalama wa nchi na wananchi kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 pamoja na Sheria ya Ulinzi wa Taifa Sura ya 192.

Jeshi hilo limeeleza kuwa litaendelea kushirikiana na vyombo vya dola kukabiliana na matukio yoyote ya vurugu, ghasia na uvunjifu wa amani.

Aidha, wananchi wamehimizwa kutoa taarifa kwa viongozi wa vijiji, mitaa na vyombo vya ulinzi na usalama kuhusu viashiria vya uchochezi ili kudumisha utulivu nchini.

JWTZ pia limewahakikishia wananchi kuwa litaendelea kutekeleza majukumu yake ya kulinda mipaka, Katiba na mamlaka ya nchi sambamba na kushirikiana na wananchi katika kuimarisha amani, umoja na maendeleo ya taifa.

Taarifa hiyo imetolewa na Mkurugenzi wa Habari na Uhusiano Makao Makuu ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Luteni Kanali Sylvester Mangure.
Hatimaye Jeshi la ccm limejitokeza as expected. Captain Tesha alisema uchaguzi ukipita basi Jeshi litakuwa chini ya ccm.
 
sijaelewa wanaposema "hatutawlinda" wanamaanisha nini? kwamba hawatowalinda against who? je, ni hawatawalinda against the regime? hiyo lugha peke yake inaonyesha kabisa kwamba muelekeo ni mzuri hata kama siyo 7/7 lkn siajabu maandamano yatakayofwatila lugha itakuwa nyingine kwani jeshi sijawahi kusikia wakitumia lugha kama hiyo kwamba "hatutawalinda" ina maana kuna adui yetu na wanamjua hivyo ni swala la muda tu watakuwa apande wetu ...
Kaz ipo
 
eshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ)
eshi....
Na ieleweke hivyo
Nilishawahi kuleta mada kuwa polisi wamewezeshwa kushinda hilo eshi.....

sijaelewa wanaposema "hatutawlinda" wanamaanisha nini? kwamba hawatowalinda against who? je, ni hawatawalinda against the regime? hiyo lugha peke yake inaonyesha kabisa kwamba muelekeo ni mzuri hata kama siyo 7/7 lkn siajabu maandamano yatakayofwatila lugha itakuwa nyingine kwani jeshi sijawahi kusikia wakitumia lugha kama hiyo kwamba "hatutawalinda" ina maana kuna adui yetu na wanamjua hivyo ni swala la muda tu watakuwa apande wetu ...
Umefikiri vizuri sana. Wanajua kuna adui anawapiga wananchi , ila wao wamesema hawatalinda hao wananchi..
 
View attachment 3622142

Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) limewataka wananchi kupuuza wito wowote unaohamasisha vurugu na uvunjifu wa amani, likisisitiza kuwa hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi ya watakaohusika na vitendo hivyo.

Katika taarifa yake kwa umma, JWTZ imesema kuwa ina jukumu la kulinda usalama wa nchi na wananchi kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 pamoja na Sheria ya Ulinzi wa Taifa Sura ya 192.

Jeshi hilo limeeleza kuwa litaendelea kushirikiana na vyombo vya dola kukabiliana na matukio yoyote ya vurugu, ghasia na uvunjifu wa amani.

Aidha, wananchi wamehimizwa kutoa taarifa kwa viongozi wa vijiji, mitaa na vyombo vya ulinzi na usalama kuhusu viashiria vya uchochezi ili kudumisha utulivu nchini.

JWTZ pia limewahakikishia wananchi kuwa litaendelea kutekeleza majukumu yake ya kulinda mipaka, Katiba na mamlaka ya nchi sambamba na kushirikiana na wananchi katika kuimarisha amani, umoja na maendeleo ya taifa.

Taarifa hiyo imetolewa na Mkurugenzi wa Habari na Uhusiano Makao Makuu ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Luteni Kanali Sylvester Mangure.
KIKWETE ALIUZA NCHI KWA GENGE LA RAIA FEKI KINA ROSTAM GSM ZUNGU NK ..Wataua sana watanganyika hao watu... kwa kifupi JWTZ linatakiwa kuvunjwa lote na kuundwa upya.
 
Back
Top Bottom