"K" tatu ninazotamani kukutana nazo kabla ya mwaka kuisha...

sidhani hawasikii,japo nawajua kwa kiburi
watakuja niamini,sipe moyo kisirani
wasubiri waja na kheri,nawajua majirani
nawajua kwa jeuri japo waja ila wasubiri
Kofia nakuvulia, Mwalimu uko vizuri,
Vina umepangilia, na mizani iso shari,
Lugha umeipatia, kiswahili adhimuni
Hongera mwalimu wetu, Kwa ushairi tukuka
 
Dogo una mistari, ya vina hata mizani,
Kwa hakika ninakiri, kipaji kiko damuni,
Imelazimu kukiri, bila ya donge rohoni,
Kilichochacha usambe, uzima wake ni moto.

Loh,

Hawavumi kumbe wamo, babu ninakusifia
kwako mimi mbilikimo, kichanga ninatambaa
vipaji viso kipimo, bibi wajikusanyia
-ila-
unajichimbia shimo, wengine (uwe) unaniachia!

hahahah...

Kofia nakuvulia, Mwalimu uko vizuri,
Vina umepangilia, na mizani iso shari,
Lugha umeipatia, kiswahili adhimuni
Hongera mwalimu wetu, Kwa ushairi tukuka
 
Kofia nakuvulia, Mwalimu uko vizuri,
Vina umepangilia, na mizani iso shari,
Lugha umeipatia, kiswahili adhimuni
Hongera mwalimu wetu, Kwa ushairi tukuka
Kofia bora uvae,mwalimu hana uzuri,
MENGINE MALIZIA
 
[emoji23] [emoji23] [emoji23]...........kwani mnazungumzia K zipi mkuu?
 
Duuuhhh, nimefurahi sana kwa kutiririka vina!

Asante Mentor na Mzee mwanzangu Asprin kwa kunijibia!!

babu nakusalimia, labeka niitikie
jukwaani mepotea, umenyimwa na bibie
busara nakumbukia, urudi utupatie
na K kuwapitia, urudipo niitie!!!
 
Kwema jamani naomben niulize swali na mtaji wa laki nane naweza pafom bizness ya nafaka .Niko Moro.
 
Kausha damu je?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…