K Vant na tatizo la kusahau

K Vant na tatizo la kusahau

Acha upuuzi,unakunywa k-vant na stress zako na njaaa zako,pata supu kwanza kabla haujaanza kunywa alf agiza wa k-vant.ukiona zinaanza kkuita,agiza nyama au kitimoto roast na ndizi.endelea na zoezi la kumalizia kunywa.
 
Ukienda bar ukanywa Kvant utakuja tu kujikuta umeamka nyumbani kesho yake. Kumbukumbu ya mwisho ni kuwa ulikuwa bar fulani ukaagiza kvant.

Ndio maana babu yangu Asprin huwa yeye kvant yake ananitumaga nimletee nyumbani. Akinywa anasahau shida zake.
Achana kabisa na K Vant. Nliendaga kwetu migombani nikajiapiza sitatoka na motokaa mpaka siku narudi Dar. K Vant ikanituma twenzetu Mamsera... nikapiga mtungi nikasahau nimeenda na motokaa. Nikapanda boda mpaka home. Asubuhi nastuka sioni motokaa... nikaenda kuripoti polisi wizi wa motokaa...m

Jioni naenda baa kupunguza msongo wa mawazo, naiona motokaa na mmasai ananidai buku 2 ya ulinzi.....

K Vant shenzi sana walahi
 
We kunywa bia tuu ,k vant waachie wao wenyewe ,k vant haijawai kuwa na mwisho mzuri, kama ujapoteza simu basi umepasua kioo au imearibika vibaya, kama hamjapigana na wale ulioenda nao basi umekwaruzana na muhudumu au meneja ,kama hujamshika mtu makalio basi kunatukio tu utakuwa umelifanya linalofanana nalo kama hukupata ajari basi kulala kituoni ni kawaida.
 
We kunywa bia tuu ,k vant waachie wao wenyewe ,k vant haijawai kuwa na mwisho mzuri, kama ujapoteza simu basi umepasua kioo au imearibika vibaya, kama hamjapigana na wale ulioenda nao basi umekwaruzana na muhudumu au meneja ,kama hujamshika mtu makalio basi kunatukio tu utakuwa umelifanya linalofanana nalo kama hukupata ajari basi kulala kituoni ni kawaida.
Sitosahau hii kitu ktk maisha yangu yote
 
Sasa hivi ugonjwa wa kufeli Figo ni namba nne.
1. Kisukari
2. Presha
3. Ukosefu wa nguvu za kiume
4. Kufeli kwa Figo

Kumbuka Kuna pombe Kali nyingi Sana feki mtaani wanazotengeneza wachina majumbani. Zina sticker za tra na chupa halisi.
Especially konyagi, K vant na Hennessy.
Drink at your own risk.
Hasa hizi chupa ndogo za konyagi na kvant yani feki zipo mpaka kwenye maduka makubwa,nimeachana na hayo makalakali,yani usiombe ukagongana na hiyo feki ukinywa hata chupa ndogo moja utalewaeea siku tatu.
 
Wakuu, wote tunajua pombe zina athari nyingi ingawa pia zina utamu wake.

Mimi ni mnywaji wa pombe ingawa hazijawahi kunisumbua kwa maana ya kuwa addicted ila nikinywa siku yoyote naenjoy tu. Sijawahi kuwa mpenzi wa konyagi au pombe za aina hiyo.

Juzi juzi hapa nilipiga K Vant, ilinipeleka sana aisee. Na kwa siku kadhaa baada ya hapo nilikuwa nasahau sahau tu vitu ovyo. Niliwahi kusikia hii pombe ina matatizo hayo. Je, ni kweli yanawatokea wengi na ni ya muda mrefu au ni kama sehemu tu ya hangover?
Hilo la K Vant kusababisha tatizo la kusahau ni HUJUMA ya wapinzani dhidi ya kinywaji changu kitamu cha K Vant! Nina mwaka wa tano sasa nakunywa K Vant na nipo fiti kwenye memory.
 
Back
Top Bottom