Kaanzisha mahusiano mengine akiwa na mimba

Kaanzisha mahusiano mengine akiwa na mimba

Ukimpenda sanaaaa na ukamsikiliza sanaaaaa atakuchukulia poa sanaaaa matokeo yake atakutreat vyovyote.
Japo ngumu ila jaribu kumpuuza,usimtafute kwa simu wala njia yoyote,mfanye ajue kua to you ni kama kafariki ila mjulishe nia yako ya kumpima mtoto DNA akizaliwa.
Atajaribu kujirudisha after some time,Nina uhakika.Ila kamwe,narudia tena KAMWE usimrudie!
Sawa mkuu...
 
Hayo maneno tu mkuu...Kama ana mimba bhasi hilo jamaa linamtumia tu itakuwa demu wako mshamba hajui tabia za Madoctor kuna siku atarudi analia Mrudianw mkuu amini nakwambia... Wanawake akili zao hizi achana nazo usitake serious maneno yake lakini kwa hili analofanya Hakika move on damu ya mtu haipoteo kamwee...
 
Hayo maneno tu mkuu...Kama ana mimba bhasi hilo jamaa linamtumia tu itakuwa demu wako mshamba hajui tabia za Madoctor kuna siku atarudi analia Mrudianw mkuu amini nakwambia... Wanawake akili zao hizi achana nazo usitake serious maneno yake lakini kwa hili analofanya Hakika move on damu ya mtu haipoteo kamwee...
Daah kweli mkuu, ngoja nisitake sana serious
 
Mwache aende ..atarudi mwenyewe tu tena kwa magoti
 
Pole kwa yote endelea na mambo yako mengine yatajulikana mbele kwa mbele.
 
Duh aiseee mademu bana wakati mwingine akili zao wanazijuaga wenyewe
 
Wapo tu mkuu
Vijana wa sasa kuna sehemu mnakosea nayo ni kuchukua mwanamke bila kumjua vizuri mnachojua ni kutongoza kuchomeka na kutia mimba hamjui kama huyo mwanamke dish liko sawa au mwezi mchanga
 
Nashindwa kuelewa hata huyu jamaa anakwamia wapi, mimi mwanamke aniambie Sikutaki tuachane! Wala hata siulizi, mbaya zaidi akileta ushenzi unaopelekea kuleta maana ya Huna Hadhi ya kuwa na mimi, wala siwazi mara mbili.

Au nimeshakuwa Malaya!?
Ndiyo mkuu
 
Wakuu habari ya asubuhi.

Moja kwa moja niende kwenye mada, huyu mwanamke nimekuwa naye kwenye mahusiano kwa miezi kadhaa, kuna wakati alishika ujauzito, tukakubaliana kulea mimba hiyo, basi tukalea mpaka ilipofika miezi mitatu ndio balaa likaanza, yeye kutaka tuachane.

Kuna siku alikuja kunitembelea, alipofika akawa anachat sana na simu nikamuuliza vipi mbona uko busy na simu? Akanijibu "hata hivyo ni simu yangu" nilichukizwa na jibu hilo nikanyamaza, nikampa muda zaidi, nilivyoona kazidisha nikamnyang'anya hiyo simu nikaiweka pembeni, basi tukaendelea na mazungumzo, wakati simu yangu mimi iko pembeni ilipigwa na sms ziliingia ila sikupokea wala kusoma sms, baada ya muda nikasema ngoja niichungulie, nikajibu sms za muhimu kwa dakika chache, nikamrudia tukaendelea kuongea, tukamaliza tukaagana akaenda.

Alipofika nyumbani, akaniuliza hivi ulinionaje pale ulivyokuwa unajibu sms mimi nipo pale, nikamueleza vizuri kuwa nilijibu kuwa kuna ujumbe wa muhimu nilitumiwa, basi akaanza kusema hanitaki tuachane, sikumtilia maana nikihisi ni hali ya mimba, ila aliendelea kukaza msimamo wake, baadae nilikuta ameniblock njia zote, sms, calls whatsapp, njia zote za mawasiliano nikawa simpati, hiyo hali ikaendelea kwa week mbili.

Jana ndipo alinitumia sms ya kunijulia hali, nikamuuliza mustakabali wa mahusiano, akanijibu kuwa kashaanzisha mahusiano mengine, yana wiki moja, na amemueleza huyo mwanaume kuhusu mimba akakubali kuilea, nikamuuliza sababu ya kufanya hivyo endapo mimi mhusika wa mimba hiyo nipo na nimekubali kuilea akaniambia ni kwa sababu mimi hawezi kunitambulisha kwao kama baba wa mtoto, nikamueleza sio vizuri alivyofanya, nikamuuliza kuwa kuhusu suala la clinic akasema kuwa nikitaka nitampeleka au nisipotaka huyo jamaa atampeleka! akiwa katika mizunguko yake na huyo jamaa siku ya jumatatu nimpitie nimpeleke clinic.

Nikauliza kuhusu hatma ya mtoto alichonijibu kuwa mtoto atakuwa na baba yule atakayefahamika kwao kama baba mtoto na mimi nitakuwa kama baba mzazi, kitu asichoweza ni kunitambulisha kama baba mzazi wa mtoto na yule jamaa anafahamu hilo kuwa mimba ni yangu ila yeye ni mlezi, sasa wakuu niko njia panda.

Mtu aliyeamua kuwa nae ni doctor wa hospital ambayo nimekuwa nikimpeleka kwa ajili ya kucheck ultrasound scan, mwanzoni nilikuta mawasiliano yao akasema amemcheck kwa ajili ya issue za kiafya nikamzuia asiwasiliane naye, kumbe hakufanya hivyo aliendelea kuwasiliana nae kwa siri, ndipo imefikia mahali hapa.

Nifanyeje.
Hilo lina ugumu gani hadi uulize huku kwanza una uhakika gani kuwa mimba ni ya kwako.
Huyo achana naye endeleza mishe zako hivi wewe ni kijana au mtu mzima.
Acheni kutuaibisha wanaume.
 
Pole sana. Huyo amekuona "Zoba". Wanawake akili zao za kushikiwa sana, sasa inaonekana weww ulikuwa unampeleka "kidemokrasia" sana, akawa anakuona ni zoba.

Hiyo mimba ni yako, na mtoto ni haki yako hawezi kukunyang'anya hiyo.

Wewe achana nae, ila mtoto atakapozaliwa nakushauri uweze kuongozana na mzee mmoja, uende kwa wazazi wake ukaeleze kilichotokea na kuwa yule ni mtoto wako; Ili aitwe na yeye tuone kama atakukana mbele ya wazazi wake....
asisubiri mtoto azaliwe, kama kweli ana uhakika mimba ni yake na kwa hali ilivyo aende kwa wazazi wa binti sasahivi akaeleza kilichotokea na maamuzi na maneno ya binti yao na awambie kabisa kama binti yenu hanitaki ni sawa, na kama nyinyi pia mnaona sifai pia ni sawa lakini damu yangu kamwe haiwezi kuwa ya mtu mwingine alafu mimi ndo niwe kivuli, ijulikane mapema kabla mtoto hajazaliwa ili hata kadi la hospitali mtoto aandikwe jina la baba halisi wa mtoto
 
asisubiri mtoto azaliwe, kama kweli ana uhakika mimba ni yake na kwa hali ilivyo aende kwa wazazi wa binti sasahivi akaeleza kilichotokea na maamuzi na maneno ya binti yao na awambie kabisa kama binti yenu hanitaki ni sawa, na kama nyinyi pia mnaona sifai pia ni sawa lakini damu yangu kamwe haiwezi kuwa ya mtu mwingine alafu mimi ndo niwe kivuli, ijulikane mapema kabla mtoto hajazaliwa ili hata kadi la hospitali mtoto aandikwe jina la baba halisi wa mtoto
Nachukua ushauri huu
 
Back
Top Bottom