Nasra82~~
Uislam unafundisha:
Ikitokea mis understanding katika ndoa,tumia lugha nzuri ya busara,heshima na upendo kuwekana sawa.Ikiwa hamtosikilizana then wafuate watu wenye busara na hekma katika familia yake mkae wote mtafute muafaka,ikishindikana hapo washirikishe ndugu zako wewe wenye busara na hekma mjadili kwa lengo la kufikia muafaka,ikishindikana hapo wakutane ndugu wa pande zote mbili kwa wema na busara kutafuta suluhu.
Hizi hatua kwa asilimia kubwa huwa zinaleta matunda mazuri,kama ni mas'ala ya kisheria ya dini,basi atafutwe msomi na mjuzi wa mambo hayo alete fatwa na maadam mmechagua kuwa waislam inabidi tu mkosaji atii amri ya ALLAH na Mtume WAKE(SAW).
Ikiwa basi jitihada zote zimeshindikana na tatizo haliwezi kuisha basi muachane kwa wema ili kuepuka madhara ya namna moja ama nyingine kama vile kuchokana na kuudhiana na hatimaye kujihusisha katika zinaa,ama kuvunjika wema ambae ulitengenezwa kupitia kuunganisha familia zenu .
Tatizo lako linaonekana ni dogo(unless sijaelewa vema),sitarajii kama litafika mbali,almuhim mnasihi tu mumeo na kumkumbusha aya katika suratul-Nnuur inayozungumzia ukaribu wa wanandoa ni zaidi ya partnership,kila mmoja ni nguo ya mwenzake,kwahiyo hamna budi kufahamiana vema na kuhifadhiana mazuri na mabaya,no one is perfect,ni jukumu la kila mmoja kukumbushana ili mradi lugha laini ya mahaba na utii itumike katika kurekebishana.
Kama ndoa yako ni changa,ni muhimu kujifunza kwa waliotangulia katika hilo miongoni mwa watu wanaokutakia kheir katika maisha yako ya ndoa ikiwa ni pamoja na ndugu na jamaa wa karibu,pia hata ukweni kwako.
Nakutakia kila kheir katika ndoa yako,Mola amkuze vema mtoto wenu na awe MchaMungu.
Shukran
Qadhi