Kabati la Mr

Kabati la Mr

Konakali yani huwezi amini ktk ushirikina huyo mwanaume hayupo kabisa maana nawafaham kwao vizuri sana labda sababu zingine tu! ila la ushirikina nina uhakika hakuna maana ningeona baadhi ya mambo, kwa mfano nimejifungua karibuni tu lakn mtoto hana shada lolote la uganga zaidi kasomewa hakika tu na kwa watu washirikina mtoto huyo angekuwa na kamba mwanzo mwisho! kwa wale wakrisitu hakika ni dua ambayo anasomewa mtoto wa kiislam akizaliwa ipo ktk quran hiyo hivo sio shiriki! kipo anachoficha lakn sio dumba

bwanae we ndo mama mwenye nyumba
kama umejariu kuongea naye na haelewi somo wala darasa...
ngoja aende kazini "bomoa kabati"
 
Inaelekea unaijua sababu ukizingatia ulishakuta na kanga ambayo sio yako, zidisha maujuzi ili arudishe hiyo kanga kule alikoitoa!
 
Salaam aleykum!
Wapendwa naomba mnijuze, mme wangu kila akisafiri anafunga kabati lake la nguo hii inaashiria nn? kipindi cha nyuma nilikuwa nampangia nguo zake baada ya kizinyoosha nikakuta kanga na haikuwa ya kwangu, nilimuuliza sikupata jibu la kueleweka, siku iliyofuata akafunga kabisa na kuondoka na funguo kw bahati mbaya nilikuwa sijamaliza kunyoosha nguo zote hivo nilipomaliza nafungua kabati limefungwa nikaweka nguo ktk kabati yangu mpk jioni alivorudi nikampatia nguo zake, j2 nilikuwa nafanya usafi wa nguo zake nimeshazinyoosha naenda kufungua kabati lake nakuta kafunga na hayupo nchini na atakaa huko km 1 month hivi jamani nimuelewe vp au ni kawaida kwa wanaume kufunga makabati? au anaficha nn? hii inanipa mawazo naona mnieleweshe

Kuna vitu vya siri humo angalia sasa umeona Khanga tu tayari umekuja Jamvini hapa.

Je ukiona bange? au ukiona bwibwi? au ukiona mkuyati si utampeleka polisi kabisa Mr. wako!

Mmeo ameona huna siri ili kuepusha balaa ameamua awe anafunga na solex kabisa kabati
 
Salaam aleykum!
Wapendwa naomba mnijuze, mme wangu kila akisafiri anafunga kabati lake la nguo hii inaashiria nn? kipindi cha nyuma nilikuwa nampangia nguo zake baada ya kizinyoosha nikakuta kanga na haikuwa ya kwangu, nilimuuliza sikupata jibu la kueleweka, siku iliyofuata akafunga kabisa na kuondoka na funguo kw bahati mbaya nilikuwa sijamaliza kunyoosha nguo zote hivo nilipomaliza nafungua kabati limefungwa nikaweka nguo ktk kabati yangu mpk jioni alivorudi nikampatia nguo zake, j2 nilikuwa nafanya usafi wa nguo zake nimeshazinyoosha naenda kufungua kabati lake nakuta kafunga na hayupo nchini na atakaa huko km 1 month hivi jamani nimuelewe vp au ni kawaida kwa wanaume kufunga makabati? au anaficha nn? hii inanipa mawazo naona mnieleweshe

Usiwe na wasiwasi MAMA juu ya uaminifu wa ki-mapenzi. ningekuwa wewe ningeweka hisia zaidi ktk mambo ya kishirikina- huyo mr. wako anaweza akawa ni mtu wa ku attend mlingotini , huko ndiyo wanapewa mashart ya ajabuajabu, kuna kitu humo kabatini. wewe tafuta fundi akisafiri vunja uone kunani, weka kitasa ingine. mengine yatafuata badae- hawezi kukupa talaka wala nini, kwani itakula kwake
 
bwanae we ndo mama mwenye nyumba
kama umejariu kuongea naye na haelewi somo wala darasa...
ngoja aende kazini "bomoa kabati"

Inaelekea kuna Tatizo lipo tangu mwanzo, inakuwaje kila mtu na kabati lake katika chumba kimoja? Hivi mwanamume anakuwaga na kabati ehee?

anyway dada Nasra82, ushauri uliopewa na Afrodez ufanyie kazi, kama ulishamuuliza akasema alisahau na hajuhi kama kafunga ama la, we nenda katafute seremala na uvunje huo mlango akija atautengeneza tena

lakini kumbuka utakacho kiona uje utuambie
 
Nasra, acha kuchunguza mumeo, kama kafunga kabati, usiulize wala usiyake kujuwa kuna nini, kama umekuta Kanga usiulize wala kutaka kujuwa kuna nini. Washahili hunena "Akunyimae kunde, akupunguzia mashuzi".

Sasa wew unahangaika nini? Sometimes the best weapon ni ukimya, jifanye kama hujui wala huna habari ya kinachoendelea. Chunga ndoa yako, ndio muhim.
 
Konakali yani huwezi amini ktk ushirikina huyo mwanaume hayupo kabisa maana nawafaham kwao vizuri sana labda sababu zingine tu! ila la ushirikina nina uhakika hakuna maana ningeona baadhi ya mambo, kwa mfano nimejifungua karibuni tu lakn mtoto hana shada lolote la uganga zaidi kasomewa hakika tu na kwa watu washirikina mtoto huyo angekuwa na kamba mwanzo mwisho! kwa wale wakrisitu hakika ni dua ambayo anasomewa mtoto wa kiislam akizaliwa ipo ktk quran hiyo hivo sio shiriki! kipo anachoficha lakn sio dumba

Sasa kama si mshirikina, basi jibu unalijua.

Mmeo ni mzinzi. Kapime, ukijikuta uko salama omba talaka kabla hajakuambukiza virusi.

Ukikuta umeshayakanyaga mawaya, usikubali, nawe muambukize...:redfaces::redfaces::redfaces:
 
mbona jibu ni rahisi bi nasra?mume hayupo,kama wasiwasi umekuzidi,kwa nini usimwite fundi,ukavunja mlango wa kabati,ukaangalia kilichomo ndani,na lazima atakuwa ameficha kitu.Na kitu alichoficha hataki wewe ukione,ila jitayarishe kwa chochote utakachokiona.Huyo ni mume wako usiwe muoga,ukishaangalia cha kuangalia mwambie fundi akutengenezee kabati lako,na kama hujaona kitu nyamaza kimya usimwambie kitu huyo bwana.wanaume wengine mbele za watu huwadhanii kabisaaaaaaaa,lakini huwezi kujua pengine ana siri zake nzito,ondoa wasiwasi chungulia.Usipofanya hivyo,kila siku utaishia kujiuliza mwenyewe bila ya kupata jibu lolote lile
 
Inaelekea kuna Tatizo lipo tangu mwanzo, inakuwaje kila mtu na kabati lake katika chumba kimoja? Hivi mwanamume anakuwaga na kabati ehee?

anyway dada Nasra82, ushauri uliopewa na Afrodez ufanyie kazi, kama ulishamuuliza akasema alisahau na hajuhi kama kafunga ama la, we nenda katafute seremala na uvunje huo mlango akija atautengeneza tena

lakini kumbuka utakacho kiona uje utuambie

ahaa bibie umenichekesha sana....
lakini umeongea cha maana sasa mke na mume wanatakiwa wachagie kila kitu especially kwenye master bedroom.....
kama wanaishi pamoja na kufanya kila kitu ni kwanini kuonyesheana vitu iwe ngumu??
hahahahaahah na hiyo sentensi ya mwisho nimeipenda usisahau kutuambia utakacho kiona ....
 
Konakali yani huwezi amini ktk ushirikina huyo mwanaume hayupo kabisa maana nawafaham kwao vizuri sana labda sababu zingine tu! ila la ushirikina nina uhakika hakuna maana ningeona baadhi ya mambo, kwa mfano nimejifungua karibuni tu lakn mtoto hana shada lolote la uganga zaidi kasomewa hakika tu na kwa watu washirikina mtoto huyo angekuwa na kamba mwanzo mwisho! kwa wale wakrisitu hakika ni dua ambayo anasomewa mtoto wa kiislam akizaliwa ipo ktk quran hiyo hivo sio shiriki! kipo anachoficha lakn sio dumba
Basi rejea pendekezo namba tatu....! Nalo unalikataa?
 
Hivi kwanini usifungue hilo kabati? Fungua ujionee mwenyewe vilivyomo humo ndani kisha funga akili kichwani.

Sasa shosti, tumeambiwa kabati anafunga halifunguki..inamaanisha kafunga na funguo/kufuli.Unamshauri avunje?

Kwako Muuliza swali -
Huyu mumeo ulipoanza kuishi naye alikuwa na tabia gani?
Mna maisha ya chako chako, changu changu? au chako changu changu chako? Hii itakupa uhalali wa kumuuliza kwa nguvu zote au kukaa kimya.

Na kama wewe ndio unamfulia, kupasi na kupanga kabatini, muulize bado anahitaji hiyo huduma? Kama anahitaji basi dai funguo/kufuli la kabati ili uendelee na huduma.Vinginevyo sitisha hudumA HIYO MARA MOJA HADI HAPO MAZINGIRA MUAFAKA YATAKAPOPATIKANA KWA YEYE KUTOA USHIRIKIANO.
 
wala usipate taabu unajua wengine wanazaliwa na viuchawi vyao toka utoto we kuwa mpole fatilia taratibu utajua tu
Hilo nalo neno!!! Akikuta Hirizi inapumua anaweza ama nyumba.
 
Nasra82~~
Uislam unafundisha:
Ikitokea mis understanding katika ndoa,tumia lugha nzuri ya busara,heshima na upendo kuwekana sawa.Ikiwa hamtosikilizana then wafuate watu wenye busara na hekma katika familia yake mkae wote mtafute muafaka,ikishindikana hapo washirikishe ndugu zako wewe wenye busara na hekma mjadili kwa lengo la kufikia muafaka,ikishindikana hapo wakutane ndugu wa pande zote mbili kwa wema na busara kutafuta suluhu.

Hizi hatua kwa asilimia kubwa huwa zinaleta matunda mazuri,kama ni mas'ala ya kisheria ya dini,basi atafutwe msomi na mjuzi wa mambo hayo alete fatwa na maadam mmechagua kuwa waislam inabidi tu mkosaji atii amri ya ALLAH na Mtume WAKE(SAW).

Ikiwa basi jitihada zote zimeshindikana na tatizo haliwezi kuisha basi muachane kwa wema ili kuepuka madhara ya namna moja ama nyingine kama vile kuchokana na kuudhiana na hatimaye kujihusisha katika zinaa,ama kuvunjika wema ambae ulitengenezwa kupitia kuunganisha familia zenu .

Tatizo lako linaonekana ni dogo(unless sijaelewa vema),sitarajii kama litafika mbali,almuhim mnasihi tu mumeo na kumkumbusha aya katika suratul-Nnuur inayozungumzia ukaribu wa wanandoa ni zaidi ya partnership,kila mmoja ni nguo ya mwenzake,kwahiyo hamna budi kufahamiana vema na kuhifadhiana mazuri na mabaya,no one is perfect,ni jukumu la kila mmoja kukumbushana ili mradi lugha laini ya mahaba na utii itumike katika kurekebishana.

Kama ndoa yako ni changa,ni muhimu kujifunza kwa waliotangulia katika hilo miongoni mwa watu wanaokutakia kheir katika maisha yako ya ndoa ikiwa ni pamoja na ndugu na jamaa wa karibu,pia hata ukweni kwako.

Nakutakia kila kheir katika ndoa yako,Mola amkuze vema mtoto wenu na awe MchaMungu.

Shukran

Qadhi
 
Na kwanini kila mtu na kabati lake in the first place?

Salaam aleykum!
Wapendwa naomba mnijuze, mme wangu kila akisafiri anafunga kabati lake la nguo hii inaashiria nn? kipindi cha nyuma nilikuwa nampangia nguo zake baada ya kizinyoosha nikakuta kanga na haikuwa ya kwangu, nilimuuliza sikupata jibu la kueleweka, siku iliyofuata akafunga kabisa na kuondoka na funguo kw bahati mbaya nilikuwa sijamaliza kunyoosha nguo zote hivo nilipomaliza nafungua kabati limefungwa nikaweka nguo ktk kabati yangu mpk jioni alivorudi nikampatia nguo zake, j2 nilikuwa nafanya usafi wa nguo zake nimeshazinyoosha naenda kufungua kabati lake nakuta kafunga na hayupo nchini na atakaa huko km 1 month hivi jamani nimuelewe vp au ni kawaida kwa wanaume kufunga makabati? au anaficha nn? hii inanipa mawazo naona mnieleweshe
 
Assalaama alaykum. kwanza ningemshauri mke wangu afuate ushauri wa Kadhi.
Pili nimeshamueleza kama nimefunga sio big deal, achukue funguo upo kwenye droo ndogo ya kabati hilohlo, afungue aangalia na kisha awaambie alichokiona.
Tatu mwambieni na yeye aondoe security codes zote kwenye simu yake.
Nne, aache mawasiliano na ex-wake wote.
Tano, ajue nampenda na sina siri.
 
ndoa kweli ndoano, pole mama labda ndo benki yake siku hizi (joke). Katika hali ya kawaida nadhani kutakuwa na ku2 hataki ukijue ambacho anakitunza humo kabatini!
 
kwakuwa kasafiri 1month tafuta fundi wa vitasa alifungua ukague nguo mojamoja utajua kilichopo
 
Back
Top Bottom