Kabati la Mr

Kabati la Mr

Assalaama alaykum. kwanza ningemshauri mke wangu afuate ushauri wa Kadhi.
Pili nimeshamueleza kama nimefunga sio big deal, achukue funguo upo kwenye droo ndogo ya kabati hilohlo, afungue aangalia na kisha awaambie alichokiona.
Tatu mwambieni na yeye aondoe security codes zote kwenye simu yake.
Nne, aache mawasiliano na ex-wake wote.
Tano, ajue nampenda na sina siri.

mambo?
kumpenda mtu ni kumuamini,ungemuamini mkeo usingefungia kabati lako ukamwacha na mauza uza mwenzio...

Kwenye nyekundu nahisi,ndoa yenu imekumbwa na pepo mbaya wa kutoaminiana!...elekezenu nguvu zenu zote kuziba hio loophole kabla mambo hayajaharibika zaidi...
 
Nasra, me nafikiri haya yafuatayo yawezekana yanahusikana na ufungwaji wa kabati hilo
1. Ndoa yako imeshakuwa na mushkeli yu mkini huyo mumeo anakimada nje, especially kwa huo ushuhuda wa kanga uliyoiona
2. Inawezekana c kanga tu uliyoiona, humo kuna zawadi zitokazo kwa mumeo kwenda kwa kimada au kimada ameleta zawadi special kwa mumeo
3. Nina hakika, hayo ni maandalizi ya ndoa nyingine( jiandae na uke wenza)
4.. Inawezekana kabisa, hiyo safari ya mwezi nje , si safari ila yupo kwa nyumba ndogo(mke mdogo) na inawezekana humo kabatini kuna kadi ya gari ya mke mdogo, hati ya nyumba au kiwanja ambayo tayari mke mdogo ameshamilikishwa...

Pole kwa hilo, naungana na wadau wengine ikiwezekana mwite fundi, avunje kabati kwa nyuma then ulitudishe kama lilivyokuwa... hapo natumia mauzoefu mwenzio!!
 
mi nafikiri mtizamo wangu uko tofauti kidogo
1.kama alishamwambia na hakumpa jibu zuri asiendelee kumuliza sana hawa viumbe si mnawaelewa mara nyingi wakitoa jibu moja hawatakagi maswali mengine sivyo unaanzisha varangati
2.siwezi kusema hakupendi au anakupenda inaweza akawa ana siri zake ambazo ni ngumu kushare na wewe
3.nakushauri tafuta siku amesahau funguo hata ameingia kuoga fanya kama ulivoelekezwa gonga kwenye sabuni halafu katoe copy yako siku hayupo ingia pekua uwe tayari kupokea utayoyaona lakini funga vizuri sasa akirudi ndo umueleze,ukianza zile perepere zetu wakina dada nakwambia atahamisha izo siri na kabati ataacha wazi ndo utashangaa
 
Ukome na kiherehere chako

hehehe sasa huu ndio ushauri?
Pole nasra ni wanaume wachache hufanya hivyo
Labda hataki ujue dili zake za kusaka mshiko
Jaribu kufanya kauchunguzi kimya kimya tena mkiwa pamoja halafu nyanyuka ghafla nenda kafungue kabati uchakachue vilivyomo
 
Nahisi huyu mama ni gabachori, anakwiba kwa mme anapeleka kwa ex. So mzee anachunga mali zake.
 
Hii kali. It does not click in the head why the guy lock kabati yake.
 
Nahisi huyu mama ni gabachori, anakwiba kwa mme anapeleka kwa ex. So mzee anachunga mali zake.

hata mie nahisi,mumewe amemstukia ana katabia ka udokozi,vitu vyake goes missing...akaona afunge kabati lake....na wanaume hawaongeagi sometimes...utaona actions tu..LOL:embarrassed:
 
Ameamua kufunga kabati sababu bado anakupenda na anaona kabati linaweza kuwa chanzo cha matatizo.

Kama una mpango wa kumpiga kibuti ni wakati muafaka wa kutaka kupewa copy za funguo za kabati hilo.
 
Salaam aleykum!
Wapendwa naomba mnijuze, mme wangu kila akisafiri anafunga kabati lake la nguo hii inaashiria nn? kipindi cha nyuma nilikuwa nampangia nguo zake baada ya kizinyoosha nikakuta kanga na haikuwa ya kwangu, nilimuuliza sikupata jibu la kueleweka, siku iliyofuata akafunga kabisa na kuondoka na funguo kw bahati mbaya nilikuwa sijamaliza kunyoosha nguo zote hivo nilipomaliza nafungua kabati limefungwa nikaweka nguo ktk kabati yangu mpk jioni alivorudi nikampatia nguo zake, j2 nilikuwa nafanya usafi wa nguo zake nimeshazinyoosha naenda kufungua kabati lake nakuta kafunga na hayupo nchini na atakaa huko km 1 month hivi jamani nimuelewe vp au ni kawaida kwa wanaume kufunga makabati? au anaficha nn? hii inanipa mawazo naona mnieleweshe

Ni kabati la Mumeo na sio la kwako. Hivi tutajifunza lini kuheshimu mambo ya wengine. Hata kama ni mumeo bado una mipaka yako na ni lazima uiheshimu (privancy). tatizo watu wanataka kila kitu wawe huru nacho. pengine jamaa kaweka siri za ofisi na haruhusiwi kumwonyesha mtu. Pia kwanini kila mtu ana kabati??. Si mngeweka kabati moja tuu ili kila mtu ajifungulie anavyo taka. Mie naona jamaa anahaki kabisa ya kuondoka na fungue zake . jifunzeni kuheshimu mipaka yenu.
 
Jamani, wengi mnafanya conclusion ya haraka. nadhani huko nyuma hakuwa anafunga kabati. Alianza kufunga kabati baada ya Nasra kumconfront kuwa amekuta Kanga wakati anapanga nguo na hakupata jibu la kueleweka. Siku za nyuma hajatuambia kama amewahi kukuta kitu kama hicho.

Nadhani Mr wake anajua connection ya hiyo kanga na sasa hana jibu na huenda kuna zaidi. Je, kama kanga hiyo ni ya kimada wake? Ila itakuwa inafanya nini? Alisahau akarudi nayo home? Au alimleta home wakati Mrs hayupo?

Binafsi makabati ya home kwetu na wife yako accessible na kila moja wetu. In fact Mrs yeye ndo ana kazi ya kunichagulia nini ni nivae labda kama sijapenda. Pia hupanga na kupangua sanduku au bag langu kila ninapoenda na kutoka safari, sababu kitecheni party waliambiwa hivyo . . . . msiniulize mimi.

Kuna hadithi nyingi, wengine wamewahi kuwakuta husbands zao na underwear mpya na sisizo mpya lakini si za Mrs wao nk.

Kubwa, ambane mume wake hadi apate jibu la uhakika kuhusu hiyo kanga. Kisha amuulize sababu za kufunga kabati. Tatu afungue sixth sense yake, je ni yeye tu au ana mwenzake?
 
Ni kabati la Mumeo na sio la kwako. Hivi tutajifunza lini kuheshimu mambo ya wengine. Hata kama ni mumeo bado una mipaka yako na ni lazima uiheshimu (privancy). tatizo watu wanataka kila kitu wawe huru nacho. pengine jamaa kaweka siri za ofisi na haruhusiwi kumwonyesha mtu. Pia kwanini kila mtu ana kabati??. Si mngeweka kabati moja tuu ili kila mtu ajifungulie anavyo taka. Mie naona jamaa anahaki kabisa ya kuondoka na fungue zake . jifunzeni kuheshimu mipaka yenu.


Kazi kweli kweli. Ama kweli ndoa hazina formula. Privacy ya kabati la nguo?
 
Back
Top Bottom