Kabila la kwanza hadi la mwisho nchini kwa ubora wa kiasili wa uzalishaji vyakula vyenye lishe nchini:

Kabila la kwanza hadi la mwisho nchini kwa ubora wa kiasili wa uzalishaji vyakula vyenye lishe nchini:

Mgambilwa ni mntu

JF-Expert Member
Joined
May 30, 2017
Posts
2,869
Reaction score
3,187
Tangu kuingia kwa wageni nchini Tanzania hasa kuanzia kipindi cha wakoloni miaka ya 1880s hadi leo, kumekuwepo mabadiliko makubwa ya uingilianaji wa watu kutoka jamii/koo tofauti tofauti kutokana na mabadiliko yanayoletwa na maendeleo hasa ukuaji wa miji na kuimarika kwa miundombinu ya usafiri. Hali hii imesababisha mazao yanayolimwa upande mmoja wa nchi, kufikika kwa urahisi sehemu ya mbali. Mfano: leo hii sato wabichi (tilapia) wa Ziwa Victoria wanauzwa jijini Dar es Salaam kutokana na uwepo wa barafu na majokofu lakini zamani waliishia eneo la mwambao wa Ziwa ndani ya wastani wa km 15. Watu wa maeneo jirani na Ziwa umbali wa iliko kwa sasa miji kama Geita, Utegi, Bunda, Sengerema na Kamachumu, hawakuwa na uwezo wa kula samaki wabichi kwa kuwa, hakukuwepo hata baiskeli kipindi hicho zaidi ya kusafirisha kwa miguu.
Katika mazingira hayo, vyakula vilivyokuwa vikizalishwa na Kabila husika, viliishia kwenye Jamii hiyo kutokana na kutokuwepo mwingiliano wa kutosha wa watu wa makabila tofauti kipindi hicho pamoja na ukosefu wa usafiri. Hivyo, kama kabila lilikuwa linazalisha vyakula vya kutosha, vilisaidia tu jamii hiyo huku jamii ambayo iliishi maeneo yasiyozalisha chakula kwa wingi, ikiteseka yenyewe kutokana na mahusiano ya kishindani na ya kuogopana kati ya jamii na jamii.
Ifuatayo ni orodha ya makabila yote makubwa na maarufu nchini Tanzania, yakiwa na na uchambuzi wa masuala yafuatayo:
  • Hali ya hewa: viwango vya joto na mvua; idadi ya miezi inayopata mvua kuanzia mm 60.
  • Upatikanaji maji safi na ya uhakika (yasiyo na kiwango kikubwa cha fluoride)
  • Kiwango cha rutuba udongoni.
  • Kutokuwepo kwa magonjwa hatari (endemic) ya malaria na malale.
  • Uzalishaji wa mazao aina nyingi ya chakula.
  • Ufugaji.
  • Uvuvi.
  • Uzalishaji wa matunda.
IMG_2719.JPG
IMG_2724.JPG
IMG_2726.JPG

Makabila yaliyopata wastani wa A, ni yafuatayo:
1: Wanyakyusa
2: Wachaga
3: Wahaya
4: Wakerewe
5: Wameru
6: Waarusha
7: Wazanzibar (Wapemba, Watumbatu & Wahadimu)
8: Wakara
9: Waluguru
10: Wakurya
11: Waha
12: Wabondei
13: Wajaluo
14: Wasambaa
15: Wavidunda

NB:
I: Maeneo yenye A ndiyo yenye kiwango cha juu cha ubora na D (E) ni kiwango cha mwisho.
II: Chumba cha mwisho kulia "Ubora katika Uzalishaji" ndicho chenye wastani kwa kila kabila.
III: Kwa kuwa, kila Jamii ina maeneo yenye sifa tofauti, eneo (tarafa/kata/mji) lenye sifa nyingi ndilo lililochukuliwa kuwakilisha kabila husika. Kuna changamoto kwa baadhi ya jamii kuchagua mji/tarafa/kata ya kuwakilisha Jamii husika. Mfano: ushindani wa Kibosho, Marangu na Machame kwa uchagani. Hivyo nitafurahi sana kupata mrejesho wa masuala mengi, hasa kama kweli eneo nililochagua ni mwakilishi muafaka wa Kabila lako.
IV: Kuna maeneo yaliyoendelezwa miaka ya hivi karibuni (tangu kuja ukoloni) dhidi ya maeneo maarufu ya asili. Mfano kwa Wakwere, maeneo ya Chalinze, Mlandizi, Bagamoyo na Kibaha ni bora sana kwa sasa lakini hayakuwa hivyo kabla ya ukoloni. Eneo la Yombo linaonyesha kuwa na sifa zaidi.
V: Kuna vipengele vingine muhimu, sijaviingiza kwenye vigezo vya ushindani ili kupunguza taarifa kuwa more complex. Vigezo hivyo ni: kiwango cha Fluoride (fluorine); madini ya Iodine na ugonjwa wa schistosomiasis (bilharzia).
VI: Vyanzo vikuu vya Takwimu, ni pamoja na: Joshuaproject.net; en.climates-data.org; mapcarta.com; Aroundguides; Citypopulation.de; pamoja na Atlas nilizo nazo zipatazo tisa.

Nawasilisha wazee.
 
Kuna ka ukweli 100% hapo. Nkicheki kwa Tanga hayo maeneo kweli haya hali ya hela nzuri sana na wanazalisha vyakula kwa wingi hadi leo. Lakini kwa sasa karibu maeneo yote yanapata vyakula bora na ya uhakika kutokana na kuimarika kwa miundombinu ya usafirishaji na teknolojia ndo maana na sisi wanaume wa Dar es Salaam tunakula SATO ya Mwanza na Mafenesi na machingwa ya leo leo ya Muheza Tanga.Pia viazi/viepe vyua Mbeya vinatufikia bila wasiwasi.
 
Tangu kuingia kwa wageni nchini Tanzania hasa kuanzia kipindi cha wakoloni miaka ya 1880s hadi leo, kumekuwepo mabadiliko makubwa ya uingilianaji wa watu kutoka jamii/koo tofauti tofauti kutokana na mabadiliko yanayoletwa na maendeleo hasa ukuaji wa miji na kuimarisha miundombinu ya usafiri. Hali hii imesababisha mazao yanayolimwa upande mmoja wa nchi kufikiri kwa urahisi sehemu ya mbali. Mfano: leo hii sato wabichi (tilapia) wa Ziwa Victoria wanauzwa jijini Dar es Salaam kutokana na uwepo wa barafu na majokofu lakini zamani waliishia eneo la mwambao wa Ziwa ndani ya wastani wa km 15. Watu wa maeneo jirani na Ziwa kama miji ya Geita, Utegi, Bunda, Sengerema na Kamachumu, hawakuwa wakila samaki wabichi kwa kuwa, hakukuwepo hata baiskeli kipindi hicho zaidi ya kusafirisha kwa miguu.
Katika mazingira hayo, vyakula vilivyokuwa vikizalishwa na Kabila husika, viliishia kwenye Jamii hiyo kutokana na kutokuwepo mwingiliano wa kutosha wa watu wa makabila tofauti kipindi hicho pamoja na ukosefu wa usafiri. Hivyo, kama kabila lilikuwa linazalisha vyakula vya kutosha vitasaidia tu jamii hiyo huku jamii ambayo iliishi maeneo yasiyozalisha chakula kwa wingi, iliteseka yenyewe kutokana na mahusiano ya kishindani kati ya kabila na kabila.
Ifuatayo ni orodha ya makabila yote makubwa na maarufu nchini Tanzania, yakiwa na na uchambuzi wa masuala yafuatayo:
  • Hali ya hewa: viwango vya joto na mvua; idadi ya miezi inayopats mvua kuanzia mm 60.
  • Upatikanaji maji safi na ya uhakika (yasiyo na kiwango kikubwa cha fluoride)
  • Kiwango cha rutuba udongoni.
  • Kutokuwepo kwa magonjwa hatari (endemic) ya malaria na malale.
  • Uzalishaji wa mazao ya chakula.
  • Ufugaji.
  • Uvuvi.
  • Uzalishaji wa matunda.
View attachment 653183 View attachment 653184 View attachment 653185

Makabila yaliyopata wastani wa A, ni yafuatayo:
1: Wachaga
2: Wanyakyusa
3: Wahaya
4: Wakerewe
5: Wameru
6: Waarusha
7: Wazanzibar (Wapemba, Watumbatu & Wahadimu)
8: Wakara
9: Waluguru
10: Wakurya
11: Waha
12: Wabondei
13: Wajaluo
14: Wasambaa
15: Wavidunda

NB:
I: Maeneo yenye A ndiyo yenye kiwango cha juu cha ubora na D (E) ni kiwango cha mwisho.
II: Chumba cha mwisho kulia "Ubora katika Uzalishaji" ndicho chenye wastani kwa kila kabila.
III: Kwa kuwa, kila Jamii ina maeneo yenye sifa tofauti, eneo (tarafa/kata/mji) lenye sifa nyingi ndilo lililochukuliwa kuwakilisha kabila husika. Kuna changamoto kwa baadhi ya jamii kuchagua mji/tarafa/kata ya kuwakilisha Jamii husika. Mfano: ushindani wa Kibosho, Marangu na Machame kwa uchagani. Hivyo nitafurahi sana kupata mrejesho wa masuala mengi, hasa kama kweli eneo nililochagua ni mwakilishi muafaka wa Kabila lako.
IV: Kuna maeneo yaliyoendelezwa miaka ya hivi karibuni (tangu kuja ukoloni) dhidi ya maeneo maarufu ya asili. Mfano kwa Wakwere, maeneo ya Chalinze, Mlandizi na Kibaha ni bora sana kwa sasa lakini hayakuwa hivyo kabla ya ukoloni. Eneo la Yombo linaonyesha kuwa na sifa zaidi.
V: Kuna vipengele vingine muhimu, sijaviingiza kwenye vigezo vya ushindani ili kupunguza taarifa kuwa more complex. Vigezo hivyo ni: kiwango cha Fluoride (fluorine); madini ya Iodine na ugonjwa wa schistosomiasis (bilharzia).
VI: Vyanzo vikuu vya Takwimu, ni pamoja na: Joshuaproject.net; en.climates-data.org; mapcarta.com; Aroundguides; Citypopulation.de; pamoja na Atlas nilizo nazo zipatazo tisa.

Nawasilisha wazee.

Mbona sie wapimbwe hatupo
 
Wa Darslamu mbona hawapo?
Wa Dar es Salaam, ni Wazaramo kiasili, sisi wengine ni wa kuja. Mfano eneo la Mji wa Dar es Salaam kulikuwepo kijiji cha wavuvi lakini mwaka 1866 ndio Sultan Majid alijenga mji eneo hilo na ulikuwa hasa baada ya Wajerumani kuhamishia makao yao hapo kutoka Bagamoyo 1888 but Wazaramo wamekuwepo eneo hilo kwa miaka mingi. Hivyo huwezi ukasema Dar es Salaam ndilo lililokuwa bora wakati halina rutuba kama Maneromango japokuwa kuna bahari na wanaweza kuvua samaki.
So rutuba ya Tarafa ya Maneromango ni sababu kuu ya kuona eneo hilo ndilo bora kwa Wazaramo kuliko Dar ambako hakukuwepo watu wengi kwa kuwa ni udongo wa kichanga.
 
Kuna ka ukweli 100% hapo. Nkicheki kwa Tanga hayo maeneo kweli haya hali ya hela nzuri sana na wanazalisha vyakula kwa wingi hadi leo. Lakini kwa sasa karibu maeneo yote yanapata vyakula bora na ya uhakika kutokana na kuimarika kwa miundombinu ya usafirishaji na teknolojia ndo maana na sisi wanaume wa Dar es Salaam tunakula SATO ya Mwanza na Mafenesi na machingwa ya leo leo ya Muheza Tanga.Pia viazi/viepe vyua Mbeya vinatufikia bila wasiwasi.
Asante kwa kuielewa taarifa. Labda ninachokuomba pamoja na wengine, mnaweza kuwa na ufahamu mzuri wa makabila yenu hasa eneo lenye historia ya kuzalisha vyakula vingi na vya aina nyingi, pamoja na mifugo mingi, matunda na samaki.
 
Mbona sie wapimbwe hatupo
Wapimbwe ni nayo taarifa yao, tatizo nilitaka taarifa zote ziishie kwenye karatasi moja tu. Karatasi ya kwanza niliweka makabila 90 ikawa haionekani vizuri, hivyo nikaamua kupunguza baadhi ya makabila hasa madogo madogo. So kwa ajili yako nikitoka ofisini nitakupostia uone ilivyo na mazingira.
Of course ukiacha Wapimbwe, makabila mengine niliyoandaa taarifa yake lakini nikashindwa kuzi-feed zote ni:
Wawungu (wabungu), Wabende, Waalagwa, Wambugu, Wambugwe, Waikoma, Wadoe, Wasegeju, Wapemba, Watumbatu na Wahadimu.
 
Kila kabisa lingekuwa linakula chakula chote wanachokizalisha bila kutegemewa na wengine Nina uhakika wanyakyusa wangepasuka kwa misosi kedekede.
Wanyakyusa ni balaa. Mungu aliwajalia Kanda mbili tofauti kabisa za hali ya hewa:
  • Rungwe: Huku kuna baridi na mvua nyingi sana. Wanaishi kwa kutegemea zaidi ndizi.
  • Busokelo: Huku kuna baridi pamoja na joto la kadri. Wanaivisha ndizi na mikakao pia.
  • Kyela: Huku kuna joto na wanalima sana mpunga. Matunda pia ndio kwao. Ndizi pia zipo kibao. Ni wavuvi pia.
Ndicho kinachowafanya wawe na akili sana maana wanapata vya kula vya aina zote. Ukivikosa kwao, ni nadra kuvipata kwa makabila mengine.
Hakuna kabila lingine lililobarikiwa eneo kubwa lenye hali ya hewa na udongo wenye rutuba kama Wanyakyusa.
Baada ya Wanyakyusa, ndio wanafuatia Wahaya, bahati mbaya eneo la Wahaya halina rutuba kubwa kama maeneo yenye udongo wa volcano.
 
Ukiangalia mwaandiko kwa makini utagundua aliyeandika ni kabila gani
 
Ukiangalia mwaandiko kwa makini utagundua aliyeandika ni kabila gani
Dah, mzee umeniamulia. Sijataka kuitype but ni kwa sababu niko naandaa taarifa ambayo ni more comprehensive, ambayo nitai-type, hivyo nisamehe kama mwandiko umekuwa tatizo kwako.
 
Haya mambo ya Takwimu, ndio yaliomweka ndani Mh. Zitto Kabwe
Ndugu nimeweka vyanzo vingi vya taarifa hapo chini. Nilichofanya kama mchambuzi ni kuchambua hizo data katika perspective ya uzalishaji vyakula. Hebu angalia kwanza vyanzo vyangu vya taarifa ndiyo unihukumu.
But kwa kuwa, ninavifahamu vyote nilivyoviandika na na uelewa in and out, niko tayari kuvitetea vyote nilivyoandika hata kama ni pannel ya maprofesa, ikionekana kuna tatizo kwenye nilichoandika, pliz niko tayari kukifafanua.
Hii kazi mnayoiona siyo ya wiki moja wala mwaka mmoja, nimeifanya with patience and passion kwa miaka ipatayo kumi (10). Tangu niko UDSM, nilianza taratibu kukusanya details za baadhi ya masuala niliyokuwa tayari na idea nayo, mojawapo ni utofauti mkubwa wa makabila kielimu.
Ukiisoma taarifa hii with passion, for sure kuna kitu kikubwa sana utakipata.
 
Back
Top Bottom