Tangu kuingia kwa wageni nchini Tanzania hasa kuanzia kipindi cha wakoloni miaka ya 1880s hadi leo, kumekuwepo mabadiliko makubwa ya uingilianaji wa watu kutoka jamii/koo tofauti tofauti kutokana na mabadiliko yanayoletwa na maendeleo hasa ukuaji wa miji na kuimarisha miundombinu ya usafiri. Hali hii imesababisha mazao yanayolimwa upande mmoja wa nchi kufikiri kwa urahisi sehemu ya mbali. Mfano: leo hii sato wabichi (tilapia) wa Ziwa Victoria wanauzwa jijini Dar es Salaam kutokana na uwepo wa barafu na majokofu lakini zamani waliishia eneo la mwambao wa Ziwa ndani ya wastani wa km 15. Watu wa maeneo jirani na Ziwa kama miji ya Geita, Utegi, Bunda, Sengerema na Kamachumu, hawakuwa wakila samaki wabichi kwa kuwa, hakukuwepo hata baiskeli kipindi hicho zaidi ya kusafirisha kwa miguu.
Katika mazingira hayo, vyakula vilivyokuwa vikizalishwa na Kabila husika, viliishia kwenye Jamii hiyo kutokana na kutokuwepo mwingiliano wa kutosha wa watu wa makabila tofauti kipindi hicho pamoja na ukosefu wa usafiri. Hivyo, kama kabila lilikuwa linazalisha vyakula vya kutosha vitasaidia tu jamii hiyo huku jamii ambayo iliishi maeneo yasiyozalisha chakula kwa wingi, iliteseka yenyewe kutokana na mahusiano ya kishindani kati ya kabila na kabila.
Ifuatayo ni orodha ya makabila yote makubwa na maarufu nchini Tanzania, yakiwa na na uchambuzi wa masuala yafuatayo:
- Hali ya hewa: viwango vya joto na mvua; idadi ya miezi inayopats mvua kuanzia mm 60.
- Upatikanaji maji safi na ya uhakika (yasiyo na kiwango kikubwa cha fluoride)
- Kiwango cha rutuba udongoni.
- Kutokuwepo kwa magonjwa hatari (endemic) ya malaria na malale.
- Uzalishaji wa mazao ya chakula.
- Ufugaji.
- Uvuvi.
- Uzalishaji wa matunda.
View attachment 653183 View attachment 653184 View attachment 653185
Makabila yaliyopata wastani wa A, ni yafuatayo:
1: Wachaga
2: Wanyakyusa
3: Wahaya
4: Wakerewe
5: Wameru
6: Waarusha
7: Wazanzibar (Wapemba, Watumbatu & Wahadimu)
8: Wakara
9: Waluguru
10: Wakurya
11: Waha
12: Wabondei
13: Wajaluo
14: Wasambaa
15: Wavidunda
NB:
I: Maeneo yenye A ndiyo yenye kiwango cha juu cha ubora na D (E) ni kiwango cha mwisho.
II: Chumba cha mwisho kulia "
Ubora katika Uzalishaji" ndicho chenye wastani kwa kila kabila.
III: Kwa kuwa, kila Jamii ina maeneo yenye sifa tofauti, eneo (tarafa/kata/mji) lenye sifa nyingi ndilo lililochukuliwa kuwakilisha kabila husika. Kuna changamoto kwa baadhi ya jamii kuchagua mji/tarafa/kata ya kuwakilisha Jamii husika. Mfano: ushindani wa Kibosho, Marangu na Machame kwa uchagani. Hivyo nitafurahi sana kupata mrejesho wa masuala mengi, hasa kama kweli eneo nililochagua ni mwakilishi muafaka wa Kabila lako.
IV: Kuna maeneo yaliyoendelezwa miaka ya hivi karibuni (tangu kuja ukoloni) dhidi ya maeneo maarufu ya asili. Mfano kwa Wakwere, maeneo ya Chalinze, Mlandizi na Kibaha ni bora sana kwa sasa lakini hayakuwa hivyo kabla ya ukoloni. Eneo la Yombo linaonyesha kuwa na sifa zaidi.
V: Kuna vipengele vingine muhimu, sijaviingiza kwenye vigezo vya ushindani ili kupunguza taarifa kuwa more complex. Vigezo hivyo ni: kiwango cha Fluoride (fluorine); madini ya Iodine na ugonjwa wa schistosomiasis (bilharzia).
VI: Vyanzo vikuu vya Takwimu, ni pamoja na: Joshuaproject.net; en.climates-data.org; mapcarta.com; Aroundguides; Citypopulation.de; pamoja na Atlas nilizo nazo zipatazo tisa.
Nawasilisha wazee.