namwandele9
Member
- Jan 24, 2017
- 19
- 7
Mbeya kabila linalolima vyakula ni Wasafya na si Wanyakyusa wao walifanikiwa kusoma nashangaa hawapo hapo kabisa
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Hao jamaa wa Kaskazini wanasaidiwa sana na milima yake mirefu iliyojitenga na yenye uwezo wa ku-regulate mvua. Kijiografia kuna mvua za aina tatu: conventional; monsoon; na orographic (relief). Katika aina zote hizo za mvua, ya uhakika ni ya orographic kwa sababu yenyewe inanyesha eneo lenye milima pekee, kumbuka mambo ya windward na leeward kwenye some la jiografia. Sasa, Kaskazini kuna milima mingi iliyojitenga ambayo imeleta neema kubwa sana kwa watu wa huko kuweza kuwa na mvua za uhakika kwa mwaka mzima. Na kwa kuwa, eneo hilo lipo karibu na Ikweta, linapata mvua za aina mbili - za vuli na masika (bi-modal). Halafu milima hiyo ni ya volcano ambayo inatoa udongo wa kiwango kikubwa cha nutrients kuliko udongo wa aina yoyote duniani. Ndiyo maana maeneo yenye udongo huo, yana vyakula vitamu sana na vyenye afya. Hata makabila yanayoishi eneo hilo, nao wanafanikiwa kutokana na vyakula bora.Samahani tena...!!
Unaweza nuambia kwanini Wachagga wamekuwa wa kwanza kwa mambo mengi mazuri ndani ya nchi hii...???
Alafu pia nimefuatilia takwimu zako nimeona ukanda wa kaskazini mwa Tanzania umetoa makabila zaidi ndani ya 10 bora..!!!nini hasa Kisababishi/Vishababishi vikuu...????
Nitaongezea ili niweke makabila yote. Kwa taarifa yako kadri ya uchambuzi, Wasafwa wako namba 19. Vuta subira nita-display makabila yote, coz sikutaka bandiko liwe refu sana.Mbeya kabila linalolima vyakula ni Wasafya na si Wanyakyusa wao walifanikiwa kusoma nashangaa hawapo hapo kabisa
Kabila lako limepata FStupid
We bidada upo? Ulipotelea wapi?Hongera kwa hii topic umenifanya ni log in JF baada ya mda mrefu coz mada yako nzuri sana I hope to learn more from you honestly
Mazao mengine ni kama KARANGA, MUHOGO, MAHARAGE, KUNDE, ALIZETI,ULEZI,NJUGU KWA WINGI SANA, MTAMA AINA MBALI MBALI NA NDIZI KATIKA BAADHI YA MABONDE KAMA KULE KISANA.Sasa nadhani hukuelewa maana ya kijedwali kile cha vyakula. Simaanishi kulima chakula cha aina moja tu bali aina mbalimbali za vyakula. Kuna mazao makuu ya chakula nchini kama: ndizi, mpunga, mahindi, mihogo, viazi vitamu, viazi mviringo, viazi vikuu, ulezi, mtama, ngano, njegere, mbaazi, maharage, kunde na njugu mawe.
Sasa, niambie ni mazao mangapi yanayolimwa hapo Iramba halafu jitahidi kulinganisha na makabila mengine ambayo uliwahi kupata nafasi ya kutembelea. Linganisha na makabila mengine ya kati yasiyopata mvua ya kutosha hasa Wagogo, Wanyamwezi, Wasukuma, Wanyaturu, Waisanzu, Wagorowa, Warangi, Wasandawe, Wabulunge, Wadatooga na Wambulu, uone kama nimeionea Unyilamba halafu tusaidiane niweze kurekebisha penye makosa.
Ama linganisha ulimaji wa mazao hayo na makabila kama Wahaya, Waha, Wakurya, Wakerewe, Wachaga, Waluguru, Wasambaa na Wanyakyusa utaona utofauti kati ya kuivisha vyakula vya kutosha na vyakula vya aina nyingi vya kutosha.
Asante sana kwa swali zuri. Nilichagua Yombo siyo kwa sababu imeshaendelezwa bali nilifuatilia eneo lenye rutuba ya kutosha kulinganisha na maeneo mengine ya Wakwere. Yes, Mlandizi na Chalinze Biko kwenye mabonde so wamekuwa wakifaidika na kilimo cha mpunga but kule Yombo, Wakwere walioishi huko, ni lazima walikuwa wakilima mazao ya aina nyingi kuliko Mlandizi, Chalinze ama Kibaha ama Bagamoyo. Vilevile, uwepo wa Bahari karibu ulisaidia sana kuchagua Tarafa hiyo kwa kuwa ilikuwa inaweza ku-access samaki wabichi tofauti na Chalinze, Mlandizi na Kibaha ambayo iko mbali kuweza kupata samaki wabichi kipindi cha kabla ya kuja kwa magari, pikipiki wala baiskeli.Mazao mengine ni kama KARANGA, MUHOGO, MAHARAGE, KUNDE, ALIZETI,ULEZI,NJUGU KWA WINGI SANA, MTAMA AINA MBALI MBALI NA NDIZI KATIKA BAADHI YA MABONDE KAMA KULE KISANA.
Pia vigezo vyako havijazingatia eneo kisiasa, mfano huwezi kuwa na upimaji linganifu kwa miji, majiji na wilaya na uka conclude kuwa hawa wako na A au B au C. Kuna makabila mengine maeneo yao ya asili ndio palipata fursa ya kuwa makao makuu ya mkoa toka zamani sana na hivyo resource zikawekwa hapo na hata walioendeleza hayo maeneo sio watu wa asili ya pale tu na pengine wenye asili hata wameondoka kabisa. Mfano wakwere ni wangapi waliojenga na kupaendeleza YOMBO kama sio eneo lote limevamiwa na watu wa kuja??
Usihofu kuhusu hilo, hii takwimu nimeitoa kwenye mtandao mkubwa duniani wa joshuaproject.net. La muhimu fuatilia idadi ya wakazi wa mikoa ya Mwanza, Shinyanga, Simiyu na Geita kwa sensa ya mwaka 2012. Mikoa hiyo ilikuwa na wakazi zaidi ya milioni 7.3. Sasa fikiria kwa kasi ya ukuaji wa watu kwa mikoa hiyo yenye wastani wa zaidi ya asilimia 2.7%, watakuwa wangapi kwa sasa?Sina mashaka na kusudio lako LA hii takwimu ila mashaka yangu ni population ya wasukuma 7m hapo naona haiwezekani
Hilo nalo neno. Maneno kuntu hayo mzazi.Mimi nimevutiwa na effort iliyotumika kutengeneza hayo majedwali bila kutumia kompyuta!
Inanikumbusha mbali, lakini pia inanifikirisha sana juu ya dhana ya kujenga uchumi wa viwanda katika nchi yetu.
Hebu cheki ramani hiyo ya Tanzania ikionyesha idadi ya watu Sensa ya mwaka 1957.Mimi nimevutiwa na effort iliyotumika kutengeneza hayo majedwali bila kutumia kompyuta!
Inanikumbusha mbali, lakini pia inanifikirisha sana juu ya dhana ya kujenga uchumi wa viwanda katika nchi yetu.
Umetaja kama vile wachaga wote ni wa Kibosho?? Mbona hukufikiria wale wa Rombo, Machame au kule Marangu??Asante sana kwa swali zuri. Nilichagua Yombo siyo kwa sababu imeshaendelezwa bali nilifuatilia eneo lenye rutuba ya kutosha kulinganisha na maeneo mengine ya Wakwere. Yes, Mlandizi na Chalinze Biko kwenye mabonde so wamekuwa wakifaidika na kilimo cha mpunga but kule Yombo, Wakwere walioishi huko, ni lazima walikuwa wakilima mazao ya aina nyingi kuliko Mlandizi, Chalinze ama Kibaha ama Bagamoyo. Vilevile, uwepo wa Bahari karibu ulisaidia sana kuchagua Tarafa hiyo kwa kuwa ilikuwa inaweza ku-access samaki wabichi tofauti na Chalinze, Mlandizi na Kibaha ambayo iko mbali kuweza kupata samaki wabichi kipindi cha kabla ya kuja kwa magari, pikipiki wala baiskeli.
Ila kiukweli hakuna sehemu yoyote niliyoconsider maendeleo ya mji, angalia mfano Waluguru sikuchukua Morogoro ama Wachaga kwa Moshi, au Mwanza kwa Wasukuma, ama Wasambaa kwa Lushoto. Ni miji michache sana mikubwa ya mikoa imefanikiwa kuwakilisha eneo bora la kabila.
Ndiyo maana kwenye post yangu awali nilieleza wazi kupata changamoto hasa kati ya Kibosho na Marangu. Binafsi Mimi huwa napenda sana Marangu kuliko eneo lolote la uchagani na ndilo bonde lenye msongamano mkubwa wa watu kuliko eneo la uchagani.Umetaja kama vile wachaga wote ni wa Kibosho?? Mbona hukufikiria wale wa Rombo, Machame au kule Marangu??
Ndio maana naona Data zilizotumika sio Represenatative! Sampuli za aina hii zinakuwa na mashaka katika kuamua, maana inategemea tu wewe uliona wapi pameendelea zaidi kumbe population kubwa ipo mahali pengine ambapo bado hapajaendelezwa na bado wanawakikilisha population ya kabila husika.
Ipo tofauti kubwa tena sana katika maisha yetu ya tangu kuingia kwa formal education. Zamani kabla ya elimu hiyo ya darasani, wazee wetu walikuwa wakiturithisha elimu za mazingira tuliyokuwa tukitegemea kupata mahitaji yetu ya kila siku, hivyo walitufundisha kulima, kufuga na kuvua samaki kama shughuli kuu za kiuchumi. Hata hivyo, kutokana na kuja kwa elimu ya darasani, jamii zikaingizwa katika mfumo wa kupeleka watoto shuleni ambako wanafundishwa theory tangu darasa la kwanza hadi Chuo kikuu ili aitumie elimu hiyo. So, jamii zilizokuwa na watoto wenye kumbukumbu nzuri ndio zilifanikiwa kutoa wanafunzi wengi elimu za juu na hivyo kuneemeka kiajira na hence kimaisha.Ni nini faida kubwa ya ziada waliyonayo watu/jamii yenye ardhi au vyakula vingi na mvua nyingi au hali ya hewa iliyoitwa nzuri ?
Na ni mapungufu gani waliyonayo jamii yenye ardhi isiyo na rutuba au mvua nyingi,!!
Kuna relevance kwenye hzo faida na hasara NA hyo ardhi au Maeneo husika!!?
Ndiyo maana kwenye post yangu awali nilieleza wazi kupata changamoto hasa kati ya Kibosho na Marangu. Binafsi Mimi huwa napenda sana Marangu kuliko eneo lolote la uchagani na ndilo bonde lenye msongamano mkubwa wa watu kuliko eneo la uchagani.
But kilichofanya nichague Kibosho ni yafuatayo:
Nikiri wazi, ugumu wa kuchagua ndio ulichelewesha taarifa hii kwani awali nilikuwa nachambua vigezo hivi kwa Kuzbass eneo la Marangu. Hata hivyo, kwa taarifa yako, hata ningetumia Marangu, Kibosho, Machame ama Mkuu, ilijionyesha wazi, miji yote hiyo ingewakilisha vyema Wachaga na kuperform the way Kibosho imefanya kwa kuwa maeneo hayo yana sifa zinazofanana sana.
- Bonde la Kibosho na maeneo yanayoizunguka hasa Uru kuna mvua nyingi kuliko lile la Marangu.
- Bonde la Kibosho Lina mito mingi kuliko eneo lolote la uchagani.
- Bonde la Kibosho Lina mashamba ya mazao ya aina nyingi tofauti na Marangu ambako maeneo mengi yamefunikwa na migomba.
- Blonde la Kibosho ndilo lililo katikati ya uchagani ikiunganisha Wamachame na Wasiha kwa upande wa kulia dhidi ya Wavunjo na Warombo kwa upande wa kushoto, pamoja na mji wa Moshi, Himo na Wa-Kahe.
Pia kwa Wahaya, nilisumbuka sana kuamua upi wa kuwakilisha Wahaya kati ya Bukoba, Kamachumu, Kemondo Bay (Kanazi). Vilevile kwa Wapare (Ugweno vs Usangi); Wajaluo (Utegi vs Shirati); Wakurya (Tarime vs Sirari); ni. Ni maeneo machache sana ambako sikutumia nguvu ya ziada kuchagua ukanda.
Hata hivyo, uchambuzi huu una mambo mengi ya "arms-chair thinking" yaani siyo ya kwenda field, hivyo kuna possibility kubwa ya baadhi ya vigezo nimevi-exaggerate, hivyo kwa kuwa Wewe ni wazi ni mwenye ni wa uchagani, nakuomba pamoja na wengine wa uchagani na maeneo mengine nchini mnisaidie, ni ukanda upi kiasili (achana na maeneo ya mijini) ambako umekuwa ukizalisha mazao mengi na ya aina mbalimbali?