Kabila la kwanza hadi la mwisho nchini kwa ubora wa kiasili wa uzalishaji vyakula vyenye lishe nchini:

Kabila la kwanza hadi la mwisho nchini kwa ubora wa kiasili wa uzalishaji vyakula vyenye lishe nchini:

Orodha ya makabila kuanzia la kwanza hadi la mwisho katika kuwa na mazingira bora ya uzalishaji wa mazao, mifugo na samaki:
1: Wachaga
2: Wanyakyusa
3:Wahaya
4: Wakerewe
5: Wameru
5: Waarusha
6: Wazanzibar
7: Wakara
8: Waluguru
9: Wakurya
10: Waha
11: Wabondei
12: Wajaluo
13: Wasambaa
14:Wavidunda
16 Wandali
17: Wanyasa
18: Wapare
19: Wasafwa
20: Wamafia
21: Wabena
22: Wadigo
23: Wambulu
24: Wasukuma
25: Wapogoro
26: Wazinza
27: Wahehe
28: Wasuba
29: Wapangwa
30: Wambunga
31: Warufiji
32: Wajita
33: Wasagara
34: Waruri
35: Wamatengo
36: Wazanaki
37: Waikizu
38: Wahangaza
39: Wakinga
40: Wasangu
41: Wangurimi
42: Wanyiha
43: Wandamba
44: Wamakila
45:Wadatooga
46: Wafipa
47: Wamambwe-Lungu
48: Wanyaturu
49: Wanyilamba
50: Wamwera
51: Wangoni
52: Wazaramo
53: Wamasai
54: Walambya
55: Wasubi
56: Wakwere
57: Wamakonde
58: Wagogo
59: Wagorowa
60: Wabulunge
61: Wadengereko
62: Wamatumbi
63:Wanyamwezi
64: Wazigua
65: Wasumbwa
66: Wakagulu
67: Wanyamwanga
68: Wandendeule
69: Wamakua
70: Wangindo
71: Wayao
72: Wakutu
73: Wasandawe
74: Wakonongo
75: Wamachinga
76: Wakimbu
77: Wahadzabe.

Wahadzabe ndio kabila la mwisho kwa sababu ya kutokuwa na option kubwa ya vyakula kama makabila mengine. Vilevile, eneo wanaloishi ndio lenye mvua chache kabisa kuliko maeneo yote wanakoishi jamii nyingine.
Makabila mengine mengi madogo madogo, yatakuwa kwenye nafasi za katikati na zinazokaribiana na za majirani wao, mfano:
Wamanda kwa Wapangwa
Wakisi kwa Wapangwa
Wandonde kwa Wangindo
Wanyika kwa Wabungu (Wawungu) na Wawanda
Wawanda kwa Wabunge
Wabungu kwa Wawanda
Wambugwe kwa Wagorowa
Wambugu kwa Wasambaa
Wasegeju kwa Wadigo
Wadoe kwa Wazigua
Wakami kwa Wakisi
Wangasa na Wakahe kwa Wachaga
Wapimbwe, Wabende, Watongwe na Waholoholo kwa Wakonongo, etc.

Nawasilisha tena
 
Lkn kuna maeneo au mikoa yenye ardhi isiyo na rutuba na isiyopendeza au ku reflect hiyo Dhana:mikoa hiyo ina mvua kidogo na vyakula si vingi kulingana na data zako. Mfano,mkoa wa singida ina watu wenye uwezo wa akili na kumbukumbu nzuri, wanaojiamini na kujisimamia,hawa nao sababu ni nini!?

Lkn pia ardhi na hali ya hewa ya Lushoto- Tanga na ya Kigoma haitofautiani na mikoa hyo ya Kilimanjaro na Mbeya -Tukuyu. Lkn mikoa hyo ya Kigoma na Tanga (Lushoto ) haina wasomi au wenye elimu wengi (Formal Education )kama jamii/mikoa uliyoisema!! Sasa hawa walipatwa na nini kama ardhi, vyakula na hali ya hewa ni kigezo!?

Hata mvua na hali ya hewa ya Mara-Musoma, Ruvuma, Sumbawanga, Morogoro na Katavi siyo mbaya. Kwa mantiki yako Ingefaa kuwa na matokeo au mafanikio at least 75 percent ya jamii zile unazosema, walizipata sababu ya vyakula from good soil fertility na mvua toshelezi. Nako huko kuna mvua, hali ya hewa Karibia 75percent ya mikoa unayozingatia!!
Yes, unasema kweli, niliogopa kuweka alama za wastani kwa kila kabila, zingekuwa na bias kubwa ila kwa kuwa umeniwahi, nilipanga kusubiri kwanza mjadili ili baadaye niwaambie ukweli kuwa, vipimo vya hali ya hewa vimechukuliwa kwenye maeneo bora tu, hivyo kama Kabila Lina ukanda bora mdogo, basi haitareflect kwa usahihi ubora wa kabila hilo.
Mfano Mahenge ya Wapogoro, Bonga ya Wagorowa, Maramba ya Wadigo, Kiomboi ya Wanyilamba, Haubi ya Warangi, Ilongero ya Wanyaturu, ndivyo vilivyowabeba sana makabila yao, otherwise makabila hayo ndiyo yasingepata pointi nyingi kwenye kutokana na maeneo mengine kuwa na mazingira mabaya ya uzalishaji chakula.
Hilo la kutoa wasomi tutajadili later on.
 
Tangu kuingia kwa wageni nchini Tanzania hasa kuanzia kipindi cha wakoloni miaka ya 1880s hadi leo, kumekuwepo mabadiliko makubwa ya uingilianaji wa watu kutoka jamii/koo tofauti tofauti kutokana na mabadiliko yanayoletwa na maendeleo hasa ukuaji wa miji na kuimarika kwa miundombinu ya usafiri. Hali hii imesababisha mazao yanayolimwa upande mmoja wa nchi, kufikika kwa urahisi sehemu ya mbali. Mfano: leo hii sato wabichi (tilapia) wa Ziwa Victoria wanauzwa jijini Dar es Salaam kutokana na uwepo wa barafu na majokofu lakini zamani waliishia eneo la mwambao wa Ziwa ndani ya wastani wa km 15. Watu wa maeneo jirani na Ziwa umbali wa iliko kwa sasa miji kama Geita, Utegi, Bunda, Sengerema na Kamachumu, hawakuwa na uwezo wa kula samaki wabichi kwa kuwa, hakukuwepo hata baiskeli kipindi hicho zaidi ya kusafirisha kwa miguu.
Katika mazingira hayo, vyakula vilivyokuwa vikizalishwa na Kabila husika, viliishia kwenye Jamii hiyo kutokana na kutokuwepo mwingiliano wa kutosha wa watu wa makabila tofauti kipindi hicho pamoja na ukosefu wa usafiri. Hivyo, kama kabila lilikuwa linazalisha vyakula vya kutosha, vilisaidia tu jamii hiyo huku jamii ambayo iliishi maeneo yasiyozalisha chakula kwa wingi, ikiteseka yenyewe kutokana na mahusiano ya kishindani na ya kuogopana kati ya jamii na jamii.
Ifuatayo ni orodha ya makabila yote makubwa na maarufu nchini Tanzania, yakiwa na na uchambuzi wa masuala yafuatayo:
  • Hali ya hewa: viwango vya joto na mvua; idadi ya miezi inayopata mvua kuanzia mm 60.
  • Upatikanaji maji safi na ya uhakika (yasiyo na kiwango kikubwa cha fluoride)
  • Kiwango cha rutuba udongoni.
  • Kutokuwepo kwa magonjwa hatari (endemic) ya malaria na malale.
  • Uzalishaji wa mazao aina nyingi ya chakula.
  • Ufugaji.
  • Uvuvi.
  • Uzalishaji wa matunda.
View attachment 653183 View attachment 653184 View attachment 653185

Makabila yaliyopata wastani wa A, ni yafuatayo:
1: Wachaga
2: Wanyakyusa
3: Wahaya
4: Wakerewe
5: Wameru
6: Waarusha
7: Wazanzibar (Wapemba, Watumbatu & Wahadimu)
8: Wakara
9: Waluguru
10: Wakurya
11: Waha
12: Wabondei
13: Wajaluo
14: Wasambaa
15: Wavidunda

NB:
I: Maeneo yenye A ndiyo yenye kiwango cha juu cha ubora na D (E) ni kiwango cha mwisho.
II: Chumba cha mwisho kulia "Ubora katika Uzalishaji" ndicho chenye wastani kwa kila kabila.
III: Kwa kuwa, kila Jamii ina maeneo yenye sifa tofauti, eneo (tarafa/kata/mji) lenye sifa nyingi ndilo lililochukuliwa kuwakilisha kabila husika. Kuna changamoto kwa baadhi ya jamii kuchagua mji/tarafa/kata ya kuwakilisha Jamii husika. Mfano: ushindani wa Kibosho, Marangu na Machame kwa uchagani. Hivyo nitafurahi sana kupata mrejesho wa masuala mengi, hasa kama kweli eneo nililochagua ni mwakilishi muafaka wa Kabila lako.
IV: Kuna maeneo yaliyoendelezwa miaka ya hivi karibuni (tangu kuja ukoloni) dhidi ya maeneo maarufu ya asili. Mfano kwa Wakwere, maeneo ya Chalinze, Mlandizi na Kibaha ni bora sana kwa sasa lakini hayakuwa hivyo kabla ya ukoloni. Eneo la Yombo linaonyesha kuwa na sifa zaidi.
V: Kuna vipengele vingine muhimu, sijaviingiza kwenye vigezo vya ushindani ili kupunguza taarifa kuwa more complex. Vigezo hivyo ni: kiwango cha Fluoride (fluorine); madini ya Iodine na ugonjwa wa schistosomiasis (bilharzia).
VI: Vyanzo vikuu vya Takwimu, ni pamoja na: Joshuaproject.net; en.climates-data.org; mapcarta.com; Aroundguides; Citypopulation.de; pamoja na Atlas nilizo nazo zipatazo tisa.

Nawasilisha wazee.
Hongera kwa utafiti wako
 
Mtoa mada ndo wakufungwa na kugongwa viboko kama alivyosema mh rais.
Analeta takwimu za mfukoni na kichwani mwake kudanganya umma
 
Kwa mantiki nyingine, binadamu anavyoweza kuonyesha uwezo wake wa akili kwa memories, thinking ability,uwezo wa kujifunza, perception, kufanya maamzi, kuamini na kujiamini, uwezo wa kutambua na kutenda mema na mabaya,na hata anavyoipokea dunia na tabia zake na kila hali anayoonyesha binadamu haitegemei tu mazingira kwa maana ya hali ya hewa km mvua, joto, rutuba ya ardhi nk.

Binadamu pia uwezo wake na kila anachoonyesha na kujidhihisha kama nilivyoeleza hapo juu hutegemea pia GENETICS INHERITANCE! Yaani urithi kutoka kwa wazazi na vizazi na vizazi! Jinsi tunavyorithi sura na umbo kutoka kwa vizazi na vizazi, ndivyo tunavyorithi uwezo wa akili na tabia!

Kwa hyo kila hali ya kiakili na kitabia ya binadamu yeyote ni matokeo ya URITHI na MAZINGIRA.
 
Uchambuzi huu umetokana na kutumia vyanzo vingi ambavyo nimevitaja mwanzoni mwa bandiko hili. Tofautisha kutoa takwimu na kuchambua takwimu. Nitendee haki ndugu, vitu nilivyoongea siyo vya sayansi kwamba moja kujumlisha moja ni mbili, so kwa kuwa nimepost vitu vya ki-social, ni wazi siyo kila mtu atakubaliana nao kama ambavyo mambo yote yasiyo ya kisayansi/kitakwimu huwa yanapata waungaji na wakosoaji.
 
Unaandika thesis unataka tukusaidie...nyambafu.
Sijaamua ndugu yangu but nina uhakika kwa stage niliyofikia, nikiamua iwe hivyo nina uhakika imekamilika kwa mambo mengi. Hata hivyo, haja yangu ni kupanua mjadala wa masuala magumu yanayoendelea duniani, ambayo kimakosa huwa tunaya-perceive ndivyo sivyo.
 
Kwa mantiki nyingine, binadamu anavyoweza kuonyesha uwezo wake wa akili kwa memories, thinking ability,uwezo wa kujifunza, perception, kufanya maamzi, kuamini na kujiamini, uwezo wa kutambua na kutenda mema na mabaya,na hata anavyoipokea dunia na tabia zake na kila hali anayoonyesha binadamu haitegemei tu mazingira kwa maana ya hali ya hewa km mvua, joto, rutuba ya ardhi nk.

Binadamu pia uwezo wake na kila anachoonyesha na kujidhihisha kama nilivyoeleza hapo juu hutegemea pia GENETICS INHERITANCE! Yaani urithi kutoka kwa wazazi na vizazi na vizazi! Jinsi tunavyorithi sura na umbo kutoka kwa vizazi na vizazi, ndivyo tunavyorithi uwezo wa akili na tabia!

Kwa hyo kila hali ya kiakili na kitabia ya binadamu yeyote ni matokeo ya URITHI na MAZINGIRA.
Wewe umeniwahi kuongelea jambo ambalo sikutaka kuligusia kwanza. Ninajua wazi kuwa intelligence ni kazi ya inheritance zaidi kuliko hata mazingira, ndiyo maana nimetumia makabila na siyo kutumia mipaka ya kiutawala kwa sababu ninajua watu waliomo kwenye Kabila wana-share historia moja hence wana ufanano mkubwa katika uwezo wao bila kuja like kama wanaishi eneo bora ama siyo bora.
Hata hivyo kwa sababu kila kabila linaundwa na dialects, pamoja na clans, hivyo kila kabila Lina clans ambazo ni more intelligence kuliko nyingine. Sababu ya utofauti huo ni nyingi lakini asilimia kubwa inatokana eneo ambalo ukoo huo ukienda zaidi. Jaribu kufikiria kwenye kabila lako utapata jibu. Sababu nyingine ya koo fulani kuwa more bright ndani ya kabila ni aina ya clans ama kabila lingine wanalopakana nalo.
Waha wa Buhigwe hasa kuanzia Manyovu, Mnanira hadi Nganda, ukiacha ubora wa eneo lao bado wamefaidika sana na ukaribu wa Warundi who more brighter, the same kwa Wahangaza na wakimbizi wa Rwanda na Burundi.
Vilevile, Wandali wa mpakani na Rungwe are inherently more brighter than wa mpakani na Malawi.
So, nina vitu vingi kwenye genetics niliogopa kuviweka visije kuchanganya watu, Ndiyo maana taarifa hii imejifunga haiongelei intelligence kwa kuwa najua kipengele asili ya nasaba za mtu (genetics) sijaziweka.
Ndiyo hiyo niliyokuwa nikisema nitaandaa more comprehensive ambayo itacombine na vigezo vya vinasaba kuanzia kwa wale wenye vinasaba vya Semites, Hamites, Nilotes, Bantu na San.
 
Wahehe wangoni wamatengo mbona hatumo au hujaenda kilolo pawaga mbinga mufindi
Shida ya uchambuzi wangu, nimetumia elimu ndogo yangu na sijatembelea maeneo yoyote kwa ajili ya kufanya uchunguzi huu bali nimetumia ufahamu wangu wa Nchi yetu kwani tangu shule za msingi nilikuwa na hobby kubwa ya kusoma Atlas. Hata hivyo nimewahi kuishi Mwanza, Shinyanga, Tabora, Iringa na Dar es Salaam. Nimewahi kufika Arusha, Mbeya, Morogoro, Singida, Dodoma, Mara, Geita na Simiyu. Nimewahi kupita Pwani, Tanga, Kilimanjaro, Manyara na Njombe.
So nimeshaona maeneo mengi na nimejirahidi kutumia vyanzo vingi. But kwa kuwa nchi yetu ni kubwa, bado kuna errors nyingi ambazo kupitia mawazo yenu na jitihada zangu za kuendelea kusoma nitazirekebisha.
 
Lishe bora hupelekea akili inayofanya kazi... Je, wapo hivyo?
Sure, wapo hivyo. Waluguru katika makabila yote ya Mashariki ya Tanzania, ndio wanaongoza wakiwa at par na Wabondei na wakikaribiana na Wasambaa.
 
Umechanganya madawakibaohalafu swalilangu la msingihujajibu.

Unatumia kipimo gani kusema huyu ni kabila fulani?

Maana unaweza kusema Mwalimu Nyerere ni Mzanaki, kwa sababu Baba yake Chifu Burito ni Mzanaki,kumbe Chifu Burito wala si Baba yake Mwalimu Nyerere.

Mama Mgaya alikimbia kutokacourt ya Chifu Burito,akakimbilia kusini kuelekea Mwanza,hukoakakutana na Msukuma, akatunga mimba ya Mwalimu Nyerere, halafu baada ya muda,akarudi kwa Chief Burito.

Na Chifu Burito alivyokuwa na wake wengi hata hakujua. Na zaidimila zao hazihesabu mtoto kwa baba, zinahesabu mtoto kwa mama na mjomba.

Sasa wewe unapimaje kabila?

Unatumia DNA?
Senseless question!
 
Wamasai umeandika wapo 300,000 wakati kwa mwaka 2011 walikuwa zaidi ya laki nane.

Mhmhmh!.
Haya mambo ya takwimu, mnatakiwa muwakilishe NBS ya Tanzania ili waipitishe na kuangalia mapungufu, tofauti na apo ni kuichanganya jamii
 
Sasa Wakwaya na Wajita wanakosaje A wakati wako kandokando ya Ziwa na pia ni wakulima hodari?
 
Masatujr1985;
Kukosekana kwa wajita na wakwaya ilikua inanipa shida sana kwenye mada hii; mimi ni mvuvi ninayeishi Shirati-Mara; wenda mtoa mada anaweza kutuambia kwanini hajawapa wajita na wakwaya A wakati wanaishi mwambao wa ziwa?
 
Back
Top Bottom