Kabila la kwanza hadi la mwisho nchini kwa ubora wa kiasili wa uzalishaji vyakula vyenye lishe nchini:

Kabila la kwanza hadi la mwisho nchini kwa ubora wa kiasili wa uzalishaji vyakula vyenye lishe nchini:

Lishe bora hupelekea akili inayofanya kazi... Je, wapo hivyo?
Yes, sema kwa muktadha upi ama unawalinganisha na akina nani? Hata hivyo bila shaka kwa Ukanda wote wa Pwani na Mashariki ni Wasambaa pekee wa kuwatambia Waluguru. Nadhani niko right but niko tayari kwa criticism coz kuna vitu nitajifunza kwenu.
 
Haya mambo ya takwimu, mnatakiwa muwakilishe NBS ya Tanzania ili waipitishe na kuangalia mapungufu, tofauti na apo ni kuichanganya jamii
NBS ni ngumu kukubali uchambuzi, wao wako focused sana kwenye data na uchambuzi wamewaachia walaji wa taarifa zenyewe.
Kumbuka ndugu, mwanzoni kitu kipya huwa kinaleta upinzani but as time goes on, kitu kitaanza kueleweka.
Ngojeni nikiendelea kuupanua huu mjadala maana sooner or later nitawawekea uchambuzi kwa nchi tano za Afrika Mashariki - Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda na Burundi.
 
Hivi kwanini wanyakyusa wanajifanya wapo juu sana japo mkoa wa Mbeya sio wao.??

Mnapataje A mbele ya Wasafwa.??

Yani Tukuyu kuzuri na kuna hali ya hewa nzuri kuliko Uporoto..
Na vyakula gani wanavyo produce vizuri zaidi ya Wasafwa..

I May Be Hitler One Day..
 
Sasa Wakwaya na Wajita wanakosaje A wakati wako kandokando ya Ziwa na pia ni wakulima hodari?
Sawa, shida ya Wakwaya na Wajita kama yalivyo maeneo karibia yote ya Kanda ya Ziwa, hayana udongo wenye rutuba ya kutosha na inayoweza kukaa na unyevunyevu muda mrefu, huku mvua zake hasa zile muhimu sana kwenye kilimo za vuli, haziaminiki (unreliable) licha ya kuwa na miezi mingi inayopata mvua zaidi ya mm 60 kwa mwezi.
Ukanda huo wa Waruri na Wajita unasumbuliwa na malaria na it's endemic (iko damuni), hivyo ndiyo maana nilikuwa nazipunguzia pointi.
Vilevile, licha ya kutoa A, eneo la maji ya Ziwa Victoria upande wa Waruri na Wajita, siyo rich sana kwa samaki historically kwa sababu, upepo unaovuma kutokea eneo la Ukuryani (Tarime) badala ya kupuliza kuja nchi kavu, huwa unapuliza kutoka nchi kwenda majiji na hivyo samaki hawavutiwi kutembelea eneo hilo.
Niko tayari kwa kujadili zaidi.
 
Ndugu unajua kinachosababisha mwanadamu awe na afya nzuri ni chakula chenye lishe, pamoja na kutokuwepo kwa magonjwa. Sasa kama umesoma jiografia utagundua kuwa vyakula vinasitawi vizuri sana kwenye maeneo yenye hali nzuri ya hewa - yaani mvua nyingi (hasa mm 1500 - 2000) na joto la kadri; udongo wenye rutuba na kutokuwepo kwa magonjwa hatari.
Kwenye hali ya hewa (mvua nyingi na joto la kadri) nchini, Miteremko ya Kilimanjaro inazidiwa na Rungwe na Bukoba pekee. Hata hivyo Miteremko hiyo inaizidi Rungwe na Bukoba kwa sababu kuna hali za hewa nyingi ndani ya eneo dogo linaloweza kuivisha mazao ya kila aina yanayoweza kuhimili baridi kali, ya kawaida, joto la wastani hadi joto jingi, pamoja na mvua nyingi sana (zaidi ya mm 1700 - Uri) nyingi (1500 - Marangu) ya kawaida (mm 1100 Siha) na chache (mm 800 - Mossi) na pakame kabisa (mm 500 - Kahe).
Eneo lote kuanzia Uri (mm 1700) hadi Kahe (mm 500) ni chini ya km 20. Huu ni umbali mdogo sana lakini ume-cover hali zote za hewa za Tanzania, hivyo kila zao linalolimwa hapa Tanzania linalimika kwenye Miteremko ya Kilimanjaro. Aidha, utofauti wa mwinuko (altitudes/relief) kati ya makazi ya juu kabisa (Marangu Magharibi mita 1800) hadi chini kabisa Kahe (mita 800) ni mita 1000. Hakuna sehemu nyingine barani Afrika yenye eneo lenye tofauti kubwa ya mwinuko kama huo ndani ya umbaliwa wastani wa km 20 tu.
Hiyo ni kitu kikubwa sana.
we jamaa Unajua kabisa[emoji106] [emoji106] [emoji106] [emoji106] [emoji122] [emoji122] [emoji122] [emoji122] [emoji122]
 
Tangu kuingia kwa wageni nchini Tanzania hasa kuanzia kipindi cha wakoloni miaka ya 1880s hadi leo, kumekuwepo mabadiliko makubwa ya uingilianaji wa watu kutoka jamii/koo tofauti tofauti kutokana na mabadiliko yanayoletwa na maendeleo hasa ukuaji wa miji na kuimarika kwa miundombinu ya usafiri. Hali hii imesababisha mazao yanayolimwa upande mmoja wa nchi, kufikika kwa urahisi sehemu ya mbali. Mfano: leo hii sato wabichi (tilapia) wa Ziwa Victoria wanauzwa jijini Dar es Salaam kutokana na uwepo wa barafu na majokofu lakini zamani waliishia eneo la mwambao wa Ziwa ndani ya wastani wa km 15. Watu wa maeneo jirani na Ziwa umbali wa iliko kwa sasa miji kama Geita, Utegi, Bunda, Sengerema na Kamachumu, hawakuwa na uwezo wa kula samaki wabichi kwa kuwa, hakukuwepo hata baiskeli kipindi hicho zaidi ya kusafirisha kwa miguu.
Katika mazingira hayo, vyakula vilivyokuwa vikizalishwa na Kabila husika, viliishia kwenye Jamii hiyo kutokana na kutokuwepo mwingiliano wa kutosha wa watu wa makabila tofauti kipindi hicho pamoja na ukosefu wa usafiri. Hivyo, kama kabila lilikuwa linazalisha vyakula vya kutosha, vilisaidia tu jamii hiyo huku jamii ambayo iliishi maeneo yasiyozalisha chakula kwa wingi, ikiteseka yenyewe kutokana na mahusiano ya kishindani na ya kuogopana kati ya jamii na jamii.
Ifuatayo ni orodha ya makabila yote makubwa na maarufu nchini Tanzania, yakiwa na na uchambuzi wa masuala yafuatayo:
  • Hali ya hewa: viwango vya joto na mvua; idadi ya miezi inayopata mvua kuanzia mm 60.
  • Upatikanaji maji safi na ya uhakika (yasiyo na kiwango kikubwa cha fluoride)
  • Kiwango cha rutuba udongoni.
  • Kutokuwepo kwa magonjwa hatari (endemic) ya malaria na malale.
  • Uzalishaji wa mazao aina nyingi ya chakula.
  • Ufugaji.
  • Uvuvi.
  • Uzalishaji wa matunda.
View attachment 653183 View attachment 653184 View attachment 653185

Makabila yaliyopata wastani wa A, ni yafuatayo:
1: Wachaga
2: Wanyakyusa
3: Wahaya
4: Wakerewe
5: Wameru
6: Waarusha
7: Wazanzibar (Wapemba, Watumbatu & Wahadimu)
8: Wakara
9: Waluguru
10: Wakurya
11: Waha
12: Wabondei
13: Wajaluo
14: Wasambaa
15: Wavidunda

NB:
I: Maeneo yenye A ndiyo yenye kiwango cha juu cha ubora na D (E) ni kiwango cha mwisho.
II: Chumba cha mwisho kulia "Ubora katika Uzalishaji" ndicho chenye wastani kwa kila kabila.
III: Kwa kuwa, kila Jamii ina maeneo yenye sifa tofauti, eneo (tarafa/kata/mji) lenye sifa nyingi ndilo lililochukuliwa kuwakilisha kabila husika. Kuna changamoto kwa baadhi ya jamii kuchagua mji/tarafa/kata ya kuwakilisha Jamii husika. Mfano: ushindani wa Kibosho, Marangu na Machame kwa uchagani. Hivyo nitafurahi sana kupata mrejesho wa masuala mengi, hasa kama kweli eneo nililochagua ni mwakilishi muafaka wa Kabila lako.
IV: Kuna maeneo yaliyoendelezwa miaka ya hivi karibuni (tangu kuja ukoloni) dhidi ya maeneo maarufu ya asili. Mfano kwa Wakwere, maeneo ya Chalinze, Mlandizi na Kibaha ni bora sana kwa sasa lakini hayakuwa hivyo kabla ya ukoloni. Eneo la Yombo linaonyesha kuwa na sifa zaidi.
V: Kuna vipengele vingine muhimu, sijaviingiza kwenye vigezo vya ushindani ili kupunguza taarifa kuwa more complex. Vigezo hivyo ni: kiwango cha Fluoride (fluorine); madini ya Iodine na ugonjwa wa schistosomiasis (bilharzia).
VI: Vyanzo vikuu vya Takwimu, ni pamoja na: Joshuaproject.net; en.climates-data.org; mapcarta.com; Aroundguides; Citypopulation.de; pamoja na Atlas nilizo nazo zipatazo tisa.

Nawasilisha wazee.
Unajua Kabisa, Upewe PhD 2[emoji106] [emoji106] [emoji106] [emoji106] [emoji122] [emoji122]
 
Hivi kwanini wanyakyusa wanajifanya wapo juu sana japo mkoa wa Mbeya sio wao.??

Mnapataje A mbele ya Wasafwa.??

Yani Tukuyu kuzuri na kuna hali ya hewa nzuri kuliko Uporoto..
Na vyakula gani wanavyo produce vizuri zaidi ya Wasafwa..

I May Be Hitler One Day..
Mzee hakuna haja ya kuhofia hilo kwani ni kweli udongo wa Milima ya Uporoto nao una rutuba kwa kuwa ni wa Volcano. Hata hivyo content ya rutuba iliyomo uporoto haifikii ya Mlima Rungwe. Hata hivyo, sababu kubwa ya kuachwa na Wanyakyusa iko kwenye hali ya hewa. Angalia idadi ya miezi ambayo mnapata mvua zenye mm 60 kwa mwezi (chini ya kiwango hicho ni ukame). Mnapata mvua nyingi but inaisha mapema. Hata hivyo tatizo mingine kubwa ni baridi kubwa (centigrade 17) kuliko kiwango kinachovumiliwa na baadhi ya mazao kama migomba. Huko kwa Wanyakyusa wana sifa nyingi, cheki ile jedwali.
Hata hivyo inawezekana Mimi ndiye nimekosea kuchagua mji wa kuwawakilisha Wasafwa na nikiri nilisumbuka sana maana swali nilichagua Mbalizi, nikabadilisha nikachukua Iyula, baadaye ndiyo nikaamua iwe Uyole, so ni uamuzi ambao niliu-annalyse kwa muda sana. Kati ya Mbeya, Uyole, Mbalizi, ama Inyala ni wapi wanaivisha mazao ya aina nyingi hasa migomba?
Anyway kwa kuwa, bado haijakamilka moja kwa moja, nitarevise tena kuangalia baadhi ya vigezo kama nilivi-overlook.
 
Kwa nini usingefanya utafiti kiwiliaya kuliko kufanya kikabila?
 
Masatujr1985;
Kukosekana kwa wajita na wakwaya ilikua inanipa shida sana kwenye mada hii; mimi ni mvuvi ninayeishi Shirati-Mara; wenda mtoa mada anaweza kutuambia kwanini hajawapa wajita na wakwaya A wakati wanaishi mwambao wa ziwa?
Nimekuwa nikisikia watu wengi wakitaja makabila yaliyoko kwenye mwambao wa Ziwa ama bahari kuwa na akili sana lakini wamekuwa hawajiulizi hali ya hewa ya maeneo hayo yaliyoko kandokando ya Ziwa. Hata hivyo makabila yote ya mwambao wa Ziwa yanayotajwa kwa akili za darasani, haitokani na samaki pekee bali Hana hali nzuri ya hewa, halafu ndiyo yanaongezea ya kuwa na samaki. Angalia mvua yanayopata makabila ya kati kati na Kaskazini mwa Ziwa Victoria - Wahaya (2000), Wakerewe (mm 1500) na Wakara (1500), halafu tofautisha na makabila yaliyoko Kusini na Mashariki ya Ziwa Victoria - Wasukuma, Wajita, Waruri (Wakwaya), Wasuba wanaopata chini ya mm 1000, huku Wajaluo na Wazinza pekee ndio wanapata angalao mm 1100 kwa mwaka.
So uhakika na ubora wa chakula ndio kigezo cha kwanza kabla mboga (samaki ama nyama) yenye virutubisho ndiyo inafuatia. Fikiria Wakurya hakuna Ziwa, ama Wazanaki but najua unaelewa uwezo wao kwa Mkoa huo wa Mara.
 
Kwa nini usingefanya utafiti kiwiliaya kuliko kufanya kikabila?
Kiwilaya isingewezekana kwani uchunguzi wangu huu kuna kipengele cha muhimu sana sijakiweka - genetics na ndicho kitakamilisha ukamilifu wa kabila husika.
Nikitumia wilaya ina kuwa ngumu kwa kuwa watu wana asili tofautitofauti but kwa Kabila, hata kama mtu haishi hapo, asili ya kabila yake itamfuata popote alipo. Hivyo Mgogo anayeishi Ulaya, atachambuliwa kwa vigezo vya sifa za ardhi ya mabavu zake kwa kuwa ukamilifu wa Kabila imetokana na kujibu na kwa miaka mingi.
Ulishawahi kujiuliza Waafrika walioko Ulaya ama Marekani nao wana-perform huko mashuleni kulingana na uwezo hali si was asili ya makabila yao? Fuatilia Waigbo huko a Ulaya na Amerika utapata jibu.
Kwa nini wazungu wa kireno walioko Afrika bado ni masikini kuliko wenye asili ya kiingereza? Fuatilia vyema suala hilo polepole.
 
Mzee hakuna haja ya kuhofia hilo kwani ni kweli udongo wa Milima ya Uporoto nao una rutuba kwa kuwa ni wa Volcano. Hata hivyo content ya rutuba iliyomo uporoto haifikii ya Mlima Rungwe. Hata hivyo, sababu kubwa ya kuachwa na Wanyakyusa iko kwenye hali ya hewa. Angalia idadi ya miezi ambayo mnapata mvua zenye mm 60 kwa mwezi (chini ya kiwango hicho ni ukame). Mnapata mvua nyingi but inaisha mapema. Hata hivyo tatizo mingine kubwa ni baridi kubwa (centigrade 17) kuliko kiwango kinachovumiliwa na baadhi ya mazao kama migomba. Huko kwa Wanyakyusa wana sifa nyingi, cheki ile jedwali.
Hata hivyo inawezekana Mimi ndiye nimekosea kuchagua mji wa kuwawakilisha Wasafwa na nikiri nilisumbuka sana maana swali nilichagua Mbalizi, nikabadilisha nikachukua Iyula, baadaye ndiyo nikaamua iwe Uyole, so ni uamuzi ambao niliu-annalyse kwa muda sana. Kati ya Mbeya, Uyole, Mbalizi, ama Inyala ni wapi wanaivisha mazao ya aina nyingi hasa migomba?
Anyway kwa kuwa, bado haijakamilka moja kwa moja, nitarevise tena kuangalia baadhi ya vigezo kama nilivi-overlook.
Uwage unauliza sasa..

jibu ni KAWETELE..
 
Uwage unauliza sasa..

jibu ni KAWETELE..
Mimi nilidhani unalalamikia kuhusu Wasafwa? Sasa mbona unatoa eneo la Tukuyu kwa Wanyakyusa? Nilitaka wewe unipe alternative na eneo la Uyole kwani ulidai nimelionea, but kwa Tukuyu, Hilo ni eneo nililo na uhakika nalo kwa asilimia 100%. Hata hivyo naona umechukua kata moja tu wakati Tukuyu ina kata tatu, so hakuna shida la muhimu ni kuangalia ukanda zaidi na siyo mtaa ama kijiji.
 
IMG_0681.JPG



IMG_0680.JPG



IMG_0678.JPG



IMG_0679.JPG

Ninaposema umuhimu wa vyakula ndio huu. Kila chakula hata kama kiasili ni kitamu, kitazidiana utamu na ubora wake kutoka sehemu moja hadi nyingine.

Hebu chekini hao samaki mseme kila kundi wanaweza kuwa wamevuliwa eneo (kabila) gani la Ziwa ama kwenye maji ya aina (yenye virutubisho vingi/vichache) gani? Ni kundi lipi la samaki katika picha hiyo ndio watamu zaidi na why?
 
IMG_2761.JPG
IMG_2763.JPG



IMG_2770.JPG

IMG_2765.JPG


Angalieni pia mifano ya ng'ombe hawa, aina ya Ankole (Tusi) wanaopatikana eneo la Interlacustrine (ama Ziwa Makuu) ukiwemo Mkoa wa Kagera dhidi ya aina ya Zebu wanaopatikana maeneo mengine nchini.
Ni wapi watamu? Kwa nini Ankole wana bei kubwa kuliko Zebu?
 
So wale samaki (tilapia) kama weusi kwenye picha walioko chini wanastawi tu kwenye ukanda wa Ziwa wenye virutubisho vingi (planktons). Maeneo hayo mara kwa mara ni yale yanayopata mvua nyingi ama ambayo mito inaingia ziwani. So mlio na asili ya maziwa na hata mito fuatilieni kwa upande wenu kulinganisha. Wale wekundu siyo watamu sana level ya wale wa chini.
 
Back
Top Bottom