Nashukuru sana kwa kufuatilia vyema. Changamoto niliyoipata ni kuelewa kama Ziwa dogo kama hilo limekuwa na samaki so nitaiconsider kwenye taarifa mpya.
Hata hivyo kwenye uzalishaji wa vyakula, nimewapa Wanyilamba D kwa sababu wana alternative ndogo sana ya kuliwa mazao ya vyakula kutokana na kuwa na mzima mfupi wa kilimo. Kwa kuwa eneo hilo linapata mvua chache (chini ya mm 850), limekuwa na rainfall unreliability, hivyo wanaweza kuzalisha vyakula kwa wingi but still njaa imekuwa ya mara kwa mara kulinganisha na maeneo yenye misimu mirefu ya mvua.
Mfano: mwezi unaopata mvua chini ya mm 60 kwa mwezi basi ni mwezi wenye ukame na ikiwa ni mm 30 ni ukame mkubwa, so angalia nimechukua eneo bora la Kionboi but still wana miezi sita pekee ya mvua isiyo ya ukame. Huwezi kulinganisha na maeneo yenye bi-modal.