Mgambilwa ni mntu
JF-Expert Member
- May 30, 2017
- 2,869
- 3,187
- Thread starter
- #61
Sijawasahau mzee. Mbona wamefanikiwa kwenye baadhi ya vigezo mfano ufugaji na samaki? Icheki vizuri ndugu.Wasukusu umetusahau eeeh acha mambo yako ww
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Sijawasahau mzee. Mbona wamefanikiwa kwenye baadhi ya vigezo mfano ufugaji na samaki? Icheki vizuri ndugu.Wasukusu umetusahau eeeh acha mambo yako ww
Hapo ndipo huwa siwaelewi wanatakwimu. Kuna maeneo yana mvua mara 2 lakini kwa muda mfupi mfupi tu ambao mahindi ya miezi miwili hupata shida kufika. Iramba ina mvua ya nusu mwaka na hakika sijawahi kuona Iramba mahindi yasifike/yasikomae mpaka kuvuna huku Maeneo mengine kama Dodoma, Shinyanga kukiwa na miaka ambapo hawavuni kabisa mazao kama mahindi.Nashukuru sana kwa kufuatilia vyema. Changamoto niliyoipata ni kuelewa kama Ziwa dogo kama hilo limekuwa na samaki so nitaiconsider kwenye taarifa mpya.
Hata hivyo kwenye uzalishaji wa vyakula, nimewapa Wanyilamba D kwa sababu wana alternative ndogo sana ya kuliwa mazao ya vyakula kutokana na kuwa na mzima mfupi wa kilimo. Kwa kuwa eneo hilo linapata mvua chache (chini ya mm 850), limekuwa na rainfall unreliability, hivyo wanaweza kuzalisha vyakula kwa wingi but still njaa imekuwa ya mara kwa mara kulinganisha na maeneo yenye misimu mirefu ya mvua.
Mfano: mwezi unaopata mvua chini ya mm 60 kwa mwezi basi ni mwezi wenye ukame na ikiwa ni mm 30 ni ukame mkubwa, so angalia nimechukua eneo bora la Kionboi but still wana miezi sita pekee ya mvua isiyo ya ukame. Huwezi kulinganisha na maeneo yenye bi-modal.
Sasa nadhani hukuelewa maana ya kijedwali kile cha vyakula. Simaanishi kulima chakula cha aina moja tu bali aina mbalimbali za vyakula. Kuna mazao makuu ya chakula nchini kama: ndizi, mpunga, mahindi, mihogo, viazi vitamu, viazi mviringo, viazi vikuu, ulezi, mtama, ngano, njegere, mbaazi, maharage, kunde na njugu mawe.Hapo ndipo huwa siwaelewi wanatakwimu. Kuna maeneo yana mvua mara 2 lakini kwa muda mfupi mfupi tu ambao mahindi ya miezi miwili hupata shida kufika. Iramba ina mvua ya nusu mwaka na hakika sijawahi kuona Iramba mahindi yasifike/yasikomae mpaka kuvuna huku Maeneo mengine kama Dodoma, Shinyanga kukiwa na miaka ambapo hawavuni kabisa mazao kama mahindi.
Pia kuhusu Njaa nadhani sio sahihi sana, Miaka mingi sijapata taarifa kwa wilaya ya Iramba kuomba chakula cha msaada. Hii ni kutokana na ukweli kwamba mavuno ni ya kutosha. Nenda maeneo ya Misigiri, mampanta, kiomboi mpaka kisiriri, zunguka mpaka kinampanda miezi ya mavuno utakutana na Fuso zinatoka mikoa Jirani kuja kununua mazao kama Mahindi na Alizeti-Njaa ni kwa mtu binafsi na uzembe wake
Vipimo vya mvua na joto nimevitoa kwenye mtandao wa en.climates-data.org. So naweza kuestablish makadirio kwa kila kabila but inahitaji uchambuzi ambao kwa malengo ya bandiko hili sitaweza kwani ni kazi ngumu.By the way umepata wapi Vipimo vya mvua?? I mean source ya data zako?? Unaweza establish mavuno/family/year ili tuone upungufu wa chakula ni wa kiwango gani na kama unatosheleza??? Cuz kama huna taarifa hizi hutaaminika.
Mbona nimewaweka ndugu, tena wamepata wastani wa A hadi nafasi ya 15? Checki kwenye makabila ya watu wapatao 70,000 chini ya Wambunga (60,000) utaliona kwa chini kabisa.Umewasahau Wavidunda kule kilombero
Kuna Mungu wa kweli kule.Inakuwaje mbona Wachagga mnapenda kuwa A A sana na kila kitu kizuri wanakuwa wa kwanza kwanza?? Kuna nini uchaggani??
Duh karibu makabila yote yaliyopo kwenye comment hii sijawahi kuyasikia kabisaa.Wapimbwe ni nayo taarifa yao, tatizo nilitaka taarifa zote ziishie kwenye karatasi moja tu. Karatasi ya kwanza niliweka makabila 90 ikawa haionekani vizuri, hivyo nikaamua kupunguza baadhi ya makabila hasa madogo madogo. So kwa ajili yako nikitoka ofisini nitakupostia uone ilivyo na mazingira.
Of course ukiacha Wapimbwe, makabila mengine niliyoandaa taarifa yake lakini nikashindwa kuzi-feed zote ni:
Wawungu (wabungu), Wabende, Waalagwa, Wambugu, Wambugwe, Waikoma, Wadoe, Wasegeju, Wapemba, Watumbatu na Wahadimu.
Uzalishaji ninaoongelea siyo mtu kufanya kazi kwa bidii katika uzalishaji bali namna hali ya hewa na udongo wake pamoja na mazingira ya ufugaji na uvuvi, ndivyo vigezo vinavyoangaliwa. Unaweza ukawa na maliasili kibao umeilalia hiyo siyo issue bali wanapata vyakula cha kutosha ama hawapati. Achana na Wazanzibar wa kizazi cha sasa, kumbuka Wapemba, Watumbatu na Wahadimu, wamekuwepo huko visiwani tangu zamani kabla ya kuja kwa Waarabu. Kama wangekuwa hawazalishi chakula cha kutosha, isingewezekana kwa wao kuwa na msongamano mkubwa wa watu kuliko maeneo yote nchini Tanzania, ukitoa tu miteremko ya Mlima Kilimanjaro na baadhi ya maeneo madogomadogo machache sana nchini kama Kamachumu, Bukoba, Rungwe, Arumeru, Usambara na Uluguru.Wazanzibar toa hapo.
Watu wamekuta minazi na karafuu iliyopandwa na waarabu hata kupalilia hawapalilii kisha unawaita wazalishaji?
Au siku hizi kutengeneza urojo nao ni uzalishaji vyakula?
Samahani Mkuu..!!Unguja nimeweka makundi yake ya Watumbatu na Wahadimu kwa pamoja na Wapemba ndani ya Wazanzibar.
Hiyo yote imetokana na cha he wa nafasi.
Samahani tena...!!Ndugu nimeweka vyanzo vikundi vya taarifa hapo chini. Nilichofanya kama mchambuzi ni kuchambua hizo data katika perspective ya uzalishaji vyakula. Hebu angalia kwanza vyanzo vyangu vya taarifa ndiyo unihukumu.
But kwa kuwa, ninavifahamu vyote nilivyoviandika na na uelewa in and out, niko tayari kuvitetea vyote nilivyoandika hata kama ni pannel ya maprofesa, ikionekana kuna tatizo kwenye nilichoandika, pliz niko tayari kukifafanua.
Hii kazi mnayoiona siyo ya wiki moja wala mwaka mmoja, nimeifanya with patience and passion kwa miaka ipatayo kumi (10). Tangu niko UDSM, nilianza taratibu kukusanya details za baadhi ya masuala niliyokuwa tayari na idea nayo, mojawapo ni utofauti mkubwa wa makabila kielimu.
Ukiisoma taarifa hii with passion, for sure kina kitu kikubwa sana utakipata.
Acha kuingiza Imani za kishirikina ndugu, eneo hilo Lina mazingira bora ya uzalishaji wa vyakula vya karibia kila aina kuliko eneo lolote lile duniani hali iliyopelekea vizazi vilivyokulia eneo hilo kuneemeka na kurithishana genes bora kwa muda mrefu. Sifa ya mitelemko ya Kilimanjaro ni:Kuna Mungu wa kweli kule.
Hakuna ushirikina wa asili kama wa waswahili, kwahiyo hawakuilaani ardhi yao.
Hata matambiko yaliyokuwepo wanayaacha pia halafu YEHOVA anasimama upande wao.
Nani kakuuuliza hayo yooote?Acha kuingiza Imani za kishirikina ndugu, eneo hilo Lina mazingira bora ya uzalishaji wa vyakula vya karibia kila aina kuliko eneo lolote lile duniani hali iliyopelekea vizazi vilivyokulia eneo hilo kuneemeka na kurithishana genes bora kwa muda mrefu. Sifa ya mitelemko ya Kilimanjaro ni:
Wachaga, pamoja na Wahaya na Wanyakyusa, ni makabila makubwa nchini kwetu yenye mazingira bora kabisa ya uzalishaji wa vyakula vya aina mbalimbali katika Bara zima la Afrika na duniani kwa ujumla, yakiwa katika rank ya kwanza at par with the Kikuyu, Luo, Luhya, Gusii, Baganda, Banyankore, Rwanda, Rundi and the Igbo.
- Ndilo eneo lenye rutuba (volcanic) bora kuliko yote barani Afrika na probably duniani.
- Ndilo lenye msongamano mkubwa wa watu kuliko maeneo yote ya vijijini barani Afrika, ukitoa Nile Delta.
- Eneo linapata mvua za uhakika za aina mbili "bi-modal" ambayo ni vuli na masika.
- Ndilo lenye tofauti kubwa ya hali ya hewa (kuwepo kwa barafu hadi joto kali; na pia uwepo wa mvua nyingi hadi chache sana) katika umbali mdogo kuliko eneo lolote duniani (labda miteremko ya Himalaya pekee nchini Nepal). Hivyo wanaivisha kuanzia mazao ya baridi kali ikiwemo ngano hadi ya joto jingi ikiwemo mkonge.
- Hakuna malaria.
- Hakuna mbung'o wanaoeneza malale
- Lina msongamano mkubwa wa ng'ombe hapa nchini.
- Wachaga ni mchanganyiko wa Wabantu, Wahamites na Wanilotes. Mfano Wilaya ya Rombo iko dominated na koo zenye asili ya Wakamba ambao ni Hamitic lakini eneo la Marangu hadi Kibosho ni mostly Wabantu na la Machame hadi Siha ni Wanilotes.
Mzee naomba uamini kuwa, nimefanya kazi ya ziada kufikia hapo. Mimi siyo mwendawazimu kujitungia vitu nisivyo na uhakika navyo hadi kuviweka mitandaoni ambako kuna vichwa vingi humu JF vyenye kupambanua mambo.Samahani Mkuu..!!
Hizi takwimu zako zinaonekana zina ukweli ndani yake
Unaweza kuniambia umezipika kwa njia zipi...????
Mbona umefika huko ndugu? nilimaanisha kuwa, usihusishe sana mambo ya kiimani kwani vitu hivyo viko practically ndugu kuwa, uwepo wa vizazi na vizazi eneo hilo kwa muda mrefu ndiyo kumepelekea hayo. Sikumaanisha in reality kuwa wewe unaendekeza ushirikina.Nani kakuuuliza hayo yooote?
Unaweza kunionesha Imani ya kishirikina niliyoleta hapo?