Kabila lako bado mnaendelea kufanya matambiko ama mmeikacha asili yenu? Tambiko lenu hufanyikaje liwe la upatanishi, kufukuza mikosi, msamaha, n.k

Kabila lako bado mnaendelea kufanya matambiko ama mmeikacha asili yenu? Tambiko lenu hufanyikaje liwe la upatanishi, kufukuza mikosi, msamaha, n.k

sky soldier

JF-Expert Member
Joined
Mar 30, 2020
Posts
5,407
Reaction score
19,264
kabila hutambuliwa kwa Lugha, Mila, Miko, Majina na matambiko , hapa tutagusia matambiko .... Hakuna mtanzania asiye na tambiko, kila kabila alilotoka lina tambiko lake .

yapo makabila ambayo.97% ya kabila hilo ni wakatoliki lakini matambiko ya kiukoo yanaendelea na wazee wamila wanatambuliwa, mambo yao yanaenda fresh tu maana tambiko sio uchawi bali ni kuenzi mila na kupokea baraka zake.

Hata Baba wa taifa alifuta uchifu lakini alisema kabila lina kazi moja ya kuendelea kutambika lakini kwenye taifa ukabila haupaswi kuingizwa.

kwa bahati mbaya utandawazi wa sasa umefanya watu wadanganywe kirahisi kwamba mambo haya ni ushirikina na wengi hata mambo yao yamekwenda kombo kwa kupuuza asili zao bila kujua kwamba tambiko aliloshiriki baba na mababu zake limo bado ndani ya damu yake na ana jukumu la kutambika.

ni makabila yanayohesabika yenye utaratibu wa kuyafanya kila baada ya kipind flani kulingana na miiko ya mila .

sdstg.jpg
 
Matambiko maana yake ni nini na yana uhusiano gani na mambo kwenda au kutokwenda sawa? tuanzie hapo kwanza.
 
kuna hiyo ngoma inaitwa kifudu mimi naona wazimu mana wanacheza hovyo hadi naona aibu
 
Back
Top Bottom