Kabla hujaacha kazi au masomo, fahamu hili

Kabla hujaacha kazi au masomo, fahamu hili

Renald Gasper

Member
Joined
May 6, 2012
Posts
12
Reaction score
28
• Maana hasa ya 'Ujasiriamali' kama kujiajiri.

Watu wengi hukimbilia kujiajiri bila kuwa na ufahamu sahihi na halisi juu ya jambo hilo, kama hapo nyuma kwenye masomo yalio kwisha kupita nilisema, "pesa sio inayomfanya mtu kuwa tajiri, bali ni taarifa/elimu sahihi aliyonayo" vivyo hivyo kuwa mjasiriamali au kujiajiri kunautofauti na mtu alieajiriwa au mwajiriwa na sio tofauti ifahamiwayo na wengi.

Pindi unapoacha kazi, kipato chako huporomoka kufikia sifuri, hakuna malipo ya kila mwezi au wiki, hakuna akiba ya kustaafu lakini matumizi yako hayashuki bali hupanda zaidi. Mbaya zaidi hakuna afahamuue nilini tena utakapo weza kuanza kupokea malipo kwa kila baada ya muda fulani, yaweza chukua mwaka hata miaka. Na hii ndio tofauti kubwa ya mwajiriwa na mjasiriamali, mjasiriamali lazima awe na uweza wa kujishughulisha kwa akili zake zote na kwa umakini hata bila ya fedha.

Lakini pia tofauti nyingine kubwa ya mwajiriwa na mjasiriamali ni uweza wa kufahamu kutumiapesa kiusahihi uweza ambao wengi hawana hasa wafanyakazi. Hiyo nikwasababu wanauhakika wakupokea mshahara kila baada ya muda fulani, wakati mjasiriamali hana uhakika huwo hasa pindi anapoanza.

Hivo, kujiajiri sio jambo rahisi kama wengi wadhaniavyo, nijambo gumu sana na linahitaji umakini mkubwa sana ili uweze kuwa mjasiriamali halisi na mwenye mafanikio.

• Kwanini kujiajiri sio jambo rahisi?
Ukitazama duniani watu wanaofahamika sana kama matajiri wa kubwa tunaona niwengi ambao wawaliacha kazi na wakakimbia shule, matajiri kama; ~Bill Gates, mwanzilishi wa Microsoft, ~Steven Job, mwanzilishi wa Apple, ~Ted Turner, mwanzilishi wa CNN, ~Michael Dell, mwanzilishi wa Dell n.k. lakini pia wapo wachache wenye elimu ya juu sana lakini hawajulikani sana kama hao. Hivyo, swali linajiyokeza, kuacha shule au kazi ndio njia pekee yakuwa tajiri??? Hapana. Twende nyuma kidogo tufahamu uhalisia alisi.

∆ Miaka ya zamani sana kulikuwa hakuna wafanyakazi bali kulikuwa na wajasiriamali, watu ambao wàlifanya kazi kwenye mashamba ya wafalme, nao walikuwa hawalipwi mshahara bali walikuwa waki lipa wao pesa/vitu vya thamani kwa mfalme. Walijulikana kama wakulima wengi wao na wachache walikuwa wafanya biashara wadogo kama waoka mikate, watengeneza mishumaha nk. Na watoto walio kuwa kipindi hicho walifata njia za wazazi wao nakujifunza kuwa wajasiriamali.

Lakini mambo yalibadilika tulipo ingia kipindi cha viwanda. Ongezeko la uhitaji wa wafanyakazi ulikuwa kwa kasi, na ndipo serikali ya wazungu ikaamua kuingiza mfumo wa elimu ya Perssian, mfumo huu uhalisia wake ulikuwa ni kutengeneza au kufundisha watu watakao weza kufwata kanuni na maelekezo wapewayo, wanajeshi na waajiriwa/wafanyakazi. Hivyo ndivyo ujasiriamali ulipotea na watu wakaingia katika mfumo wa ajira hadi leo.
.
Kabla hatuja endelea, wapo watu wasemao kuwa ujasiriamali unazaliwa nao, wakimaanisha kuwa kama wewe hujazaliwa kuwa mjasiriamali hutaweza kuwa hivyo. Hii, sio kweli, hakuna mtu anaezaliwa kuwa mfanyakazi bali ni kwa kujifunza. Yeyote yule anaweza kuwa mfanyakazi bora au mjasiriamali mwenye mafanikio kama akipatiwa elimu sahihi. Huwezi kuendesha ndege kama ukipatiwa elimu ya kuendesha gari, lazima utapata ajali tu. Vivyo hivyo, huwezi kuwa mjasiriamali bora kama ukipata elimu ya kuwa mwajiriwa bora.
.
Hivyo, kuwa mjasiriamali nilazima ujifunze kama ujifunzavyo kuwa mwajiriwa, ugumu unaongezeka pale ambapo kuna sehemu nyingi wanapo fundisha jinsi ya kuwa mwajiriwa lakini hakuna sehemu nyingi au sahihi zifundishazo kuwa mjasiriamali, hapo ndipo panapo kuwa pagumu kwani wote tumezaliwa katika kipindi cha viwanda, kipindi cha waajiriwa.

• Hivyo, swali la kwanini inakuwa ngumu kujiajiri na kupata mafanikio litajibiwa kwa ufupi tu, hasa kwa kuonyesha tofauti halisi ya KUJIAJIRI na KUAJIRIWA.

~ Hakuna mtoto wa kizazi hiki anae ambiwa na mzazi wake nenda shule ukasome ili uje kujiajiri, la, bali nenda kasome ili upate kazi nzuri yenye malipo mazuri. Hili ni jambo jema na nzuri, lakini maana halisi ni hii; KUAJIRIWA tunaongelea Ulinzi (Kazi nzuri itakulinda maishani, maana yake, hautakuwa na hofu juu ya fedha na kipato chako kitakidhi matumizi yako, na unapofikia kustaafu utapewa pesa yako ya mstaafu).

Huku nikujilinda kwani hakuna ambae anapenda kuanguka kiuchumi. Lakini unapoongelea KUJIAJIRI (UJASIRIAMALI), unaongelea Uhuru (maisha yako hasa ya kifedha yapo mikononi mwako, wewe ndiyo unaeamua unayapelekaje, hakuna anae kusimamia ndio maana unaweza kuamua kwenda kazini au usiende, huwezi fanya hivo ukiwa umeajiriwa).

Hivyo, kadri unavyo hitaji Ulinzi bora zaidi katika maisha yako ya kifedha ndivyo utakavyo poteza uhuru zaidi. Hivyo, unapo hitaji uhuru lazima uwetayari kuachia ulinzi ili uwe huru, na hapa ndio msemo wa "Entrepreneurship is very risk" ukimaanisha, kujiajiri kunagharama sana kwani unakuwa huru lakini ulinzi wa kifedha ni mdogo kwako na hapa ndipo watuwengi hawaelewi na wanaishia kuporomoka kiuchumi kila wanapo jaribu kufanikiwa kupitia kujiajiri. Lakini sio kwamba ujasiriamali hauna ulizi hapana ugumu unakuwa mkubwa kwani ulinzi wake upo mikononi mwako mwenyewe, mbeleni tutaelewa zaidi.

Hivyo, ulinzi wa kuajiriwa na kujiajiri naweza linganisha kwa mfano huu, unapoajiriwa unalindwa na watu fulani kama vile kuwa mfanyakazi katika nyumba ya kifalme, wewe nikutekeleza majukumu yako tu navingine vyote hasa ulinzi ni juu ya mfalme hivyo wewe huna shaka juu ya mali zako, mfalme bora atakulindia mali zako salama zaidi kadri utakavyo tekeleza majukumu hivyo wewe waweza kulala na kufanya shughuli/majukumu yako bila ya kuwa namashaka juu ya mali zako. Lakini unapo jiajiri ulinzi wako unakuwa juu yako hakuna mtu anae kulinda au kukulindia mali zako bali ni jukumu lako kuwa makini na mali zako na kuziweka salama.

Hivyo, kuwa mjasiriamali kunaanza nakubadili fikra zako na kuwa na shahuku ya kuwa huru (kutokuwa chini ya mtu), lakini ifahamike kuwa unapo amaua kuwa mjasiriamali mwenye maendeleo njia na mfumo mzima wa kufikia lengo lako lakuwa huru sio rahisi kama wengi wajuavyo, ugumu mkubwa ni kubadilisha mtazamo wako, fikra na mwenendo wa maisha kwani mjasiriamali hafanyi vile mwajiriwa afanyavyo. Mjasiriamali kamwe hawi peke yake bali hutegemea watu katika mafanikio yake.

Ningependa tumalize kwa maana hii nzuri na yenye kuleta picha halisi ya mjasiriamali iliyo tolewa na Howard H. Stevenson, profesa katika chuo cha Harvard, aliesema, "Mjasiriamali ni mtu mwenye kutafuta nafasi za mafanikio bila ya kujali vitu alivyo navyo tayari", ('the persuit of opportunities without regard to resources currently controlled.'), ikimaanisha mtu asiye mjasiriamali sio mtu anaetafuta sana nafasi za mafanikio kwani hupenda sana kusema, "sina fedha za kuweza kuwekeza katika biashara hiyo", "sina mda nimetingwa sana namajukumu", "biashara hiyo niyakubahatisha sana", husema hivyo pindi apatapo nafasi ya mafanikio, wakati mjasiriamali halisi misemo yake mikuu huwa ni, "nawezaje", kufanyahivyo?, kuanzisha/kuwekeza katika biashara hiyo?, kupata hizo bidhaa? Hatakama hana pesa au mda kwa wakati huo, mjasiriamali haangalii ni pesa kiasi gani inahitajika bali anaangali ni mafanikio kiasi gani yanaweza kupatikana.

<BONUS>
•Kabla hujafanya uwamuzi wowote ule, kuacha kazi, kuacha masomo au shule, kuanzisha biashara au kufanya jambo lolote lile, ni lazima uwe na uelewa mpana na sahihi tena toka kwa mtu sahihi juu ya jambo utakalo kwenda kulifanya baada ya uwamuzi huo na ujue faida na hasara, raha na shida na jinsi gani utakavyo weza kukabiliana na changamoto zake pia, jinsi utakavyo weza kufikia lengo lako. Bila ya hivyo jua unakwenda kupotea, na ni vyema pia kumtanguliza MUNGU kwani atakusaidia kukuonyesha njia sahihi na uamuzi sahihi wa kufanya ✓
• Endelea kuungana nasi kuongeza uelewa wako zaidi wa kifedha.


∆ Somo litakalofwata ni, 'KWANINI UNAHITAJI UWELEWA WA KIFEDHA NA SIO KUJITUMA SANA'

Unaweza kusoma na kujifunza zaidi kupitia page yangu hii; facebook Elimu ya pesa or https://m.facebook.com/elimuyapesa

#Fedha
#Money
#IQ
 
Walioajiriwa wasia he kazi,wawekeze wakiwa katika ajira zao.

Ukijifanya kuchima meli moto utaumia,kumbuka hutopewa tuzo ya kuwa wewe ni mtu uliyeacha kazi huku ukiwa hujawekeza,utasota peke yako ulimwengu utajifanya kama haukuoni
 
Yeyote anaweza kuamua chochote bila kujali miongozo yenu.Sitakagi ushauri wa mtu mimi nikiamua langu Sipend kuja laumu mtu au mtu ajiskie vibaya kuwa hakunishaur vizur pindi mambo yanapobuma pia sihitaji mtu aje achukue credit kuwa ni ushaur wake umenifakisha pind risk yangu ikiniweka juu ya mstari.
 
Back
Top Bottom