Kabla hujanunua Azam TV pitia hapa; Usije kujuta

Huo ni mkakati maalum wa kuendeleza tamaduni za kihindi kama mlikuwa hamjui,haiwezkani decoda imejaa michanel ya kihindi tu,na hii michanel inaoneka tu hata usipolipia,lkn tv zetu la local usipolipia tu znakata!sinunui ng'o azam nimeshaghairi,nashkuru kwa taarifa mkuu
 
Fanya maamuzi sahihi mkuu! utafiti utakusaidia kupata decoder bora sio kelele za Azam
 
Sinema Zetu inaboa mpaka basi, movie moja wanairudia zaidi ya mara 4 kwa wiki.
Hahaaa...... Azam katika ubora wao.
 
Mkuu hzo chanel za kihind hata wakiacha bure..unazielewa kwanza hahaha
 
Azam hamna kitu kabisa wakuu, wamenikera sana kukata channel za ndani pale kifurushi kinapoisha! Wanabakiza tbc 1 tu! Nimerudi Startimes
 
mimi tangu 2012 nipo kwa makaburu dstv...sijutii maamuzi na sina mpango wa kuhama! dstv watamu balaaaa sema tu inshu yao ni malipo...kifurushi cha chini kbsa tsh. 23,500/-!!!

ila picha zao ziko bora sanaaaa ukilinganisha na vingamuzi vingine....mzazi hakuna chenga wala nini!!! KAMA UNAPENDA SPORTS DSTv ndo home
 
nakuja
 
Mwaka Wa Nne Huu Nipo DSTV Na Sijawahi Kujuta, Hivi Unaanzaje Kununua Azam Tv au Startimes?
 
natafta king,amuzi cha startimes nina 20000 nipm plsss
 
Dstv ...yes ni nzuri kakini expensive
Azam....inakwenda vizuri tuwape muda
Azam.... wanazo OB van za kisasa kabisa ktk kanda zote na the best srudios south of sahara.
Time is the best nedicine
 
azam nmemuachia mwanangu anaangalia makatuni basi.yaaan nikimuona mtu ananunua kingamuzi cha azam namuonea huruma sana.mar ya kwanza tulifaidi burudani.ila sasa cjui nani kawaloga hawa jamaa.ukihesabu channel za kiarabu na kihindi ni robo tatu ya channel zote!!
 
Hata mpangilio wa channels wameshindwa kutafuta za michezo Moja ipo kusini nyingine magharibi, wanaboa! Hawana channel ya maana, channels 90% ni free to air, ila bado wanatulipisha! Wezi wakubwa!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…