Kabla hujanunua godoro pitia hapa ujue lipi litakufaa

Attachments

  • IMG_0787.mov
    10.5 MB
  • IMG_0745.png
    IMG_0745.png
    7.2 MB · Views: 9
  • IMG_0380.jpeg
    IMG_0380.jpeg
    2.2 MB · Views: 11
Unahitaji spring karibu lala kwa kunesa nesa usingizi muruaaa maisha mafupi jipe raha mwenyewe
20231201_102603-BlendCollage.jpg
 
Godoro zipo katika daraja tatu kama vitu vingi vilivyo hapa duniani sio kila godoro linafaa kulaliwa na mtu yeyote.

Mfano wale wanene ana godoro lake huyo ukichukua lenye ujazo mdogo lazima tu litaleta tatizo kwako

Ujazo ni nini?
Godoro zote tunazipima kwa mgandamizo uliotumika katika utengenezaji wake yaani density hapa shule kidogo wale ambao physics hamkuikimbia.

Kiufupi kama soda zilivyo na ujazo yaani yenye 350ml au vile vibambucha vilikuwa 250ml
Hata godoro zipo hivyo hivyo pia.

Maana wengi hukosea kuamini kwamba godoro ngumu sana ndio ubora hapana sio hivyo

Godoro lenye ujazo mdogo
Hizi ni godoro zenye ujazo chini ya 18

Godoro lenye ujazo mdogo ni zile ujazo wake upo chini ya 18 hapa Shirika letu la viwango Tbs limeyapa makampuni ya magodoro watengeneze zaidi ya hapo.

Japo vipo viwanda baadhi vinakaidi hilo. Ila pia wana sababu maana kudumu kwa godoro hutegemea mtumiaji

Mfano
Kwenye kambi zote za Jeshi wale muda wao wa kulala ni mfupi hawa wana godoro zao hupewa light density yaani ujazo kiasi.

Au wale watalii wa muda mfupi, sasa kosa ununue ndugu yangu kutwa kwenye movie

Godoro ujazo wa kati(Medium density)
Hizi huanzia ujazo wa 18 mpaka 24 zinafaa sana kwa matumizi ya ndani ila nazo zina utofauti kwenye kudumu
Lenye 19 sio sawa na lenye 24 hapa nadhani tunajua sababu kwanini

Yes ni ujazo wake mkubwa ina maana hata materials zimetumika nyingi (mgandamizo mkubwa )
Mwemye uzito wa kilo 55 sio sawa na mwenye uzito wa 80 hawawezi kutumia godoro moja

Huyu mwenye uzito wa 80 anatakiwa atumie godoro lenye ujazo wa 23 au 24 sio chini ya hapo
Na unene aanzie walau inchi 10 hapo itakuwa burudani kwake

Magodoro ujazo mkubwa
Hapa ni zile godoro ujazo zaidi ya 24 mpaka 32

Hizi zinawawafaa sana wenye uzito mkubwa yaani zaidi ya kilo 80

Au mwenye kusumbuliwa na maumivu iwe mgongo au kiuno huyu atumie kuanzia ujazo wa 28
Ujazo wa 28 ndio godoro nchi ngapi
 
Ujazo wa 28 ndio godoro nchi ngapi
Tunaposema ujazo sio unene boss yaani inchi bali ni mgandamizo uliotumika katika utengenezaji wa hilo godoro ndio utalifanya liwe gumu au laini

Au kiufupi ujazo hapa tunamaanisha ulaini na ugumu wa godoro
 
kipindi hiki cha likizo watoto wetu wabadidilishie godoro au kuongeza godoro watoto wameshakua tayari
 
unahitaji godoro lenye ubora hilo ulilonalo mgongo unakuuma karibu upate ushauri godoro gani linakufaa
 
Godoro zipo katika daraja tatu kama vitu vingi vilivyo hapa duniani sio kila godoro linafaa kulaliwa na mtu yeyote.

Mfano wale wanene ana godoro lake huyo ukichukua lenye ujazo mdogo lazima tu litaleta tatizo kwako

Ujazo ni nini?
Godoro zote tunazipima kwa mgandamizo uliotumika katika utengenezaji wake yaani density hapa shule kidogo wale ambao physics hamkuikimbia.

Kiufupi kama soda zilivyo na ujazo yaani yenye 350ml au vile vibambucha vilikuwa 250ml
Hata godoro zipo hivyo hivyo pia.

Maana wengi hukosea kuamini kwamba godoro ngumu sana ndio ubora hapana sio hivyo

Godoro lenye ujazo mdogo
Hizi ni godoro zenye ujazo chini ya 18

Godoro lenye ujazo mdogo ni zile ujazo wake upo chini ya 18 hapa Shirika letu la viwango Tbs limeyapa makampuni ya magodoro watengeneze zaidi ya hapo.

Japo vipo viwanda baadhi vinakaidi hilo. Ila pia wana sababu maana kudumu kwa godoro hutegemea mtumiaji

Mfano
Kwenye kambi zote za Jeshi wale muda wao wa kulala ni mfupi hawa wana godoro zao hupewa light density yaani ujazo kiasi.

Au wale watalii wa muda mfupi, sasa kosa ununue ndugu yangu kutwa kwenye movie

Godoro ujazo wa kati(Medium density)
Hizi huanzia ujazo wa 18 mpaka 24 zinafaa sana kwa matumizi ya ndani ila nazo zina utofauti kwenye kudumu
Lenye 19 sio sawa na lenye 24 hapa nadhani tunajua sababu kwanini

Yes ni ujazo wake mkubwa ina maana hata materials zimetumika nyingi (mgandamizo mkubwa )
Mwemye uzito wa kilo 55 sio sawa na mwenye uzito wa 80 hawawezi kutumia godoro moja

Huyu mwenye uzito wa 80 anatakiwa atumie godoro lenye ujazo wa 23 au 24 sio chini ya hapo
Na unene aanzie walau inchi 10 hapo itakuwa burudani kwake

Magodoro ujazo mkubwa
Hapa ni zile godoro ujazo zaidi ya 24 mpaka 32

Hizi zinawawafaa sana wenye uzito mkubwa yaani zaidi ya kilo 80

Au mwenye kusumbuliwa na maumivu iwe mgongo au kiuno huyu atumie kuanzia ujazo wa 28
Asante ila mimi nina hasira na watengenezaji wote wa magodoro,kwanini ama kushindwa japo kutoa elimu kwa wateja kuhusu bidhaa zao ama kwa makusudi kuwaibia wateja wao kwa bidhaa chini ya kiwango kwa maana ya kujipatia faida nono.Mimi binafsi nachukulia swaĺa la ubora wa magodora kama alarm ya uwepo wa bidhaa fake.Vinginevyo kwa kuwa umejitokeza kama mtoa huduma,ama mtengenezaji wa bidhaa hii,uje na elimu mahususi ili wote ambao wamekuwa wahanga wa bidhaa hii au ubora au ukodefu wa elimu juu ya bidhaa hii warejeshe imani iliyopotea.
 
Tupo kukupa elimu boss pia nikusahihishe kidogo hakuna Kiwanda kinachozalisha godoro feki ukisema hivyo kazi ya Tbs ni nini? Godoro Zipo katika viwango mbalimbali na kuruhusu uzito tofauti tofauti unapaswa kulijua kwanza godoro gani ulinunue sio lolote likionekana mbele yako
 
Back
Top Bottom