Kabla hujanunua godoro pitia hapa ujue lipi litakufaa

Kabla hujanunua godoro pitia hapa ujue lipi litakufaa

Vita supreme
 

Attachments

  • IMG-20240601-WA0000.jpg
    IMG-20240601-WA0000.jpg
    63.4 KB · Views: 27
Mleta uzi, hii density ina affect bei? Kama haiafekti bei nimeshapata jibu langu. Ila kama ina affect bei, naomba ufanye kuedit uzi wako pale juu kuelekeza bei fulani kwa density fulani.
 
Mleta uzi, hii density ina affect bei? Kama haiafekti bei nimeshapata jibu langu. Ila kama ina affect bei, naomba ufanye kuedit uzi wako pale juu kuelekeza bei fulani kwa density fulani.
Density ndipo ubora wa godoro ulipo mkuu kama umeweza kuelewa asante kwako
Inamaana lenye ujazo mdogo hata bei itakuwa ndogo
 
Na kuligeuza kila baada ya miezi mitatu
Kuligeuza kwa godoro bora haina haja sababu kama ni mbonyeo ni wa kawaida pande zote tunashauri kugeuza sababu uzito wa mtu hubadilika ndani ya huo muda
Uzito wa wife na mume ni tofauti itasaidia kidogo kwa wenye uzito mkubwa lakini chini ya 80 haina haja mkuu karibuni sana kwa ushauri zaidi

0657050325 calls na WhatsApp
 
Godoro zipo katika daraja tatu kama vitu vingi vilivyo hapa duniani sio kila godoro linafaa kulaliwa na mtu yeyote.

Mfano wale wanene ana godoro lake huyo ukichukua lenye ujazo mdogo lazima tu litaleta tatizo kwako

Ujazo ni nini?
Godoro zote tunazipima kwa mgandamizo uliotumika katika utengenezaji wake yaani density hapa shule kidogo wale ambao physics hamkuikimbia.

Kiufupi kama soda zilivyo na ujazo yaani yenye 350ml au vile vibambucha vilikuwa 250ml
Hata godoro zipo hivyo hivyo pia.

Maana wengi hukosea kuamini kwamba godoro ngumu sana ndio ubora hapana sio hivyo

Godoro lenye ujazo mdogo
Hizi ni godoro zenye ujazo chini ya 18

Godoro lenye ujazo mdogo ni zile ujazo wake upo chini ya 18 hapa Shirika letu la viwango Tbs limeyapa makampuni ya magodoro watengeneze zaidi ya hapo.

Japo vipo viwanda baadhi vinakaidi hilo. Ila pia wana sababu maana kudumu kwa godoro hutegemea mtumiaji

Mfano
Kwenye kambi zote za Jeshi wale muda wao wa kulala ni mfupi hawa wana godoro zao hupewa light density yaani ujazo kiasi.

Au wale watalii wa muda mfupi, sasa kosa ununue ndugu yangu kutwa kwenye movie

Godoro ujazo wa kati(Medium density)
Hizi huanzia ujazo wa 18 mpaka 24 zinafaa sana kwa matumizi ya ndani ila nazo zina utofauti kwenye kudumu
Lenye 19 sio sawa na lenye 24 hapa nadhani tunajua sababu kwanini

Yes ni ujazo wake mkubwa ina maana hata materials zimetumika nyingi (mgandamizo mkubwa )
Mwemye uzito wa kilo 55 sio sawa na mwenye uzito wa 80 hawawezi kutumia godoro moja

Huyu mwenye uzito wa 80 anatakiwa atumie godoro lenye ujazo wa 23 au 24 sio chini ya hapo
Na unene aanzie walau inchi 10 hapo itakuwa burudani kwake

Magodoro ujazo mkubwa
Hapa ni zile godoro ujazo zaidi ya 24 mpaka 32

Hizi zinawawafaa sana wenye uzito mkubwa yaani zaidi ya kilo 80

Au mwenye kusumbuliwa na maumivu iwe mgongo au kiuno huyu atumie kuanzia ujazo wa 28
Kuna taarifa imekosekana hapa. Mfano hiyo ujazo wa 28 n.k. Unapatikana katika inch zipi? Pili SI unit ya huo ujazo ni ipi? Tatu kuna magodoro fulani hivi ya kichina, very sophisticated. Bila shaka umeshaona promo zake mitandaoni. Yale ujazo wake ukoje na ubora je?
 
Duh nimecheka mpaka kupaliwa na dawn yote hii🤣🤣
Ndiomana akasema wale ambao hawjakimbia physics watamuelewa na kwa swali lako hili unadhihirisha hata physics ya form one huijui maana maneno DENSITY, MASS, MATTER yasingekuwa mageni kwako. Hapa limetumika moja tu density je angeelezea full details za utengenezaji wake hata kunusa huu Uzi usingeunusa🤣🤣🙌
Kabisaaa mkuu ni kuelezea hata la saba tu aelewe maana wengi wanajua godoro ni godoro tu lina vitu vingi vya kuzingatia
 
Kuna taarifa imekosekana hapa. Mfano hiyo ujazo wa 28 n.k. Unapatikana katika inch zipi? Pili SI unit ya huo ujazo ni ipi? Tatu kuna magodoro fulani hivi ya kichina, very sophisticated. Bila shaka umeshaona promo zake mitandaoni. Yale ujazo wake ukoje na ubora je?
Mkuu hapa tunazungumzia Tanzania tulipo na hizi kampuni ni zetu hapa hapa
Pia kuli attack kampuni moja kwa moja sio vizuri kibiashara ni kosa ushauri zaidi njoo namba zetu hizo boss

Pia hizo za kichina nyingi ni fibre zingine huwa pia za upepo
 
Back
Top Bottom