Kabla hujanunua godoro pitia hapa ujue lipi litakufaa

Kabla hujanunua godoro pitia hapa ujue lipi litakufaa

Mbona comfy sioni kwenye maoni yakoo au lenyewe halina kasoro yoyote?
Naomba utuchambulie kwa kina kuhusu magodoro ya comfy hata kwa machahe tu.🙏🏽
 
Godoro ulizotaja zote ni ujazo wa 23 na 24 pia kubonyea kwa godoro kuna sababu nyingi miongoni ni hizi

Kitanda chako chaga zina uwazi mkubwa
Godoro kukunjwa muda mrefu
Kulala godoro na karatasi lake bila kulivua


Pia kwa huo uzito bado huo ujazo sio sahihi kwako walau uende inchi 10 au 12

Godoro linalokufaa ujazo wa 28 na kuendelea karibu kwa ushauri zaidi
Godoro gani utumie
Unapatikana wapi nijaribu Hilo la ujazo hio maana kuhusu Chaga na karatasi sio Sahihi
 
Godoro zipo katika daraja tatu kama vitu vingi vilivyo hapa duniani sio kila godoro linafaa kulaliwa na mtu yeyote.

Mfano wale wanene ana godoro lake huyo ukichukua lenye ujazo mdogo lazima tu litaleta tatizo kwako

Ujazo ni nini?
Godoro zote tunazipima kwa mgandamizo uliotumika katika utengenezaji wake yaani density hapa shule kidogo wale ambao physics hamkuikimbia.

Kiufupi kama soda zilivyo na ujazo yaani yenye 350ml au vile vibambucha vilikuwa 250ml
Hata godoro zipo hivyo hivyo pia.

Maana wengi hukosea kuamini kwamba godoro ngumu sana ndio ubora hapana sio hivyo

Godoro lenye ujazo mdogo
Hizi ni godoro zenye ujazo chini ya 18

Godoro lenye ujazo mdogo ni zile ujazo wake upo chini ya 18 hapa Shirika letu la viwango Tbs limeyapa makampuni ya magodoro watengeneze zaidi ya hapo.

Japo vipo viwanda baadhi vinakaidi hilo. Ila pia wana sababu maana kudumu kwa godoro hutegemea mtumiaji

Mfano
Kwenye kambi zote za Jeshi wale muda wao wa kulala ni mfupi hawa wana godoro zao hupewa light density yaani ujazo kiasi.

Au wale watalii wa muda mfupi, sasa kosa ununue ndugu yangu kutwa kwenye movie

Godoro ujazo wa kati(Medium density)
Hizi huanzia ujazo wa 18 mpaka 24 zinafaa sana kwa matumizi ya ndani ila nazo zina utofauti kwenye kudumu
Lenye 19 sio sawa na lenye 24 hapa nadhani tunajua sababu kwanini

Yes ni ujazo wake mkubwa ina maana hata materials zimetumika nyingi (mgandamizo mkubwa )
Mwemye uzito wa kilo 55 sio sawa na mwenye uzito wa 80 hawawezi kutumia godoro moja

Huyu mwenye uzito wa 80 anatakiwa atumie godoro lenye ujazo wa 23 au 24 sio chini ya hapo
Na unene aanzie walau inchi 10 hapo itakuwa burudani kwake

Magodoro ujazo mkubwa
Hapa ni zile godoro ujazo zaidi ya 24 mpaka 32

Hizi zinawawafaa sana wenye uzito mkubwa yaani zaidi ya kilo 80

Au mwenye kusumbuliwa na maumivu iwe mgongo au kiuno huyu atumie kuanzia ujazo wa 28

Una swali lolote weka chini tutakujibu

Namba WhatsApp 0657050325
Tatizo mnaouza vitu humu wengi mnauza vitu vya wizi...Kuna jamaa alikua anauza tairi nikataka nimuungishe anadai ofis ipo Vingunguti nikamuambia niletew tairi 4 Sinza saa 4 asubuhi akasema poa. Mpaka inafika saa 7 anasema yupo njiani. Baadae nikamuambia nakuja huko huko. Ile nafika Baracuda nishuke Vingunguti kazima simu mazima.
 
Zipo 5x6 na 6x6 boss bei hizi [emoji116]
IMG_20240201_193108_802.jpg
 
Tatizo mnaouza vitu humu wengi mnauza vitu vya wizi...Kuna jamaa alikua anauza tairi nikataka nimuungishe anadai ofis ipo Vingunguti nikamuambia niletew tairi 4 Sinza saa 4 asubuhi akasema poa. Mpaka inafika saa 7 anasema yupo njiani. Baadae nikamuambia nakuja huko huko. Ile nafika Baracuda nishukr Vingunguti Lazima simu mazima
Ndugu katika kutaja watu nakushauri usipende kuweka kwa jumla

Binafsi biashara yangu ipo huru na imesajiriwa na sio kwamba inategemea humu tu wapo wanaofika physically hata jf hawaijui
Kiufupi
Binadamu wana tabia tofauti ila nikukaribishe ofisi zetu
 
Nitajuaje ujazo wa godoro nikifika pale dukani
Kujua kama sio mzoefu ni ngumu ila baadhi ya viwanda wamesaidia kuweka label zenye kuonyesha ujazo wa godoro
Mfano dodoma qfl density 24
Comfy density 23
Vita raha density 23
Vita supreme density 28
20240213_135935801.jpg
20230318_181846-BlendCollage.jpg
20221224_170129493.jpg
 
Nimeelewa halafu sijaelewa

Huo ujazo ni nini (kipimo) na nautambuaje au umeandikwa kwenye magodoro?
Nikuweke kwenye kundi la walioelewa pia nikuongezee uelewa kidogo kwa kukupa mfano wa soda zilivyo katika ujazo tofauti
Kwamba ipo soda ila ml 350 na nyingine kubwa ml 500 mpaka vile vidogo vilikuwa ml 250 wengi tuliziita bambucha

Sasa hata godoro nazo zina ujazo ukinunua lenye ujazo mdogo hata kudumu kwake hivyo hivyo ni muda mfupi
Ukilinganisha na ujazo mkubwa
Nadhani sasa umeelewa in fully
 
Godoro ni tanform Arusha pekee au Banco mwaka wa 15 huu lishabeba coaster za kutosha lakini kama jipya
Hapana sio pekee bali kuna vingi vya kuzingatia kwako boss huenda hata uzito wako sio mkubwa
Pia rate yako ya kulala sio kubwa
Ila zipo nyingi nzuri kama TAN foam na Banco
Kama
Dodoma
Comfy
Vita raha
Deluxe Arusha
 
Mbona comfy sioni kwenye maoni yakoo au lenyewe halina kasoro yoyote?
Naomba utuchambulie kwa kina kuhusu magodoro ya comfy hata kwa machahe tu.[emoji1431]
Comfy ni godoro nzuri boss na pia ni kiwanda cha zamani lenyewe ujazo wake ni 23 linawafaa sana chini ya kg 70 na kama zaidi ya hapo basi uchukue lenye unene mkubwa
 
Back
Top Bottom