HAKI KWA WOTE
JF-Expert Member
- Nov 30, 2022
- 2,783
- 2,396
MBINGUNI AU MOTONIIwapo kuna mbinguni na kuzimu wanakoenda Wafrika wakifa je kabla ya wamisionari walienda wapi?
upo utumwani,akili yako imefungamana na utumwa wa vitabu vilivyotungwa kwa lengo la kukutawala akili yako. Zinduka mwafrika mwenzangu.MBINGUNI AU MOTONI
Wale waliotenda dhambi bila kuijua sheria wataangamia ingawaje hawaijui sheria. Na wale wanaotenda dhambi wakiwa wanaijua sheria watahukumiwa kisheria. Maana sio wanaosikia sheria ndio walio waadilifu mbele ya Mungu, ila wenye kuitii sheria ndio watakaokubaliwa kuwa waadilifu. Mathalani: Watu wa mataifa mengine hawana sheria; lakini kila wanapotimiza matakwa ya sheria wakiongozwa na dhamiri zao, wao wenyewe wanakuwa kipimo cha sheria ingawa hawaijui sheria. Mwenendo wao unaonesha kwamba matakwa ya sheria yameandikwa mioyoni mwao. Dhamiri zao zinashuhudia pia jambo hilo, maana fikira zao mara nyingine huwashtaki, na mara nyingine huwatetea. Hivyo, kufuatana na hii Habari Njema ninayohubiri, ndivyo itakavyokuwa wakati Mungu atakapohukumu mambo ya siri ya binadamu kwa njia ya (Warumi 2:12-16)
Kwa nn mungu alichelewa kuwajulisha mapema ??ili wamtumikieeMBINGUNI AU MOTONI
Wale waliotenda dhambi bila kuijua sheria wataangamia ingawaje hawaijui sheria. Na wale wanaotenda dhambi wakiwa wanaijua sheria watahukumiwa kisheria. Maana sio wanaosikia sheria ndio walio waadilifu mbele ya Mungu, ila wenye kuitii sheria ndio watakaokubaliwa kuwa waadilifu. Mathalani: Watu wa mataifa mengine hawana sheria; lakini kila wanapotimiza matakwa ya sheria wakiongozwa na dhamiri zao, wao wenyewe wanakuwa kipimo cha sheria ingawa hawaijui sheria. Mwenendo wao unaonesha kwamba matakwa ya sheria yameandikwa mioyoni mwao. Dhamiri zao zinashuhudia pia jambo hilo, maana fikira zao mara nyingine huwashtaki, na mara nyingine huwatetea. Hivyo, kufuatana na hii Habari Njema ninayohubiri, ndivyo itakavyokuwa wakati Mungu atakapohukumu mambo ya siri ya binadamu kwa njia ya Yesu Kristo. (Warumi 2:12-16)
Iwapo kuna mbinguni na kuzimu wanakoenda Wafrika wakifa je kabla ya wamisionari walienda wapi?
Huu ndiyo ujinga wenyewe kwahiyo kuzimu na ahera vimekuwepo au vimeanza baada ya wamisionari kuja Afrika au Mungu kavianzisha baada ya wamisionari kuja Afrika?Warumi 2 (Biblia Takatifu)
¯¯¯¯¯¯¯¯¯¯
¹² Kwa kuwa wote waliokosa pasipo sheria watapotea pasipo sheria, na wote waliokosa, wenye sheria, watahukumiwa kwa sheria.
¹³ Kwa sababu sio wale waisikiao sheria walio wenye haki mbele za Mungu, bali ni wale waitendao sheria watakaohesabiwa haki.
¹⁴ Kwa maana watu wa Mataifa wasio na sheria wafanyapo kwa tabia zao yaliyo ndani ya torati, hao wasio na sheria wamekuwa sheria kwa nafsi zao wenyewe.
¹⁵ Hao waionyesha kazi ya torati iliyoandikwa mioyoni mwao, dhamiri yao ikiwashuhudia, na mawazo yao, yenyewe kwa yenyewe, yakiwashitaki au kuwatetea;
¹⁶ katika siku ile Mungu atakapozihukumu siri za wanadamu, sawasawa na injili yangu, kwa Kristo Yesu.
naomba utafakari hapa kisha usichoke kushea ulichokipata hapa
Baada ya gharika ya Noah na baada ya MUNGU kutenganisha mataifa kulingana na lugha zao, MUNGU alichagua Taifa moja ili ajifunue / ajidhihirishe ulimwenguni,
ili kujitofautisha na mungu muovu aliyeachiwa atawale ulimwengu huu kwa muda,
mpaka wakati alioweka MUNGU wa kuchukua mamlaka yake na kukomboa watoto wake kutoka utawala wa yule muovu, na kuondoa uovu wote.
Hilo taifa ndilo lilopaswa kuwa mwanga ulimwenguni:
MUNGU wa kweli, Muumba wa mbingu na nchi ni huyu tunayemuabudu.
Hao mnaowaabudu ni wa uongo, ni god "wanna be"s, ni waasi.
Sheria za MUNGU wa kweli ni hizi,
miujiza yake,
hekalu lake ambalo utukufu wale unashukia humo,
mafundisho / hekima yake,
manabii wake,
MWANA wake, aliyeuawa na baada ya siku tatu alifufuliwa, naye sasa ndiye Mwanga wa ulimwengu.
Watu wa mataifa mengine waliomchagua MUNGU wa kweli walijiunga na taifa lake, na kutambulika kuwa moja kati ya makabila 12.
Mfano walivyotoka Misri kuna Wamisri waliungana na waisraeli, wakahesabiwa kati ya yale makabila 12 bila kubagua.
Waisraeli walikuwepo hadi Afrika (Ethiopia).
Mfano, tunasoma myahudi muEthiopia (yaani muethiopia aliyetambulika kuwa wa kabila la Yuda) alisafiri kwenda Yerusalemu kwenye hekalu kwa ajili ya siku kuu, kama ilivyo sheria.
(Kwahiyo ukifikiria Muisraeli usifikirie ngozi nyeupe, usimfikirie Netanyahu na Mossad. Muisraeli / Myahudi ni yule aliyemkubali MUNGU wa Israeli na mwana wake YESU.)
Biblia ya zamani kabisa iliyo nzima tuliyonayo imeandikwa kilugha cha Ethiopia, ya karne ya 4 huko.
Tangu ukristo umeanza karne ya kwanza ilikuwepo Afrika. Ulisambaa taratibu kwa sababu ya teknolojia. Meli zilirahisisha kusambazs ukristo. Na sasa Internet imemaliza kazi, YESU amekaribia kurudi.
So sio Africa tu, jamii / mataifa yote baada ya kusambaratika kutoka mnara wa babeli waliishia kuabudu roho waovu.
MUNGU wa Israeli katuma watumishi wake kila mahali, watakwambia yote aliyosema MUNGU kwa lugha yako wewe,
social media utawakuta,
barabarani utawakuta,
kwenye radio/ tv,
Vijarida,
Watakugongea hadi nyumbani kwako,
hata ukienda kutembelea zile site zile utakuta tangazo "DO YOU KNOW JESUS?" unafanya ku cancel na kusema yes I'm 18 and above, lakini ujumbe umefika.
Hawa miungu wengine sasa, kwanza ni wengi sijui uanzie wapi, hawakutafuti ni wewe ujipeleke uchague, ukajifunze lugha yao, wengine hata hawataki watu wa mataifa / makabila mengine,
na ukijileleke si upajue sasa, ni wanapatikana kwa connection, usafiri masafa upande milima na mabonde na wanaowapata huko hatujui kinawakuta nini maana hawasemagi,
habari za miungu hii zimefichwa na usiri na woga. Kazi za hii miungu ya giza hatuzioni, ni kazi za mafichoni gizani, probably ni za kutia aibu na kutisha pia ndomana hazisemwi! ! Probably moja ya masharti ya miungu hii ni kutosema kazi zake.
MUNGU wa ISRAELI akifanya kitu lazima muhusika akapayuke hadharani hadi kila mtu amjue MUNGU wa KWELI. Kazi zake ni za nuruni.
Ni MUNGU wa wote, wote wanaruhusiwa kumfuata bila kuzingatia rangi na kabila lako, anaunganisha watoto wake wote duniani kupitia IMANI juu ya mwana wake YESU.
Muisraeli / Myahudi wa kweli ni yule aliyemkubali YESU.Kwahiyo
Kwahiyo leo israel wameelekezwa na Mungu wapigane vita kwenye nchi takatifu eti??
Na hayo yote ya kwenye biblia na quruan Mungu aliona ayalete Afrika na watawaliwe na waliomleta yesu,kweli una ubongo wewe??
MbinguniSwali gumu mno wakikujibu wafia dini za wazungu na waarabu nakuomba unitag