Kabla ya kukubali kuolewa soma hapa dada yangu ujiridhishe

Pdidy

JF-Expert Member
Joined
Nov 22, 2007
Posts
57,951
Reaction score
32,619
DADA YANGU KABLA HUJAANZISHA MAHUSIANO NA MWANAUME HUU NDIO MGAWANYO WA WANAUME KULINGANA UMRI WAO

1. WANAUME wenye miaka 20-27 wengi hawako serious na ndoa au mahusiano yenye kesho labda wale wa vijijini. Kijijini vijana wengi huoa kwasababu kama waongeze nguvu kazi ya familia, mahari mara nyingi zinatoka kwa wazazi sio zao (hawajazitesekea) lakini wanaume waliko mjini kwa 20-27 wengi ni wanafunzi na wanakimbizana na ndoto zao huwa si rahisi kuingia kwenye ndoa. Kwahiyo, ukianzisha naye mahusiano ni vigumu sana kukuoa kwasababu ana kiu na hofu ya MAISHA sana. Wanaume walioko kijijini mara nyingi hawayatazami maisha nje ya kulima na kuvuna zaidi wao wanatafuta kwa ajili ya muda uliopo si kwa ajili ya hatma zao njema. Kwahiyo dada yangu mwanaume akiwa chini ya miaka 28 akiwa mjini ukianzisha mahusiano ni vigumu kuwaza ndoa kwake.

2. WANAUME WA UMRI WA MIAKA 28-31 hawa huwa wameshapevuka na wameanza focus ya maisha anaweza akawa hana mafanikio ila angalau au ameshaona wapi anahitajika kufanya nini na utoto huwa umepungua zaidi labda awe hana dira yaani awe bado mgalatia au ameamua kuishi maisha ya KIGALATIA. Wengi wa 28-31 huwa si wanafunzi tena wamemaliza masomo wanajitafuta mtaani, wamepata pakushika, wanajimudu kwenye mambo yao muhimu na wanawaza kuanzisha mahusiano ya kudumu ili wasogee mbele. Wengi huwa hawajajipata sana ila huhitaji mahusiano yenye focus. Hawa watu huonekana wakorofi sana kwasababu wana uchungu na mafanikio hasa mwanamke akija kwenye maisha yake anataka bata.

Hapa ndipo wanawake wengi huachwa wakionekana wanashindwa kufocus kwenye malengo, hapa ndipo single father wengi hupatikana kwasababu vijana wengi huanza kuishi na wanawake kabisa kama wake au hujiachia kwenye mahusiano yao wakuamini hao ndio watakuwa wake zao. Maisha ya wanaume hao yakiyumba wanawake huwakimbia hao vijana wakiwa tayari wameza nao au wanawake wakitaka maisha nje ya uhalisia huachwa nao vijana kwasababu wao wanawaza kusimama kiuchumi huku wanawake hao wakihitaji maisha nje ya uhalisia.

3. WANAUME wa umri wa 32-38 hawa ni wanaume waliopitia mengi kupoteza, kuumizwa na kuumiza pia. Hawa huwa na mambo mawili kumpata mwanamke wa rika lake au linaondena na lake hawapendi vidada kwasababu wengi huwa wameumizwa sana na wadada wadangaji. Hawa wao nitafuta mwanamke aliyemaliza ujana kama yeye na anayeyajua maisha na alevuka hatua za UGALATIA.

4. WANAUME wenye miaka 40 na kuendelea hawa wao hutafuta mwanamke anayeweza kumheshimisha kuwa ana ndoa au familia baada ya kupigiwa kelele kwa nini haoi, kuchezea ujana sana, watoto aliozaa nje akitaka apate mtu wa kuwalea yaani awakusanye.

Hapa kuna makundi mengi Kama

1. Waliochelewa kuoa kwasababu ya utafutaji usiokoma au kusoma sana mpaka muda wa kuwa na familia ukataka kuwapa kisogo watu hawa wengi huwa wana changamoto zao kwasababu hawana uzoefu wa mahusiano wao hutaka mahusiano ya haraka sana na kuoana na kuzaa haraka kukimbiza na umri. Mwanamke akichelewa kumzalia huhaha sana na anaweza kuzaa nje.

2. Kundi jingine ni wale wanaokimbia ndoa zao baada ya kuvumilia sana wakaachika ili waoe tena waishi kwa amani hawa huwa walishakuwa kwenye ndoa tayari na wakazikimbia

3. Kundi jingine ni wale wanaotaka kuongeza wake kwa matakwa yao baada ya kuona wamejipata kwenye maisha ya kuona wanahitaji kwasababu wamepata uzoefu wa ndoa nk. Kwahiyo huanzisha mahusiano na ndoa ya pili au zaidi

4. Kundi jingine ni wale waliofeli maisha wanatafuta kuelelewa wanatelekeza ndoa au mahusiano yao ya awali ili wakuelewe.

WANAUME wa umri huu hutafuta single mother, vibinti vidogo wanavyoweza kuvilea muhimu viwazalie watoto hasa ambao wanatoka kwenye familia duni au wanawake wenye uhitaji na ndoa ambao hawachagui mume

DADA YANGU ANGU HAYA NI MACHACHE USIYOYAJUA KWENYE UMRI WA WANAUME NA MAHUSIANO

Ameandika kaka Milton M. Tunge

Haya wadau kwa UZOEFU wako mambo yakoje huko 😀😀
 
tea.jpg
 
Jinsia 'me yoyote >40 years kama si kwa sababu za dini, na hajaoa ni yai viza. Akitokea kuoa anaoa kujipatia mtu wa kumuuguza au kumtunza
Usipende kuhukumu. Unaweza kuoa au kuolewa kwa harusi tena ukacheza na kwaito na ukapata mpk watoto ila ukifikisha 40 ukawa single.
Shilole alikuwa ameolewa ila sasa hivi ni single. Vipi kuhusu Stamina?
Kuna mambo mengi sana, subiri ukue ndiyo utajua kumbe inawezakana ukawa single? Utatega kitumbua, wanakula na hawaoi
 
Comment yake inafanana na ile una umri huo na upo Single unashindwa kujua watu wanaachana kilasiku
 
Unaonekana unacheza kamari sana (betting) hata ulivyoandika umebeat.
Mkeka wako umechanika. Jaribu tena, unaweza kubahatisha
Pole sana😁😁😁😁😁😁😁
 
Nikue mara ngapi tena ndugu Johnny, kuoa/kuolewa sio taji. Ukweli ni kwamba 'me ambao umri umeenda, na ikatokea wanatafuta mwenza huwa ni sababu za ubinafsi kuwa atapata nini kutoka kwenye mahusiano/ndoa hiyo. Show zimeanza kushuka viwango, mwili si kama ule wa enzi zile, afya inaleta taharuki. Kwanini asijipatie binti mdogo ambaye haelewi maisha akamtunza.
Kwa kusema hivi, nawaasa mabinti wachunguze kwa makini wanapokutana na kundi hili la watu. Wasipofushwe kuwa eti ooh, ni mtu mzima ana ekspriensi ya maisha sijui mapenzi. Hatasumbua sasa ameamua kutulia. Ni kwamba tu hana uwezo wa kukusumbua zaidi ya emotional au financial abuse
Binti funguka, kataa ndoa na watu wazima. Same applies kwa mapenzi yenye gap kubwa kiumri 🏃‍♀️‍➡️🏃‍♀️‍➡️🏃‍♀️‍➡️🏃‍♀️‍➡️🏃‍♀️‍➡️
 
Mtu mmoja peke yake hawezi kutengeneza ndoa nzuri, inahitaji watu wawili wenye vichwa, mioyo mizuri inayoendana kuwa na ndoa nzuri. Mmoja akiwa ovyo, ndoa yote ni ovyo
Kwa maana hiyo komenti yako haina maana.
 
Nikue mara ngapi tena ndugu Johnny, kuoa/kuolewa sio taji. Ukweli ni kwamba 'me ambao umri umeenda, na ikatokea wanatafuta mwenza huwa ni sababu za ubinafsi kuwa atapata nini kutoka kwenye mahusiano/ndoa hiyo. Show zimeanza kushuka viwango, mwili si kama ule wa enzi zile, afya inaleta taharuki. Kwanini asijipatie binti mdogo ambaye haelewi maisha akamtunza.
Kwa kusema hivi, nawaasa mabinti wachunguze kwa makini wanapokutana na kundi hili la watu. Wasipofushwe kuwa eti ooh, ni mtu mzima ana ekspriensi ya maisha sijui mapenzi. Hatasumbua sasa ameamua kutulia. Ni kwamba tu hana uwezo wa kukusumbua zaidi ya emotional au financial abuse
Binti funguka, kataa ndoa na watu wazima. Same applies kwa mapenzi yenye gap kubwa kiumri 🏃‍♀️‍➡️🏃‍♀️‍➡️🏃‍♀️‍➡️🏃‍♀️‍➡️🏃‍♀️‍➡️

hoja yako inapingana na uhalisia. binti anataka financial security na utulivu hivyo wanaume wakubwa wengi ndio wapo stable financial na utulivu wanao tofauti na vijana wadogo.

binti akisema aende kwa vijana wa umri wake hao hela hawana. na utulivu hawana. kuoa hawaoi na kutunza hawatunzi. hivyo binti anaona bora aende kwa wanaume wakubwa wakubwa tu
 
Mungu hakukosea aliposema ..umfurahie mke wa ujana wako
 
hupaswi kuingiza mambo ya imani moja kwenye hoja zinazohusisha watu wenye imani tofauti.

duniani kuna imani nyingi na dini nyingi na Mungu wanaemuabudu hajawapa mafundisho yanayofanana.

jifunze kujenga hoja kwa kutumia rationalism na logic
 
Nikue mara ngapi tena ndugu Johnny, kuoa/kuolewa sio taji. Ukweli ni kwamba 'me ambao umri umeenda, na ikatokea wanatafuta mwenza huwa ni sababu za ubinafsi kuwa atapata nini kutoka kwenye mahusiano/ndoa hiyo. Show zimeanza kushuka viwango, mwili si kama ule wa enzi zile, afya inaleta taharuki. Kwanini asijipatie binti mdogo ambaye haelewi maisha akamtunza.
Kwa kusema hivi, nawaasa mabinti wachunguze kwa makini wanapokutana na kundi hili la watu. Wasipofushwe kuwa eti ooh, ni mtu mzima ana ekspriensi ya maisha sijui mapenzi. Hatasumbua sasa ameamua kutulia. Ni kwamba tu hana uwezo wa kukusumbua zaidi ya emotional au financial abuse
Binti funguka, kataa ndoa na watu wazima. Same applies kwa mapenzi yenye gap kubwa kiumri 🏃‍♀️‍➡️🏃‍♀️‍➡️🏃‍♀️‍➡️🏃‍♀️‍➡️🏃‍♀️‍➡️
Wanawake wenyewe ukimtongoza leo gesi imeisha, hana hela ya kula, kodi Imeisha. Ataanzaje kukataa wakati wazee ndiyo wanapiga show nzuri na hela wanatoa (wanajua kutunza).
Vijana wa sasa wanahangaika na vumbi la kongo, Ali kasusu n.k halafu useme hawana uwezo wa kupiga show?
 
hupaswi kuingiza mambo ya imani moja kwenye hoja zinazohusisha watu wenye imani tofauti.

duniani kuna imani nyingi na dini nyingi na Mungu wanaemuabudu hajawapa mafundisho yanayofanana.

jifunze kujenga hoja kwa kutumia rationalism na logic
Kama binti, hauna uwezo sana wa kujua nani na nani watajaribu kutupa jarife kukunasa. Hoja ni kwamba, wawe makini sana kuchunguza hususan walio na umri uliyoenda, kuna sababu (kasoro) kubwa inayofanya wawepeke yao (kama sio kwa sababu za kidini) Na waepuke watu hao
 
Unaonekana unacheza kamari sana (betting) hata ulivyoandika umebeat.
Mkeka wako umechanika. Jaribu tena, unaweza kubahatisha
Pole sana😁😁😁😁😁😁😁
Niko na mahusiano yangu stable Mkuu bado ndoa
 
Wanawake wenyewe ukimtongoza leo gesi imeisha, hana hela ya kula, kodi Imeisha. Ataanzaje kukataa wakati wazee ndiyo wanapiga show nzuri na hela wanatoa (wanajua kutunza).
Vijana wa sasa wanahangaika na vumbi la kongo, Ali kasusu n.k halafu useme hawana uwezo wa kupiga show?
Makundi yote matatu uliyotaja kwa tabia zao hawajielewi.
1. Binti unayetegemea kutunzwa na mtu ambaye sio mzazi/mlezi wako au mume mtarajiwa (mtu anayefahamika kwenu, mahari ametoa na tarehe ya ndoa inajulikana)

2. Mtu mzima unashindana na watoto

3. Kijana muasherati asiyejua sanaa ya kufanya mapenzi
 
Hayo yalikuwepo na yataendelea kuwepo na utayaacha.
Kila unachoona kibaya kwako, kwa mwingine ni kizuri
 
Back
Top Bottom