Kabla ya kulaumu tujiulize Je, wabunge wa upinzani wanatekeleza Ilani ya uchaguzi ya CCM?

johnthebaptist

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2014
Posts
104,319
Reaction score
183,639
Tuanzie pale bungeni je wapinzani huwa wanaunga mkono hoja za serikali ya CCM?

Kwenye mabaraza ya madiwani je wapinzani wanashirikiana na CCM kuleta maendeleo?

Tukijiridhisha ndio tutaona umuhimu wa kuongozwa na wabunge wa "chama tawala" ili kukoleza kasi ya maendeleo.

Nawatakia Eid Mubarak

Maendeleo hayana vyama!
 
Vyama vya upinzani ulianzishwa kuwa kama catalyst ya serikali kufanya kazi na kutokujisahau.

Ni kwa ajili ya kuangalia mapungufu yoyote ya serikali iliyoko madarakani ili kuyaibua na kuwaambia wananchi mapungufu hayo katika jitihada za wao pia kushika dola.

Kwa kufanya hivyo serikali inajikuta inakomaa ili kuyafanyia kazi madudu yanayoibuliwa na upinzani ili wananchi wasivote against, na mwisho wa siku ni faida kwa wananchi kuletewa maendeleo.

Upinzani ukiwa unaunga mkono kila kinachofanywa na serikali basi inakuwa hakuna haja ya uwepo wa upinzani.
 
Tuanzie pale bungeni je wapinzani huwa wanaunga mkono hoja za serikali ya CCM?

Kwenye mabaraza ya madiwani je wapinzani wanashirikiana na CCM kuleta maendeleo?

Tukijiridhisha ndio tutaona umuhimu wa kuongozwa na wabunge wa "chama tawala" ili kukoleza kasi ya maendeleo.

Nawatakia Eid Mubarak

Maendeleo hayana vyama!
Huna hata aibu, eti maendeleo hayana vyama wakati spika hajasema ile kauli ya jana ifutwe.
 
Tuanzie pale bungeni je wapinzani huwa wanaunga mkono hoja za serikali ya CCM?

Kwenye mabaraza ya madiwani je wapinzani wanashirikiana na CCM kuleta maendeleo?

Tukijiridhisha ndio tutaona umuhimu wa kuongozwa na wabunge wa "chama tawala" ili kukoleza kasi ya maendeleo.

Nawatakia Eid Mubarak

Maendeleo hayana vyama!

Hao wabunge wa ccm huwa wanaunga mkono hoja za upinzani? Ni vyema mahali walipo chaguliwa wapinzani kodi zao zitumike kuendeleza majimbo yao.
 
Labda nikufundishe kwa mifano maana ya Mpinzani!!

Kwa kabisa mpinzani sio adui, mpinzani ni mtu yoyote kwenye mawazo tofauti na wewe yanaweza kuwa na maana au la, kwa kifupi mpinzani wanatakiwa wajibiwe kwa mifano ilivyo sahihi. ( sio risasi)

Je unadhani CAG aliye weka upoteaji wa fedha kwa kiasi cha shillings Trillion 1.5 ni mjinga?

Je unadhani wapinzani wanaosema miradi mingi haikupita bungeni ni wajinga?

Je Mimi nikisema rais Mkapa kakiri kuiba fedha zetu,na serikali imekaa kimya unadhani si utaweza kuwa ndio mchezo wa rais kila siku,je mimi ni mjinga?

Swali la kufikirika kwa kwako

Kwanini Mabadiliko Ya Sheria Zetu Huwa Yanaandikwa Kwa Kingereza? Huwa Wanataka Tusome Tusielewe,Tukosee Watupeleke Kweye Vidirisha Vidogo Vyenye Mwanga Hafifu?

Lengo Huwa Ni Lipi ?Kwanini Wasiweke Sheria Hizo Kwa Kiswahili? Anyway Labda Ukoloni Still Unafanya Mambo Mpaka Leo!

Mpinzani mtu muhimu sana katika nchi yako.

Mr mkiki
 
Tuanzie pale bungeni je wapinzani huwa wanaunga mkono hoja za serikali ya CCM?

Kwenye mabaraza ya madiwani je wapinzani wanashirikiana na CCM kuleta maendeleo?

Tukijiridhisha ndio tutaona umuhimu wa kuongozwa na wabunge wa "chama tawala" ili kukoleza kasi ya maendeleo.

Nawatakia Eid Mubarak

Maendeleo hayana vyama!
Inaonyesha hata kazi au majukumu ya Vyama ya Upinzani hujui toka lini chama cha Upinzani kikatekeleza Ilani ya Chama Tawala? Kwa Tanzania labda vyama tanzu na ccm kama vile Tlp Cuf Udp na Nccr ,Ccm kwa sasa inatekeleza Ilani ya Chadema ndio maana utawasikia viongozi wanasema Vyote walivyosema Chadema Ccm imetekeleza.
 
Kwa kuchangia hoja hii, niseme hivi. Kama serikali haitaki kuwepo vyama vya upinzani haviwezi kuwapo na maadamu vipo ina maana serikali imeridhia viwepo. Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, linaamua jambo kwa mfumo wa kura na ukishaweka kura ina maana kuna kura za ndiyo, hapana na ama za kuharibika au kutopiga. Kura zitakazokuwa nyingi ndizo zinazochukuliwa kuwa uamuzi wa Bunge na uamuzi huo unawa'bind' wabunge wote bila kujali nani alipiga kura ya ndiyo, hapana au hakupiga kura. Kupitisha bajeti au muswada wa sheria kunafuata utaratibu huu pia. Bejeti ikishapita inakuwa imepita kwa wote na hata muswada wa sheria fulani ukipigiwa kura za ndiyo na wabunge wengi, ina maana muswada huo umepitishwa na unapelekwa kwa Rais ili ausaini iwe sheria. Kama kuna vipengele Rais anaona ni lazima vibadilishwe, muswada hurejeshwa bungeni ili vipengele hivyo virekebishwe/viboreshwe.

Sheria yoyote ambayo imepitishwa inawa'bind' waliopiga kura ya ndiyo, hapana na wale ambao hawakupiga kura pia, wakiwemo wananchi wote waliowakilishwa na wabunge wao. Ndio utaratibu wetu wa kupiga kura ulivyo. Kuna baadhi ya wachangiaji wanadhani bajeti au muswada wa sheria ukipigiwa kura na wabunge na ikatokea kukawa kura za ndiyo na hapana, basi waliopiga kura za ndio wanaotaka maendeleo na hivyo fedha zingepelekwa majimboni kwao na wale waliopiga kura za hapana wanyimwe ili wajifunze kupiga kura za ndiyo. Ni sawa na kusema pia kodi au sheria ikipitishwa basi huwa inawahusu tu waliopiga kura za ndiyo na waliopiga kura za hapana kodi au sheria husika haiwahusu. Je, ni kweli ndivyo inavyokuwa? Kama siyo, basi inabidi tujielimishe maana ya kupiga kura ni nini. Mfano, hata viongozi ngazi ya kijiji, kata, madiwani, wabunge na Rais wanapigiwa kura za ndiyo au hapana na kura nyingine huharibika na wananchi wengine hawapigi kura kabisa. Lakini kiongozi wa kijiji, kata, diwani, mbunge au Rais akishashinda uchaguzi anakuwa kiongozi wa wote - yaani wa waliompigia kura za ndiyo au hapana na hata wa wale ambao hawakupiga kura. Hivi ndivyo ninavyoelewa utaratibu kwa kura ulivyo.
 
Mindset ya CCM na Magufuli ni kwamba upinzani ni maadui.

Wapinzani wameongea na wametoa maoni mengi sana sema hayapewi kipaumbele maana wanaonekana ni maadui.

Sasa unapataje nguvu kulaumu wapinzani?
 
Tuanzie pale bungeni je wapinzani huwa wanaunga mkono hoja za serikali ya CCM?

Kwenye mabaraza ya madiwani je wapinzani wanashirikiana na CCM kuleta maendeleo?

Tukijiridhisha ndio tutaona umuhimu wa kuongozwa na wabunge wa "chama tawala" ili kukoleza kasi ya maendeleo.

Nawatakia Eid Mubarak

Maendeleo hayana vyama!
Hii haiondoi ukweli kwamba Rais wetu ni mbaguzi wa dhahiri
 
Inaonyesha hata kazi au majukumu ya Vyama ya Upinzani hujui toka lini chama cha Upinzani kikatekeleza Ilani ya Chama Tawala? Kwa Tanzania labda vyama tanzu na ccm kama vile Tlp Cuf Udp na Nccr ,Ccm kwa sasa inatekeleza Ilani ya Chadema ndio maana utawasikia viongozi wanasema Vyote walivyosema Chadema Ccm imetekeleza.
Bwege anatekeleza ilani ya chama gani bwashee?
 
Tuanzie pale bungeni je wapinzani huwa wanaunga mkono hoja za serikali ya CCM?

Kwenye mabaraza ya madiwani je wapinzani wanashirikiana na CCM kuleta maendeleo?

Tukijiridhisha ndio tutaona umuhimu wa kuongozwa na wabunge wa "chama tawala" ili kukoleza kasi ya maendeleo.

Nawatakia Eid Mubarak

Maendeleo hayana vyama!
Kuna mkoa wenye maendeleo halisi kama Kilimanjaro blicha ya kuwa chini ya upinzani mda mrefu? Naelewa sasa kwa nini inatumika nguvu kubwa kumpamba kwa misifa fake kumbe ni kujaribu kuficha aibu ya udhaifu na uovu wake
 
Tuanzie pale bungeni je wapinzani huwa wanaunga mkono hoja za serikali ya CCM?

Kwenye mabaraza ya madiwani je wapinzani wanashirikiana na CCM kuleta maendeleo?

Tukijiridhisha ndio tutaona umuhimu wa kuongozwa na wabunge wa "chama tawala" ili kukoleza kasi ya maendeleo.

Nawatakia Eid Mubarak

Maendeleo hayana vyama!
Hivi kazi za bunge na wabunge siku hizi imekuwa kutekeleza ilani za vyama na kufanya kazi za serikali badala ya kutunga sheria na kujisimamia serikali,naomba kujuzwa
 
Hahahaaaa....... Bunge linapitisha miswada kuwa sheria.

Kazi za mbunge ni pamoja na kuchochea maendeleo ya jimbo lake!
 
Kauli hizi zitaisha itakapofika pale maendeleo kwa Tz siyo maji au umeme au barabara. Nchi ambazo kwao haya siyo maendeleo tena Rais hua anaangalia cha kusema.

So leo mbunge anapigiwa kampeni kwa wanaotakiwa kumpa kura kutishiwa juu ya barabara. Hili siyo tatizo as kwetu Tz Rais hakosei, tatizo ni wanapotokea watu wanaotetea alichokisema. Siwezi kua upande wake kwemye hili
 
Tuanzie pale bungeni je wapinzani huwa wanaunga mkono hoja za serikali ya CCM?

Kwenye mabaraza ya madiwani je wapinzani wanashirikiana na CCM kuleta maendeleo?

Tukijiridhisha ndio tutaona umuhimu wa kuongozwa na wabunge wa "chama tawala" ili kukoleza kasi ya maendeleo.

Nawatakia Eid Mubarak

Maendeleo hayana vyama!
Mkuu umelewa pilau ya Eid?
 
Hahahaaaa....... Bunge linapitisha miswada kuwa sheria.

Kazi za mbunge ni pamoja na kuchochea maendeleo ya jimbo lake!
Mkuu hii ya kuchochea maendeleo ni kwa mujibu wa katiba yetu au ilani ya ccm
 
Back
Top Bottom