Kabla ya kumtimua kocha angalia usoni wachezaji wako kwanza

Kabla ya kumtimua kocha angalia usoni wachezaji wako kwanza

kavulata

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2012
Posts
13,778
Reaction score
14,214
Kazi ya kocha wa timu ni kuratibu wachezaji kwa kutumia vipaji vyao TU, sio vingine. Kazi ya kuhakikisha fitness ya wachezaji ni ya kocha wa viungo, kazi ya kuhakikisha kuwa wachezaji, Wana furahà, Wana morali ya kucheza kwa bidii ni kazi ya uongozi wa timu.

Kabla ya kumfukuza kazi kocha kwa timu kufanya vibaya Jiulize kwanza ulitaka timu yako ipate matokeo kama timu ipi kwenye mashindano husika? Kisha ndio ujiulize kama kocha wako amepewa wachezaji wenye vipaji na afya kama wale wa timu zinazoshinda kwenye ligi.

Je, wanalipwa vizuri kwa wakati? Je, wanatibiwa na kula vizuri? Je, wanasafiri kama wanavyosafiri wale wa timu zinazoshinda? Je makocha wa fitness wapo kama kule kwa wanaoshinda? Je, kocha na wachezaji hawakudai?

Kama jibu ni ndiyo kwenye kila swali ni haki kumtimua kocha. Kama jibu ni Hapana kwenye swali mojawapo basi ujue unajihangaisha Bure kumtimua kocha.
 
Back
Top Bottom