Kabla ya Lissu, Waziri wa Ujenzi atembelea barabara ya Rusahunga - Rusumo

brazaj

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2016
Posts
34,775
Reaction score
46,063
Mabibi na mabwana heshima kwenu na moja kwa moja kwenye mada.

Wakati akisubiriwa yule mheshimiwa mfufuka kujili pande za huko Rusumo, msafara wa magari likiwamo lenye plate number: W UJ umeonekana katika barabara hii uelekeo Rusumo.

Gari W UJ likipepea bendera yetu tukuka vilivyo likiaashiria uwepo wa mnene huyo msafarani.

Hiyo bado ni habari njema kwani haiyumkiniki hali nzima ilivyo kaishuhudia vyema na habari yenyewe ataifikisha kwa bwana mkubwa live bila chenga:

"Si vishindo bali ni majanga!"

Haiyumkiniki pia kayaona haya yaliyosababishwa na huo ubovu usio mithilika wa barabara hii kwa baadhi ya wapiga kura:

IMG_20200812_141849_518.jpg

IMG_20200812_141629_466.jpg

IMG_20200812_141710_769.jpg

IMG_20200810_152339_062.jpg

IMG_20200808_090622_003.jpg

Zote hizi zikiwa baadhi tu ya ambazo zingalipo barabarani.

Kwenu watia nia. Pana kura za kumwaga pande za huko.

Watanzania ni wenye kusamehe na kuadibu ikibidi.
 
Mimi nikusifu kwa jinsi unavyoupigania barabara hii, nia yako itatimizwa Mungu ni mkubwa.

Si barabara hii tu wala barabara tu mkuu. Bali mstakabala mzima wa nchi yetu kwa ujumla. Ukizingatia maendeleo, uhuru, usawa, haki nk, havina vyama.

Tokea kwenye Corona hadi katiba mpya. Tokea JKNIA hadi Uhuru. Lupaso nilishindwa.

Bila kuacha kuwaasa tume ya uchaguzi, polisi, mahakama na mzee baba wasituvurugie uchaguzi. Tanzania kama nchi inastahili vilivyo bora na vilivyo haki.

Watanzania wazalendo hatuuwani wala kupotezana. Tunarumbana kwa hoja.

Waamuzi wanapaswa kuwa wajumbe si mwingine maana tunataka rais:

IMG_20200804_210728_515.jpg

Barabara, Corona, na mafyongo yote yanaanikwa hivi ili pia wajue:

1. Wakibadilika sisi ni watu wa kusamehe.
2. Wakishupaza Shingo, tusilaumiane.

Kwenye hayo tushakirimiwa uraia wa nchi nyingi hadi ufilipino:

Wito: Chonde chonde, Tanzania ni zaidi mno ya yeyote

Muda wa kuiponya nchi yetu ni sasa
 
Kabisa, huyu jamaa anapaswa kuungwa mkono kwa hii kelele yake kuhusu hiyo barabara.

Mkuu ingependeza zaidi kuungana mikono kwenye kelele za kuhusu mstakabala mwema wa nchi yetu. Hii barabara ni agenda moja kwani ina declare bandari ya Dar kuwa mfu katika hali ilivyo "to the detriment of us all."

Mengine ni mstakabala wa Corona ambayo haitaondoka kwa kuukimbia ukweli kuhusiana na yenyewe.

Mengine nyeti zaidi ni hawa kina tume ya uchaguzi, polisi, mahakama, jiwe kama watataka kuingilia suala zima la uchaguzi ujao kinyume cha haki.

Ni vyema ikafahamika kuwa Tanzania hii ni yetu sote. Mtu mmoja na asije taka kujifanya kuwa yeye ni mzalendo sana kuliko mwingine.
 
Mkuu nakuunga mkono kwa nondo hizi.
 
nilimsikia naibu waziri wa ujenzi akisema

tayari washapatikana wakandarasi watatu kwa ajili ujenzi wa barabara eneo hilo.

Mkuu Magufuli alishasema si mara moja kuwa pesa za kujenga hii barabara anazo. Hiyo ni tokea 2015.

Maneno matupu hayavunji mfupa.

Hadi leo hamna lolote na hali inazidi ikiwa mbaya kila siku inayopita: vishindo vya awamu ya tano.

Hali ya mbaya mno ya barabara Nyakanazi Rusumo vipaumbele vyetu ni nini?

Ziara ya Kagera, Magufuli usiende pekee tu Wasaidizi wako wanakokupangia kwenda

Hata kuziba sehemu mbovu hamna?

Too much au vipi?
 
Mabibi na mabwana heshima kwenu na moja kwa moja kwenye mada.

Wakati akisubiriwa yule mheshimiwa mfufuka kujili pande za huko Rusumo, msafara wa magari likiwamo lenye plate number: W UJ umeonekana katika barabara hii uelekeo Rusumo.

Gari W UJ likipepea bendera yetu tukuka vilivyo likiaashiria uwepo wa mnene huyo msafarani.

Hiyo bado ni habari njema kwani haiyumkiniki hali nzima ilivyo kaishuhudia vyema na habari yenyewe ataifikisha kwa bwana mkubwa live bila chenga:

"Si vishindo bali ni majanga!"

Haiyumkiniki pia kayaona haya yaliyosababishwa na huo ubovu usio mithilika wa barabara hii kwa baadhi ya wapiga kura:

Zote hizi zikiwa baadhi tu ya ambazo zingalipo barabarani.

Kwenu watia nia. Pana kura za kumwaga pande za huko.

Watanzania ni wenye kusamehe na kuadibu ikibidi.
Tunamuomba Tindu Lusu atembelee Barabara zifuatazo kabla ya tarehe 25.8.2020
1. Tarime Hadi mungumu Serengeti
2. Geita mjini kupitia msalala Hadi Kahama
3. Katoro mjini Hadi ushirombo
4. Geita mjini Hadi nzera Jimbo I kwa Joseph msukuma
5.Kahama Hadi mgodi mkubwa wa dhahabu bulhyankulu
6. Mererani Hadi kiteto
7.Kiteto Hadi dodoma
8. Msasi wilaya ya misungwi mwanza Hadi Kahama
 
Pamoja na ubovu wa hiyo barabara kuwa hivyo, ila matukio mengi ukiangalia hizo ajali ni swala la driving habit.
Mkuu hiyo Barabara ni zaidi ya hii comment yako...... Ni mbovu Sana afu iko sehemu za milima,miteremko mikali na Kona Kona balaa.
Salute to those drivers.

Hii Barabara inawavua Sana nguo Hawa viongozi wetu
 
Ni kweli barabara hiyo ni mbovu sana. Napo pia lazima tuangalie swala la nidhamu ya uendeshaji wa hivyo vyombo haswa maeneo kama hayo. Kuna human reckless nyingi kuliko ubovu wa hiyo barabara.

Waliopita NIT au other professional driving institutions wataelewa.
 
Dr. Magufuli, kwa ajili ya Tanzania.

Wengine hao waambie wakakojoe kisha wakalale.
 
Tatizo si mtu wala jina. Hapendwi mtu hapa!

Yeyote mwenye haya ni wetu:

IMG_20200804_210728_515.jpg

Kama anayo hayo tutakwenda naye kama tutavyokwenda na Lipumba, Lissu, Membe, Hashim nk.

Kama hana anaweza kuyajifunza hata sasa kwani angalia haja chelewa.

Kama hataki au hawezi, wala usipate taabu mkuu huyo tuachie wajumbe. Kwani hatukumwambia tunataka nini?

Eboo! Wala tusipigishane kelele.
 
Mabibi na mabwana heshima kwenu na moja kwa moja kwenye mada.

Wakati akisubiriwa yule mheshimiwa mfufuka kujili pande za huko Rusumo, msafara wa magari likiwamo lenye plate number: W UJ umeonekana katika barabara hii uelekeo Rusumo.

Gari W UJ likipepea bendera yetu tukuka vilivyo likiaashiria uwepo wa mnene huyo msafarani.

Hiyo bado ni habari njema kwani haiyumkiniki hali nzima ilivyo kaishuhudia vyema na habari yenyewe ataifikisha kwa bwana mkubwa live bila chenga:

"Si vishindo bali ni majanga!"

Haiyumkiniki pia kayaona haya yaliyosababishwa na huo ubovu usio mithilika wa barabara hii kwa baadhi ya wapiga kura:

Zote hizi zikiwa baadhi tu ya ambazo zingalipo barabarani.

Kwenu watia nia. Pana kura za kumwaga pande za huko.

Watanzania ni wenye kusamehe na kuadibu ikibidi.
Tatizo la hizi ajali, hasa kama zinavyoonekana kwenye picha, ni barabara mbovu au ni upakiaji hafifu usiozingatia uzito, uwiano wa uzito na kutokufunga vizuri mizigo hadi ama inasogea upande mmoja na kusababisha gari kupinduka?
 
Mizigo inaacha vipi kusogea upande mmoja kama hali ya barabara ni mbaya kiasi hiki?

Magari yanaacha vipi ku 'tilt' yaani kulalia mno upande na upande kama barabara ni mbaya mno?

Vipi barabara kama barabara limekuwa tifu tifu mno kiasi cha mguu kuzama kwenye vumbi hata kufikia hata futi nzima ndani ya vumbi kama mtu akitia mguu chini?

Kwani kuna hata haja ya kutafuta mchawi?

Mzizi wa fitina ni ubovu wa barabara pekee.

IMG_20200808_113420_115.jpg
 
nilimsikia naibu waziri wa ujenzi akisema

tayari washapatikana wakandarasi watatu kwa ajili ujenzi wa barabara eneo hilo.

Kumbe naibu waziri aliyasema hayo jana? Hiyo ni habari njema sana.

Acha tufuatilie ndani ya wiki 2 tuone kama angalau mashimo yanayopelekea ajali hizi yatazibwa.

Mtanzania ni mwenye kusamehe hata mzee baba akiokoka leo akawa huyu:

IMG_20200804_210728_515.jpg

Mbona wengi tu tutasema Magufuli tosha!

Kama hana hayo bora atangulie Chatto tu.

Hapendwi mtu hapa!
 
Back
Top Bottom