Kabla ya Tanga ya leo ni shughuli gani za kibiashara zilikuwa zinaendelea mkoani humo?

Kabla ya Tanga ya leo ni shughuli gani za kibiashara zilikuwa zinaendelea mkoani humo?

Atukuzwaye

Senior Member
Joined
Oct 5, 2026
Posts
191
Reaction score
250
Tunapozungumzia Tanga mara nyingi tunafikiria mji wa bandari tunaoujua leo. Lakini kabla ya Tanga ya kisasa, kulikuwa na vituo vya kale vya kibiashara ambapo katika pwani hii.

Moja ya hivyo ni Tongoni.

Magofu ya Tongoni ni magofu ya Waswahili ya karne ya 15 ya msikiti na makaburi arobaini yaliyopo katika kata ya Tongoni wilayani Tanga ndani ya Mkoa wa Tanga nchini Tanzania.

Tongoni ilikuwa sehemu ya mtandao wa biashara uliounganisha pwani ya Afrika Mashariki na Bahari ya Hindi. Mabaki ya majengo, msikiti na makaburi yanaonesha pia uwepo wa jamii iliyokuwa na mfumo wa maisha, imani na utamaduni uliokuwa umejengeka katika mazingira ya Pwani.

Kwa hiyo, Tongoni si mabaki ya magofu tu; bali ni ushahidi wa historia ya miji ya waswahilina nafasi ya Pwani ya Tanga katika ulimwengu wa zamani wa biashara ya bahari ya Hindi.
Tongoni_ruins_6.jpg
Details_3_Tongoni.jpg
Swahili_Monumental_Tomb,_Tongoni,_Tanzania (1).jpg


Lakini swali linabaki:
Tongoni ilikuwa na umuhimu gani katika biashara ya zamani, na ni nini kilichosababisha mji huu kupungua na kubaki magofu?

Na zaidi ya hapo,
Je, ni vituo gani vingine vya biashara vilikuwepo katika pwani ya Tanga kabla ya Tanga kuwa mji mkubwa wa bandari tunaoujua leo?
 
Back
Top Bottom