kavulata
JF-Expert Member
- Aug 2, 2012
- 13,778
- 14,214
- Thread starter
- #21
Asikudanganye mtu, amani yetu hii imetokana na uwepo wa ardhi kubwa kuliko mahitaji ya watanzania pamoja na sera yetu ya ardhi. Siku ardhi ikiwa ndogo kuliko mahitaji ya watu wetu amani yetu itatoweka. Migogoro ya wakulima na wafugaji na wachimbaji ni dalili ya kupungua ardhi ya kufugia na kulima.Jambo muhimu sana kulitazama ni hilo la ardhi, kusipokuwepo umakini kwenye suala la ardhi ipo siku tutakutana na madalali watakaoidanganya serikali kubadili sheria za ardhi na mwisho wa siku yatukute yanayoendelea Israel na Palestina
Tanzania inataka haitaki ni lazima ipime na kutenga ardhi ya makazi, kilimo, uchunguji, uchimbaji, viwanda na hifadhi. Ardhi hizi zisipunguzwe wala kuongezwa hata kwa sentimita moja. Ni bora watu wajenge nyumba za ghorofa kwenda juu kuliko kusambaa kwenda kumega maeneo mengine yaliyotengwa kwa kazi nyingine.