CONSISTENCY
Senior Member
- Feb 16, 2023
- 135
- 309
Hivi kweli ninyi wote mmekubaliana na huo mkataba wa kuuza bandari?
Bandari ndio mali kubwa tuliyobakiwa nayo sasa, nchi zote zilizotuzunguka zinatupa heshima sababu zinategemea bandari zetu kupitisha mali na mizigo yao. Ikumbukwe kwamba serikali imekua inatumia pesa nyingi kuirekebisha bandari kila wakati.
Hivi ninyi wanasiasa mnashindwa kutetea mustakabali wa Taifa letu na vizazi vijavyo sababu ya kulinda vyeo na nafasi zenu za kisiasa?
Huo mkataba wa bandari hauhusiani na siasa na kuna raia wengi sana, raia wengine ni wanasheria wazoefu wamekosoa mkataba wa bandari kwa uwazi kabisa kwamba huo mkataba una mapungufu makubwa yenye lengo la kuuza sehem muhim katika nchi yetu.
Kwanini mkataba unakua mzuri kwa watu wachache waliopo CCM tu ila unapingwa na asilimia kubwa ya wananchi na wakati wote tupo katika nchi moja?
CCM mnafaidika nini na huo mkataba hadi mmeamua kuwalinda hao waarabu kwa jambo hatari kwa nchi kama hilo?
Dkt. Bashiru Ally, Humphrey Polepole, Profesa Kabudi, Waziri mkuu Kasim Majaliwa na wazalendo wengineo, ninyi pia mmekubali huyo bibi awazidi akili hadi kufanya jambo la kuhatarisha nchi kama hilo na mpo kimya, ili kulinda nafasi zenu za kisiasa?
Wito wangu kwa watanzania, tujifunze kulinda mali zetu kwa vizazi kwa namna nyinginezo ikiwemo maandamano na migomo kuliko kutegemea wanasiasa washenzi wanaojali matumbo yao ya kifisadi na kusahau hatma kubwa ya nchi na urithi wake.
Hili jambo la bandari haliwezi kupita hivi hivi, lazima tufute huo mkataba kwa heri au kwa shari