Ulaya usingesikia kiongozi kama Kabudi tena mwenye elimu ya Profesa akakaa kimya bila kutoa maoni yake kuhusiana na suala linalovunja baadhi ya vifungu kwenye sheria mama ya nchi kama Katiba. Mbaya zaidi tena suala lenyewe lipo kwenye eneo lake la kujidai.Viongozi waoga kama hawa, hawatufai kabisa.
Kiongozi lazima ajitoe muhanga kwa ajili ya anaowaongoza. Na ndiyo maana huwa tunawapa heshima na taadhima zote kama viongozi wetu. Sasa cha kushangaza, asilimia kubwa ya viongozi tulio nao, wanapenda tu heshima na privilege zingine za kiongozi, ila ni waoga sana linapokuja suala la kuji-sacrifice!
Ndo maana nathubutu kusema sisi kama nchi, tumebahatika kuwa na viongozi kwa maana ya viongozi kweli wachache sana kama vile Hayati JPM, JKN, Sokoine, BWM, Gen Mtukula, n.k. wengine ni wapigaji tu kama wapigaji wengine.
Useless kabisa, sasa anao watoto na wajukuu na vitukuu...asipowapigania vyema kuweka mazingira mazuri ya wao kuja kuishi kwenye nchi nzuri faida yake ni nini sasa? Akumbuke kuwa kwa umri wake ata akijaliwa kuja kufa kwa natural death hawezi kuishi zaidi ya miaka 40 kutoka sasa...anachogopa ni nini sasa.
Eti profesa.