Tetesi: Kabudi: Sifahamu wao kuhusu mimi nimechagua kuishi

Tetesi: Kabudi: Sifahamu wao kuhusu mimi nimechagua kuishi

Kabudi ni mfano wa wasomi wengi wa kitanzania walivyo, wengi ni waganga njaa tu ndio maana ktk kupambana na maisha lazima wajiunge na ccm ili wapate short cut ya maisha. Bure kabisa.
 
Viongozi waoga kama hawa, hawatufai kabisa.
Kiongozi lazima ajitoe muhanga kwa ajili ya anaowaongoza. Na ndiyo maana huwa tunawapa heshima na taadhima zote kama viongozi wetu. Sasa cha kushangaza, asilimia kubwa ya viongozi tulio nao, wanapenda tu heshima na privilege zingine za kiongozi, ila ni waoga sana linapokuja suala la kuji-sacrifice!
Ndo maana nathubutu kusema sisi kama nchi, tumebahatika kuwa na viongozi kwa maana ya viongozi kweli wachache sana kama vile Hayati JPM, JKN, Sokoine, BWM, Gen Mtukula, n.k. wengine ni wapigaji tu kama wapigaji wengine.

Yaani kiongozi atakayejitoa mhanga Kwa Watanzania Kwa kweli nitamshangaa Sana.
Sisi Watanzania tunastahili kukarangizwa tuu.
 
Licha kwamba ccm siitaki! Lakini ukweli ni kwamba, Kabudi ni akili kubwa! Mengine ni siasa za kijinga
Akili kubwa aitoe wapi, huyo aliyekunywa dawa hadharani ambayo haina udhibitisho wa Kimaabara, halafu anakuja na story za kijinga eti hii dawa kule Madagascar anagawa rais tu.

Kwa mtazamo wake anamuona rais ni kama Mungu. Halafu wiki iliyofuata baada ya kutumia ile dawa ambayo haijadhibitishwa kimaabara, Covid ikaenea kwa kasi huko Madagascar! Pale ndio nilidharau sana elimu ya hilo zee pigania tumbo.
 
Diplomasia ipi aliua unaweza kueleza
Huyu dingi akiwa waziri mambo ya nje Tanzania tuliingia uhasama na Kenya, Rwanda, marekani na umoja wa ulaya, just imagine Kwa muda mfupi alivokaa wizara hiyo kavuruga mahusiano laiti mama angechelewa kumtoa asaivi tungekuwa na mafarakano dunia nzima
 
Kabudi ni mfano wa wasomi wengi wa kitanzania walivyo, wengi ni waganga njaa tu ndio maana ktk kupambana na maisha lazima wajiunge na ccm ili wapate short cut ya maisha. Bure kabisa.
We ungejiunga na chama Gani mkuu?
 
"....mwanangu nina watoto kama wewe na wajukuu pia katika muktadha huo hunibidi hasa kwa wakati huu ning'amue baadhi ya mambo kwa umakini mkubwa na ndiyo maana nimekujuza kuhusu u muhimu wa umri niliobakiwa nao niutumie kuishi vyema na wao."

"....jawabu langu li bayana sitogombea!"

Profesa.
Professa ni mzuri kwenye mihadhara yenye lengo la kukosoa.

Professa tutamkumbuka kwa kumuita mwanadam Mungu.

Aidha asije akasema ameombwa na wananchi agombee tena.
 
"....mwanangu nina watoto kama wewe na wajukuu pia katika muktadha huo hunibidi hasa kwa wakati huu ning'amue baadhi ya mambo kwa umakini mkubwa na ndiyo maana nimekujuza kuhusu u muhimu wa umri niliobakiwa nao niutumie kuishi vyema na wao."

"....jawabu langu li bayana sitogombea!"

Profesa.
Kwani alishawahi kugombea na kushinda?lini na wapi? Hivi kabudi hiyo siasa aliifanya wapi hadi axhaguliwe kuwa mbunge hapo 2020.
Tuache uzuzu!
 
We ungejiunga na chama Gani mkuu?
Sio lazima ujiunge na chama chochote cha siasa, ni sawa tu na dini kwani sio lazima uwe muumini wa dini yoyote eti ndio uingie mbinguni. Hizi dini ni usanii tu wa wanadamu.
 
"....mwanangu nina watoto kama wewe na wajukuu pia katika muktadha huo hunibidi hasa kwa wakati huu ning'amue baadhi ya mambo kwa umakini mkubwa na ndiyo maana nimekujuza kuhusu u muhimu wa umri niliobakiwa nao niutumie kuishi vyema na wao."

"....jawabu langu li bayana sitogombea!"

Profesa.
Mfalme amekaa uchi wa mnyama mbele ya halaiki, huku akiwa ameaminishwa kuwa kavaa nguo ya ghali sana na yenye thamani kubwa kupitiliza. Ila kaaminishwa ukiwa mdhambi huwezi kuiona wala kuhisi uwepo wake!

Anatambua fika, na kwa dhati kabisa kuwa naye pia ni mdhambi mkubwa, na ndiyo maana pale alipovikwa vazi hilo, hakuliona wala kulihisi uwepo wake mwilini mwake. Kundi kubwa la wanafiki limemzunguka hali likimsifia kuhusu uzuri na uthamani wa hali ya juu wa mavazi mapya ya kifalme aliyoyavaa.

Wanauona uchi wake, na aibu ya kujiweka uchi mbele ya hadhara. Lakini kutokana na unafiki hakuna mwenye uthubutu wa kumwambia afiche aibu yake. Mara sauti ya mtoto asiyekuwa na hatia inaibuka na kuleta taharuki kubwa.

Sauti ya haki na tahadhari inapenya na kusikika ikisema, MFALME U UCHI". Taharuki inatokea kwa wanafiki dhidi ya wapenda haki na wakweli. Hoja inabaki kuwa, watu wakubali uongo ili kulinda hadhi ya kiti cha mfalme na ufalme wake, ama la, mfalme aambiwe ukweli ili aweze kuificha aibu yake, na juu ya mwili wake yeye mwenyewe?
 
Back
Top Bottom