Hizo ndio sababu nchi nyingine huwa wana train industry expert baadae wakasome masters law mwaka mmoja au miwili sio ata lazima wawe wanasheria kamili.
Unaingia kwenye negotiation unakutana LLB mtaalamu maswala ya management kwenye extractive industry au oil and gas, unakutana na tax lawyer (usually hawa ni qualified accountants nchi za wenzetu), kuna geologists, kuna mtaalamu wa international law, mtaalamu wa dispute resolution na kila ghasia muhimu kwenye mkataba husika (wote hao well trained in negotiations skills on top of their qualifications).
Halafu wewe una timu inayoongozwa na Kabudi hana uelewa wowote wa biashara, finance, geology wala industry husika; unapigwa kabla majadiliano ayajaanza.
Ni sawa na kumsikiliza January akiongelea mkataba wa ‘oil and gas’ kwenye kichwa chake easy ngoja ukosee uingie kichwa kichwa utapigwa kwa muda mrefu sana. Hayo mambo bei ya nishati tu inachangia nini unapata bei ikishuka sana watu wanaendelea kuzalisha na wewe usipate chochote kama hujui source ya hizo $30 billion unazoshadadia tena ambazo likely ni over estimated investment ili wanyonye tu kwa muda mrefu.
Umenena vizuri sana.
Ukweli ile timu ya Kabudi Vs Barrick, ile ya Kabudi ilikuwa kichekesho kitupu. Halafu Kabudi akawa anajitapa eti timu ya Barrick ilikuwa na wajumbe 20, sisi tulikuwa wanne tu, tukawashinda. Ilikuwa ni sawa na mwanafunzi ambaye hajaelewa hata swali halafu anajitapa eti mtihani ulikuwa rahisi sana.
Bahati, sisi wengine tulikuwa na access ya inside plans za Barrick. Kwanza Barrick waliweka strategy ya kwanza kwamba hata iweje, hawataki wapate hasara.
Kwenye hilo wakakubaliana kuwa bila ya kujali final outcome itakuwa nini, lazima mazungumzo yavutwe mpaka ufike mwaka mmoja. Kwa sababu wakati makinikia yao yanazuiliwa walikuwa wametoka kufanya underground development ya Gokona kule North Mara iliyokuwa imewagharimu dola milioni 80. Kwa kuvuta mazungumzo yaende kwa mwaka mzima, na wao wakiendelea na uchimbaji, katika kipindi hicho pesa yao hiyo dola 80m itakuwa imerudi.
Strategy ya pili ilikuwa baada ya kurudisha hiyo dola 80m, wana uwezo wa kuonesha kiburi, na kama Serikali itawafukuza, watakwenda kwenye arbitration, na kwa vile wana uhakika wa kushinda, chochote watakacholipwa itakuwa ni faida.
Mwanzoni walikubaliana kuwa wapole kwa sababu kama wangeonesha kiburi, Serikali ikawafukuza, japo wangeshinda mahakamani, lakini Serikali ya JMT, huenda ingechukua muda mrefu kuwalipa kile ambacho kingekuwa kimeamriwa na mahakama ya usuluhishi. Na wao hawakutaka pesa yao isiwe mikononi mwao.
Baada ya mwaka mmoja wakawa wamepata dola 120m. Baada ya hapo wakawa na kiburi. Na Serikali ikawa kwenye weak position. Barrick aka-dictate mkataba. Ndiyo maana ule mkataba unawapa faida zaidi Barrick, na unahakikisha yale waliyofanyiwa mwanzo na Serikali, hayatokei tena.
Katika timu ile ya watu 20, kila mmoja alikuwa na jukumu lake. Na ilikuwa ni timu ya super intelligents. Lakini akina Kabudi wakiwa wanne wakajiona wao ni miamba.
Niliwahi kuisikiliza speech ya President wa Barrick. Yeye anasema Barrick tangu ianzishwe haijawahi kutengeneza hasara hata mwaka mmoja. Na hiyo imewezekana kutokana na aina ya watu wake. Na akamaliza kwa kusema, "every best person must work with Barrick"