Kaburi la Petro(Simoni bar-yona) lipo Jerusalem na siyo Roma

Kaburi la Petro(Simoni bar-yona) lipo Jerusalem na siyo Roma

Kwa zaidi ya maika 2000 watu wamekuwa wakiaminishwa kuwa Mtume Petro aliuwawa Roma na kuzikwa huko kwenye eneo lililojulikana kama tropaion. Tena imekuwa ikifundishwa na Kanisa Katoliki kuwa Petro ndiye alikuwa Papa wa kwanza lakini ukweli ni kwamba katika maisha yake yote Petro hakuwahi kabisa kuwa Papa achilia mbali kufika tu ROMA. Maisha yake yote Petro au Kefa kama wengine wanavyomwita hakuwahi kabisa kukanyaga ardhi ya Roma.

Mwaka 1958 huko Jerusalemu katika eneo lijulikanalo kama "Dominus Flevit" kwenye mlima wa Mizeituni ambapo kwa sasa hivi pamejengwa kanisa linaloitwa Franciscan Monastery yalichimbuliwa mabaki ya mifupa yaliyokuwa ndani ya boksi(ossuaries)na juu ya boksi hili kulikuwa na maandishi yaliyoandikwa kwa lugha ya Aramaic yakisomeka "Simon Bar Jona". Eneo ilipopatikana mifupa hiyo pia ilipatikana mifupa ya watu wengine ikiwa imehifadhiwa ndani ya maboksi hayo na juu yake yakiwa yameandikwa majina yao. Majina hayo ni pamoja na Mariam, Martha na Lazaro. Inaaminika kuwa Wakristo wa Mwanzo kabisa baada ya kupaa kwa MESSIAH kwenda mbinguni, walichagua kuzikana eneo hilo la Mlima wa Mizeituni, kwasababu imeandikwa kwenye Biblia kuwa siku MESSIAH atakaporudi tena duniani atasimama juu ya Mlima huo, soma ZEKARIA 14:3-4. Kutokana na imani waliyokuwa nayo, Wakristo hao waliamini kuwa itakuwa vema kama watazikwa eneo hilo ili siku ile BWANA YESU atakapokuja na kuwafufua, wawe wa kwanza kumlaki BWANA kwenye Mlima huo wa Mizeituni.

Franciscan "Terra Santa" Monastery, Jerusalem, mahali ambapo mifupa ya Petro ilipopatikana.
View attachment 669269
Mifupa hiyo inayoaminika kuwa ni ya Petro, ilichimbuliwa na Archeologist wa Kiitaliano ambaye alikuwa ni Priest wa Kikatoliki akijulikana kama P.B. Bagatti. Baada ya kuichimbua mifupa hii na kujiridhisha yeye na wenzake aliokuwa nao, Bagatti alikwenda Vatican na kumjulisha Papa wa wakati ule aliyekuwa akiitwa Pius XII. Papa Pius XII alopoambiwa habari hizo na kuoneshwa ushahidi wote, alijibu tu kwa kusema; “inawezekana ikawa kweli hiyo ni mifupa ya PETRO, na inabidi tufanye marekebisho makubwa, lakini kwa sasa hivi kaeni kimya kabisa”. Bagatti akamuuliza Papa Pius XII, Je, unaamini itakuwa ni mabaki ya Petro? Papa Pius XII akamjibu kwa kusema; “kwa ushahidi ulionionesha, naamini itakuwa ni mifupa ya Petro”.

Cha ajabu ni kwamba mpaka Papa Pius XII anafariki dunia Octoba 9, 1958 hakuweka hadharani kabisa uvumbuzi huo uliofanywa na Archeologist Bagatti. Mwaka huo huo Bagatti ndipo akaamua kuandika kitabu akielezea kupatikana kwa mifupa ya Petro huko Jerusalem, kitabu hicho kinachoitwa, "Gli Scavi del Dominus Flevit", kilichochapishwa mwaka 1958. Kitabu hichi kiliandikwa na P. B. Bagatti akishirikiana na Archeologist mwenzake J. T. Milik, ambao wote walikuwa pia ni Ma-Priest wa Kanisa Katoliki. Bagatti anaonekana kuficha baadhi ya mambo na haelezei kwa undani hasa nini kilifanyika. Hii inadhihirisha wazi kabisa kuwa walifungwa mdomo na Kanisa Katoliki ili wasiweke kila kitu hadharani kwani kama wangefanya hivyo ingekuwa ni sawa na kulivua nguo kanisa, kwani kwa miaka yote kanisa Katoliki limekuwa likifundisha kuwa Petro aliishi Roma kwa miaka 24 na kuuawa na kuzikwa huko.
View attachment 669271
View attachment 669272
Maneno hayo hapo juu yanasomeka "Simoni Bar Yona"​

Ushahidi mwingine unaoonesha wazi kabisa kuwa Petro hakuwahi kabisa kufika Roma, ni Biblia. Mtume Paulo katika Waraka zake zote hakuna mahali ameandika kuwa Petro alikwenda Roma na kuishi huko. Paulo alikuwa ni mtu anayependa sana kuandika kila kitu anachokutana nacho. Isingewezekana kabisa Petro ahamie Roma na kuishi huko kwa miaka 24 halafu Paulo asiandike, achilia mbali Petro mwenyewe asiandike kabisa Waraka wowote ule akielezea maisha yake akiwa Roma. Haiingii akilini hata kidogo mtu kama Petro eti akaishi mahali kwa miaka 24 akihubiri Injili, halafu jambo hilo lisiwemo kabisa ndani ya Biblia.

Isitoshe ukisoma Biblia utaona Paulo anaelezea wazi kabisa kuwa Petro alikuwa ni Mtume kwa ajili ya Wayahudi, soma WAGALATIA 2:7-8. Pia tukisoma Biblia tunaona BWANA anamtokea Anania kwenye maono na kumwambia aende akaonane na Sauli(Paulo), sababu yeye BWANA amemchagua SAULI(PAULO)kuwa Mtume wa Mataifa, soma MATENDO YA MITUME 9:10-15. Pia ukisoma Waraka wote wa Petro hakuna mahali popote Petro ameandika kuwa yupo Roma.

Kutokana na yote hayo na ushahidi wa mifupa iliyopatikana Jerusalem, ni kielelezo tosha kuwa Roman Catholic Church wanafundisha “uwongo” na wanafanya kila wawezalo kuuficha UKWELI. Kanisa hili limejaa mafundisho ya uwongo na kwa miaka mingi sana limewapotosha watu wengi sana. Kanisa hili lina intelijesia kali sana kiasi kwamba wanaweza kuficha habari yoyote ile isiwafikie watu, lakini kamwe hawawezi kushindana na MUNGU hasa pale anapoamua UKWELI lazima ujulikane.

Tokea mwaka 1958 ilipogundulika mifupa hii ya PETRO huko Jerusalem, Kanisa Katoliki limekuwa likificha uvumbuzi huu kwa kila namna. Eneo ambapo ilipatikana mifupa hii linamilikiwa na Kanisa hilo hivyo imekuwa rahisi wao kuuficha ukweli lakini pia ndani ya kanisa wapo baadhi ya Ma-Priest ambao huwa hawawezi kukaa kimya na wamekuwa wakivujisha siri hizi.
Kwa hiyo umeanza kuyaamini maandiko ya wakatoliki? Kwa nini usiiulize biblia pekee? Kwamba wakatoliki walitengeneza uongo kisha mapadri wakikatoliki wakafungwa midomo wasiseme halafu MTU haruhusiwi kulitembelea eneo ambalo pia lina monastery ya wakatoloki hata Baggati hakuvisema kwenye kitabu chao ila umeamini!!!! Unatishaaaa!!!!!

Paulo anasemaje kuhusu wale mitume wengine? Ameeleza kule walikotembelea na walikofia? Oooh! Nimekumbuka kila mmoja wao alikuwa anaandika nyaraka za kila alikoenda, alikofia hata alivyokufa.

Atakayebisha kwenye hizi fact zako lazima atakuwa na matatizo ya akili ama ni mkatoloki mdhambi.

Hongera mkuu, endelea kuwapa nondo hawa wamataifa.
 
Tatizo hapa tutaishia kubishana na watu wanaotaka kujua historia kupitia Biblia pekee utafikiri kile ni kitabu cha historia. Kanisa Katoliki ni tajiri kimafundisho sababu imetunza nyaraka, barua na mafundisho ya mababa wa Kanisa hadi sasa. Zipo barua zimetunzwa karne nyingi zinazosimulia kuanzia uinjilishaji wa Petro na Paul huko Roma hadi vifo vyao. Mlisikia barua kama ile iliyotolewa na baraza la maaskofu kuelekea uchaguzi wa 2010. Ile barua itaishi vizazi na vizazi na wapo wataopinga kuwa barua hizo ni feki nyakati hizo! Kama unataka kujua kweli safari ya Petro huko Roma ingia kwenye site ya Catholic Answers utapata shule nzuri tu.
Hizo barua zote mimi nazifahamu na wala hazina UKWELI wowote ule. Barua hizo ni za kutungwa tu baadhi ya watu. Mtu aliyeutengeneza UWONGO ni rahisi sana kwake kutengeneza UWONGO mwingine ili apate majibu ya kuwapatia watu wanaojaribu kuhoji. Kanisa Katoliki limetengeneza barua nyingi sana ambazo zote ni za uwongo. Barua zote hizi ama WARAKA hazipo ndani ya BIBLIA kabisa.

Mfano mzuri ni barua liliyoandikwa na Gaius kati ya mwaka 170 na 180. Barua hizi siyo za kweli hata kidogo. Maandiko mengine yanayohifadhiwa na Kanisa hilo ni kama The Apocryphal Acts of Peter. Kama maandiko haya yangekuwa Genuine yangejumuishwa kwenye Biblia. Nasema hivyo sababu wote tunajua kuwa vitabu vilivyojumuishwa kwenye Biblia vilijumuishwa kwa MWONGOZO wa ROHO MTAKATIFU. Kila andiko lililoachwa nje ya Biblia halikuwa sahihi kwa mafundisho ya KIKRISTO. MUNGU anatenda kazi sana na kuna watu wanafikiri ni rahisi tu kushindana naye. Kanisa katoliki linamilikiwa na Ibilisi na anafikiri atamshinda MUNGU, lakini kamwe hawezi kumshinda MUNGU.
 
Nyie wasabat kila kukicha ni kupingana na waroma na sio kupingana na mwovu shetani.
Nenda ukale makande kwa mama lishe hapo karibu nitakuja kulipa.
Sabato njema!!!!!
Hilo kanisa takatifu la mitume ndio wakala namba moja wa lucifa
 
Kwa hiyo umeanza kuyaamini maandiko ya wakatoliki? Kwa nini usiiulize biblia pekee? Kwamba wakatoliki walitengeneza uongo kisha mapadri wakikatoliki wakafungwa midomo wasiseme halafu MTU haruhusiwi kulitembelea eneo ambalo pia lina monastery ya wakatoloki hata Baggati hakuvisema kwenye kitabu chao ila umeamini!!!! Unatishaaaa!!!!!

Paulo anasemaje kuhusu wale mitume wengine? Ameeleza kule walikotembelea na walikofia? Oooh! Nimekumbuka kila mmoja wao alikuwa anaandika nyaraka za kila alikoenda, alikofia hata alivyokufa.

Atakayebisha kwenye hizi fact zako lazima atakuwa na matatizo ya akili ama ni mkatoloki mdhambi.

Hongera mkuu, endelea kuwapa nondo hawa wamataifa.
Kwa taarifa yako hata mimi nilikuwa MKATOLIKI na baada yakufundishwa UWONGO, niliamua kuitafuta KWELI. Nilipoijua KWELI nikaona nisikae kimya wacha niwajulishe na wengine ili na wao waijue KWELI. Huwezi kuujua uchafu wa nyumba kama uko nje ya nyumba na hujawahi kuingia ndani.

Kwa taarifa yako Bagatti alihojiwa na akakiri kila kitu ingawa hakuandika kwenye kitabu chake. Kuna watu waliongea na akina Bagatti na wakaamua kwenda Jerusalemu kuutafuta UKWELI na wakauona kwa macho yao. Sasa wewe endelea kuogelea kwenye UWONGO wa Kanisa Katoliki. Hata baadhi ya Mapre wa Kanisa Katoliki wapo Jerusalemu na wanakuambia ni kweli Petro alifia Jerusalemu na kuzikwa huko. Lakini kamwe hawewezi kusimama hadharani na kuongea hivi vitu.
 
Inashangaza kwakweli,unawatuhumu wakatoliki kuwa wanafundisha uongo lkn mafundisho unayoyaamini wewe kuwa Petro hakuzikwa Vatican yanatoka kwa haohao wakatoliki
Siku zote uchafu wa ndani ya nyumba huelezwa na watoto walio ndani ya nyumba hiyo. Mtu wa nje huwezi kujua siri za ndani usipoambiwa na watu wa ndani na kuoneshwa ushahidi. Ushahidi upo na waliotaka kujiridhisha walikwenda mpaka Jerusalemu miaka hiyo na wakajionea wenyewe.
 
Hongereni wasabato Kwa kutengeneza uinfo ufananao na ukweli. Toka missionary Wa alielelewa kwA maadui ya kikatoliki akajipinga mwenyewe itakuwa adabu ya karne. Hongereni wasabato Kwa kuutangaza ukatoliki baadala ya kuutangaza wenyewe.
Sisi hatuna vita na Wakatoliki, sisi tunapigana vita na IBILISI ambaye ndiye baba ya Wakatoliki, IBILISI ndiye baba ya UWONGO. Lengo letu ni watu waijue KWELI.

Mimi siyo MSABATO, mimi ni MKRISTO wa kweli ninayeishi kwa AMRI za MUNGU na IMANI ya YESU KRISTO.
 
Asante sana mkuu kwa kuongeza ufahamu mkubwa ndani yangu!!! Kuna prof Mmoja aliwahi kusema adui wa ukristo ni Roman Catholic, hawana muda na kuuishi ukristo bali mapokeo yao ambayo ni kivuli cha maovu
Acha kuaminishwa ujinga na mjinga anaesukumwa na chuki,
Kaandika anachojua yy,sisi tyo ndani ya ukatoliki tumezaliwa tukifundishwa kuwa Petro alikusibiwa na kufa Israeli na siyo Italy
Lkn mifupa yake ilichimbuliwa na kuzikwa upya kanisa la st peter km ambavyo makanisa mbali mbali hutabarukiwa na kuzikiwa masalia ya watakatifu mbali mbali toka sehemu tifauti
 
Kwa taarifa yako hata mimi nilikuwa MKATOLIKI na baada yakufundishwa UWONGO, niliamua kuitafuta KWELI. Nilipoijua KWELI nikaona nisikae kimya wacha niwajulishe na wengine ili na wao waijue KWELI. Huwezi kuujua uchafu wa nyumba kama uko nje ya nyumba na hujawahi kuingia ndani.

Kwa taarifa yako Bagatti alihojiwa na akakiri kila kitu ingawa hakuandika kwenye kitabu chake. Kuna watu waliongea na akina Bagatti na wakaamua kwenda Jerusalemu kuutafuta UKWELI na wakauona kwa macho yao. Sasa wewe endelea kuogelea kwenye UWONGO wa Kanisa Katoliki. Hata baadhi ya Mapre wa Kanisa Katoliki wapo Jerusalemu na wanakuambia ni kweli Petro alifia Jerusalemu na kuzikwa huko. Lakini kamwe hawewezi kusimama hadharani na kuongea hivi vitu.
Unasoma kitu kingine na unaandika kitu contrary! Kama kulikuwa na haja ya kujibu basi ungejikita kwenye yaloulizwa.

Sijagusia imani yako ya sasa wala ya zamani. Pole!!!!!
 
Mkuu hili Kanisa Katoliki linafundisha uwongo sana. Hakuna ushahidi wowote hata wa kihistoria tu unao onesha kuwa Mtume Petro aliwahi kuishi Roma. Hakika kabisa Kanisa hili ni adui namba moja wa UKRISTO duniani.
Nioneshe mafundisho ya kanisa yanayosema hicho mnachopinga,
Mnaanzisha maneno na kisha mnayapinga ninyi afu mnasema wakatoliki,
Lete ushahidi wa hicho unachosema kanisa linadanganya,
 
Siku zote uchafu wa ndani ya nyumba huelezwa na watoto walio ndani ya nyumba hiyo. Mtu wa nje huwezi kujua siri za ndani usipoambiwa na watu wa ndani na kuoneshwa ushahidi. Ushahidi upo na waliotaka kujiridhisha walikwenda mpaka Jerusalemu miaka hiyo na wakajionea wenyewe.
Walijionea nini, mwili wa Petro ama Monastery? Na ni kina nani hao kama ukiwataja kwa majina itapendeza zaidi
 
Sisi hatuna vita na Wakatoliki, sisi tunapigana vita na IBILISI ambaye ndiye baba ya Wakatoliki, IBILISI ndiye baba ya UWONGO. Lengo letu ni watu waijue KWELI.

Mimi siyo MSABATO, mimi ni MKRISTO wa kweli ninayeishi kwa AMRI za MUNGU na IMANI ya YESU KRISTO.
Wewe na Nani hao mnaopgana na baba wa wakatoliki?
 
Hizo barua zote mimi nazifahamu na wala hazina UKWELI wowote ule. Barua hizo ni za kutungwa tu baadhi ya watu. Mtu aliyeutengeneza UWONGO ni rahisi sana kwake kutengeneza UWONGO mwingine ili apate majibu ya kuwapatia watu wanaojaribu kuhoji. Kanisa Katoliki limetengeneza barua nyingi sana ambazo zote ni za uwongo. Barua zote hizi ama WARAKA hazipo ndani ya BIBLIA kabisa.

Mfano mzuri ni barua liliyoandikwa na Gaius kati ya mwaka 170 na 180. Barua hizi siyo za kweli hata kidogo. Maandiko mengine yanayohifadhiwa na Kanisa hilo ni kama The Apocryphal Acts of Peter. Kama maandiko haya yangekuwa Genuine yangejumuishwa kwenye Biblia. Nasema hivyo sababu wote tunajua kuwa vitabu vilivyojumuishwa kwenye Biblia vilijumuishwa kwa MWONGOZO wa ROHO MTAKATIFU. Kila andiko lililoachwa nje ya Biblia halikuwa sahihi kwa mafundisho ya KIKRISTO. MUNGU anatenda kazi sana na kuna watu wanafikiri ni rahisi tu kushindana naye. Kanisa katoliki linamilikiwa na Ibilisi na anafikiri atamshinda MUNGU, lakini kamwe hawezi kumshinda MUNGU.
Roho mtakatifu aliwaongoza akina nani walioviweka vitabu hivyo
Usiparuke hapa,
Ni akina nani hao ambao ROHO MTAKATIFU aliwaongoza ktk kuvichambua vitabu maana wakatoliki ni waongo na Roho hakai kati ya waongo
 
Suala la Kafa wapi au kazikwa wapi kwa sasa sio issue. Inshu ni je una uwezo wa kukutana na Yesu pndi arudipo mara ya pili kama huyo Petro?
 
Kwa taarifa yako hata mimi nilikuwa MKATOLIKI na baada yakufundishwa UWONGO, niliamua kuitafuta KWELI. Nilipoijua KWELI nikaona nisikae kimya wacha niwajulishe na wengine ili na wao waijue KWELI. Huwezi kuujua uchafu wa nyumba kama uko nje ya nyumba na hujawahi kuingia ndani.

Kwa taarifa yako Bagatti alihojiwa na akakiri kila kitu ingawa hakuandika kwenye kitabu chake. Kuna watu waliongea na akina Bagatti na wakaamua kwenda Jerusalemu kuutafuta UKWELI na wakauona kwa macho yao. Sasa wewe endelea kuogelea kwenye UWONGO wa Kanisa Katoliki. Hata baadhi ya Mapre wa Kanisa Katoliki wapo Jerusalemu na wanakuambia ni kweli Petro alifia Jerusalemu na kuzikwa huko. Lakini kamwe hawewezi kusimama hadharani na kuongea hivi vitu.
Ulikuwa mkatoliki makapi ndo maana alivutwa na mafundisho ya watabiri walioshindwa wa mwisho wa dunia,na wale waliotaka kwenda ulaya kwa amani bila tiketi za ndege wala viza kuhubiri
 
Sisi hatuna vita na Wakatoliki, sisi tunapigana vita na IBILISI ambaye ndiye baba ya Wakatoliki, IBILISI ndiye baba ya UWONGO. Lengo letu ni watu waijue KWELI.

Mimi siyo MSABATO, mimi ni MKRISTO wa kweli ninayeishi kwa AMRI za MUNGU na IMANI ya YESU KRISTO.
Ninaanza kukuamini! Lakini kabla sijaamini kabisa naomba uniambie dhehebu lako, najua watu wa Mungu huwa hawadanganyi kisha nitaomba tubadilishane uelewa kidogo.
 
Back
Top Bottom