Mimi sina dhehebu mkuu. Imeandikwa hivi; "Basi maana yangu ni hii, ya kwamba kila mtu wa kwenu husema, mimi ni wa Paulo, na mimi ni wa Apolo, na mimi ni wa Kefa, na mimi ni wa Kristo. Je! Kristo amegawanyika? Je! Paulo alisulubiwa kwa ajili yenu? Au Je! Mlibatizwa kwa jina la Paulo?" 1 WAKORINTHO 1:12-13
Wewe ukisema ni wa dhehebu fulani, Je! ulibatizwa kwa jina la dhehebu lako?? Nafikiri utakuwa umenielewa mkuu. Mimi sina dhehebu, mimi namwamini KRISTO na kuishi kwa kuzishika AMRI za MUNGU. Siyo kama sina dhambi au siyo kama sikosei, nakosea sana lakini, kwa IMANI nitaishi na kwa NEEMA za MUNGU wetu ninasamehewa makosa yangu.