Kaburi la Petro(Simoni bar-yona) lipo Jerusalem na siyo Roma

Kwa hiyo umeanza kuyaamini maandiko ya wakatoliki? Kwa nini usiiulize biblia pekee? Kwamba wakatoliki walitengeneza uongo kisha mapadri wakikatoliki wakafungwa midomo wasiseme halafu MTU haruhusiwi kulitembelea eneo ambalo pia lina monastery ya wakatoloki hata Baggati hakuvisema kwenye kitabu chao ila umeamini!!!! Unatishaaaa!!!!!

Paulo anasemaje kuhusu wale mitume wengine? Ameeleza kule walikotembelea na walikofia? Oooh! Nimekumbuka kila mmoja wao alikuwa anaandika nyaraka za kila alikoenda, alikofia hata alivyokufa.

Atakayebisha kwenye hizi fact zako lazima atakuwa na matatizo ya akili ama ni mkatoloki mdhambi.

Hongera mkuu, endelea kuwapa nondo hawa wamataifa.
 
Hizo barua zote mimi nazifahamu na wala hazina UKWELI wowote ule. Barua hizo ni za kutungwa tu baadhi ya watu. Mtu aliyeutengeneza UWONGO ni rahisi sana kwake kutengeneza UWONGO mwingine ili apate majibu ya kuwapatia watu wanaojaribu kuhoji. Kanisa Katoliki limetengeneza barua nyingi sana ambazo zote ni za uwongo. Barua zote hizi ama WARAKA hazipo ndani ya BIBLIA kabisa.

Mfano mzuri ni barua liliyoandikwa na Gaius kati ya mwaka 170 na 180. Barua hizi siyo za kweli hata kidogo. Maandiko mengine yanayohifadhiwa na Kanisa hilo ni kama The Apocryphal Acts of Peter. Kama maandiko haya yangekuwa Genuine yangejumuishwa kwenye Biblia. Nasema hivyo sababu wote tunajua kuwa vitabu vilivyojumuishwa kwenye Biblia vilijumuishwa kwa MWONGOZO wa ROHO MTAKATIFU. Kila andiko lililoachwa nje ya Biblia halikuwa sahihi kwa mafundisho ya KIKRISTO. MUNGU anatenda kazi sana na kuna watu wanafikiri ni rahisi tu kushindana naye. Kanisa katoliki linamilikiwa na Ibilisi na anafikiri atamshinda MUNGU, lakini kamwe hawezi kumshinda MUNGU.
 
Nyie wasabat kila kukicha ni kupingana na waroma na sio kupingana na mwovu shetani.
Nenda ukale makande kwa mama lishe hapo karibu nitakuja kulipa.
Sabato njema!!!!!
Hilo kanisa takatifu la mitume ndio wakala namba moja wa lucifa
 
Kwa taarifa yako hata mimi nilikuwa MKATOLIKI na baada yakufundishwa UWONGO, niliamua kuitafuta KWELI. Nilipoijua KWELI nikaona nisikae kimya wacha niwajulishe na wengine ili na wao waijue KWELI. Huwezi kuujua uchafu wa nyumba kama uko nje ya nyumba na hujawahi kuingia ndani.

Kwa taarifa yako Bagatti alihojiwa na akakiri kila kitu ingawa hakuandika kwenye kitabu chake. Kuna watu waliongea na akina Bagatti na wakaamua kwenda Jerusalemu kuutafuta UKWELI na wakauona kwa macho yao. Sasa wewe endelea kuogelea kwenye UWONGO wa Kanisa Katoliki. Hata baadhi ya Mapre wa Kanisa Katoliki wapo Jerusalemu na wanakuambia ni kweli Petro alifia Jerusalemu na kuzikwa huko. Lakini kamwe hawewezi kusimama hadharani na kuongea hivi vitu.
 
Inashangaza kwakweli,unawatuhumu wakatoliki kuwa wanafundisha uongo lkn mafundisho unayoyaamini wewe kuwa Petro hakuzikwa Vatican yanatoka kwa haohao wakatoliki
Siku zote uchafu wa ndani ya nyumba huelezwa na watoto walio ndani ya nyumba hiyo. Mtu wa nje huwezi kujua siri za ndani usipoambiwa na watu wa ndani na kuoneshwa ushahidi. Ushahidi upo na waliotaka kujiridhisha walikwenda mpaka Jerusalemu miaka hiyo na wakajionea wenyewe.
 
Hongereni wasabato Kwa kutengeneza uinfo ufananao na ukweli. Toka missionary Wa alielelewa kwA maadui ya kikatoliki akajipinga mwenyewe itakuwa adabu ya karne. Hongereni wasabato Kwa kuutangaza ukatoliki baadala ya kuutangaza wenyewe.
Sisi hatuna vita na Wakatoliki, sisi tunapigana vita na IBILISI ambaye ndiye baba ya Wakatoliki, IBILISI ndiye baba ya UWONGO. Lengo letu ni watu waijue KWELI.

Mimi siyo MSABATO, mimi ni MKRISTO wa kweli ninayeishi kwa AMRI za MUNGU na IMANI ya YESU KRISTO.
 
Asante sana mkuu kwa kuongeza ufahamu mkubwa ndani yangu!!! Kuna prof Mmoja aliwahi kusema adui wa ukristo ni Roman Catholic, hawana muda na kuuishi ukristo bali mapokeo yao ambayo ni kivuli cha maovu
Acha kuaminishwa ujinga na mjinga anaesukumwa na chuki,
Kaandika anachojua yy,sisi tyo ndani ya ukatoliki tumezaliwa tukifundishwa kuwa Petro alikusibiwa na kufa Israeli na siyo Italy
Lkn mifupa yake ilichimbuliwa na kuzikwa upya kanisa la st peter km ambavyo makanisa mbali mbali hutabarukiwa na kuzikiwa masalia ya watakatifu mbali mbali toka sehemu tifauti
 
Unasoma kitu kingine na unaandika kitu contrary! Kama kulikuwa na haja ya kujibu basi ungejikita kwenye yaloulizwa.

Sijagusia imani yako ya sasa wala ya zamani. Pole!!!!!
 
Mkuu hili Kanisa Katoliki linafundisha uwongo sana. Hakuna ushahidi wowote hata wa kihistoria tu unao onesha kuwa Mtume Petro aliwahi kuishi Roma. Hakika kabisa Kanisa hili ni adui namba moja wa UKRISTO duniani.
Nioneshe mafundisho ya kanisa yanayosema hicho mnachopinga,
Mnaanzisha maneno na kisha mnayapinga ninyi afu mnasema wakatoliki,
Lete ushahidi wa hicho unachosema kanisa linadanganya,
 
Walijionea nini, mwili wa Petro ama Monastery? Na ni kina nani hao kama ukiwataja kwa majina itapendeza zaidi
 
Wewe na Nani hao mnaopgana na baba wa wakatoliki?
 
Roho mtakatifu aliwaongoza akina nani walioviweka vitabu hivyo
Usiparuke hapa,
Ni akina nani hao ambao ROHO MTAKATIFU aliwaongoza ktk kuvichambua vitabu maana wakatoliki ni waongo na Roho hakai kati ya waongo
 
Suala la Kafa wapi au kazikwa wapi kwa sasa sio issue. Inshu ni je una uwezo wa kukutana na Yesu pndi arudipo mara ya pili kama huyo Petro?
 
Ulikuwa mkatoliki makapi ndo maana alivutwa na mafundisho ya watabiri walioshindwa wa mwisho wa dunia,na wale waliotaka kwenda ulaya kwa amani bila tiketi za ndege wala viza kuhubiri
 
Ninaanza kukuamini! Lakini kabla sijaamini kabisa naomba uniambie dhehebu lako, najua watu wa Mungu huwa hawadanganyi kisha nitaomba tubadilishane uelewa kidogo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…