Kacha za kimasai za bendera ya Kenya zinavaliwa kuliko za Tanzania. Hii ni kukosa uzalendo au?

WaTz hawana vinasaba vya kujipamba au urembo. Na kwa asili ya uonevu usio na mashiko, unaweza kujikuta uko chini ya ulinzi kwa kuitumia bendera ya taifa vibaya.
 
Ila kwa rangi ya Cultures za Kenya na SA zimechangamka.... ya Tanzania imepoa sana
 
Issue hapa ni rangi tu. Rangi nyekundu kiasili inavutia zaidi watu, hivyo watu wengi wanajikuta wakivaa za kenya kwa kuvutiwa na aina za rangi tu. Binafsi nilishawahi kuwa muhanga wa kuvaa kacha yenye bendera ya kenya na kuna mkenya mmoja alikuwa anafurahi kweli kweli kila akiniona nimevaa kacha hiyo.
 
Tuache unafiki rangi zao na zile logo zilizopita kwenye bendera zao zinavutia ... Sisi mbunifu wa bendera yetu alichemka
 
Umeniwahi laazizi walaqhi ningekutag,

Been asking myself the same question, nimepita Makumbusho muda mfupi uliopita nikashangaa kadada ka kichina kamevaa visendo vya kimasai vimenakshiwa na bendera ya Tanzania, nikajiuliza hivyo wageni wanakuwa proud na nchi yetu kuliko sisi wenyewe.?

Natamani kujua hao nchi jirani are they proud kuvaa vitu vyenye bendera yetu kama sisi tunavyojiona wajanja kuvaa vitu vyenye bendera zao..??
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…