Kacha za kimasai za bendera ya Kenya zinavaliwa kuliko za Tanzania. Hii ni kukosa uzalendo au?

Kacha za kimasai za bendera ya Kenya zinavaliwa kuliko za Tanzania. Hii ni kukosa uzalendo au?

Huku mtaani vijana wengi saana na wa kike na wa kiume naona wavaa sana kacha za Kenya na UG kuliko za TZ.

Ni huku kwetu pekee au hadi mtaani kwenu, nini maana yake? Rangi za KE na UG zinapendeza kuliko za TZ?

Wamekosa uzalendo au?

Hebu tupe ushuhuda mtaani kwako wapo ikiwezekana weka na kapicha au ni umbea wangu tu wa kuchunguza yasiyonihusu

View attachment 1651615
View attachment 1651605
View attachment 1651614
View attachment 1652306
Rangi za TZ zimekaa kichafuchafu, kiccm
 
Ata Rais wao uhuru akivaaga huwa inampendeza
Tena sana na sio yeye tu hiyo ni kwa yeyote yule anayezivalia. Rais UK huwa hazikosi kiganjani.
_76763326_76761259.jpg
Hadi muda mwingine huwa zinamkanganya na anajipata amezivalia mbili mbili 😀
kenyatta%2B1.jpg
Rangi tamu sana hizi, ambazo zinaleta ari ya uzalendo wa aina yake. Tena kotekote bila presha wala kushurutishwa.
45251047_503.jpg
 
Nilikuwa najiuliza sana sababu ya hili jambo, naliona sana huko twitani, shukrani kwa kulileta.
Kipindi Cha awamu ya nne tulihamasishwa Sana na My.Kikwete kuvaa bendera yetu mahala popotte ili kujifaharisha na kuongeza uzalendo kwantaifa letu na kweli tulipendeza na bendera yeu.Hivi awamu ya tan tulienedelea kuruhusiwa????
 
Kwanini uvae ya kenya na usivae ya nchi
Yako?
Hivi kuna mkenya anavaa hiyo kitu ya tanzania?

Ova
 
za tanzania c zilipigwa marufuku? alafu za kenya zinavutia sana [emoji1139][emoji1139][emoji1139][emoji1139]
 
Watanzania huwa mna mind vitu vya kijinga sana, huku huwa napishana na watu wamevaa t-shirts zimeandikwa Tanzania au Zanzibar na haijawahi kuniuma, mkoloni alitukosea sana miafrika kwa kuchora mipaka yake hiyo, yaani......
Naona umeamua kuja kidiplomasia zaidi jombaa. 😀 Mimi huwa sina huo muda hata wa kuwaza tu, achia mbali kuumwa. Kisa rangi au bendera ya nchi yoyote ile nyingine, sio tukiwa na kitu safi kama hiki.
kenya-flag-std.jpg
 
Ushamba.

Wengine hata hawajui kama ni bendera ya KE. Kuna mtu niliwahi kumuuliza akasema yeye anavaa tu ila hajui ni rangi za wapi.

Kingine, watz wanaishobokea sana KE ilhali KE despises TZ. MTZ atasifia chochote kile cha KE hata kama ni kibaya vp na kuponda cha bongo wakati KE pamoja na ukabila wao hawezi sifia chochote kile cha bongo hata kama kizuri vp.

Mbongo anafurahi zaidi kufika Nairobi kuliko kufika London.
Mkuu Nairobi ni pazuri. Hivi utalinganisha Nairobi ni miji yetu ya kimachinga kweli? Kila mahali ni uchafu na kunanuka?
 
Back
Top Bottom