Kada CCM: Hatuwezi kukubali Makamu wa Rais Kukashifiwa na Kuvunjiwa Heshima. Simai futa kauli zako

Kada CCM: Hatuwezi kukubali Makamu wa Rais Kukashifiwa na Kuvunjiwa Heshima. Simai futa kauli zako

Vonzelewsk

Member
Joined
Sep 20, 2018
Posts
93
Reaction score
283
Kama heading inavyojieleza makada waanza kujitokeza kumjibu simai aliyoyaongea kuhusu YUDA ndani panawaka moto yetu macho wachatuone mwisho wao.

=====

"Waziri wa utalii kule Zanzibar na hoja zake za kutatanisha kwamba kwanini alijiuzulu uwaziri kule anakuja kumkashifu na kumvunjia heshima Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

"Sisi kama makada wa Chama Cha Mapinduzi hatuwezi kukubali. Sisi kama vijana tunaotetea heshima za viongozi wetu hatuwezi kukubali mtu wa namna hii. Yeye kama yuko kwenye magenge ya urais, akae huko.

"Dkt. Samia na serikali yake wana miaka mitatu mpaka kufikia 2030, miaka minne penginepo, mpaka kufikia 2030. Analeta ugenge genge wa Urais kwa kuchafulia hadhi ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania?

Pia soma Mbunge Simai: Kuna Yuda Msaliti ndani ya Serikali hili anatafuta huruma kanisani

"Hata kama kuwe kuna kitu gani ndani ya chama chetu, kuwe kuna matatizo gani ndani ya chama chetu, chama chetu kina instruments za kutosha za kutatua matatizo ya viongozi. Rais wa nchi yetu ana kamati kuu ya Chama Cha Mapinduzi, ana baraza la wazee viongozi wastaafu, wapo. Kama kuna lolote lipo, rais hana tabia ya kuangaika eti amtafute mtu kama yule Simae aende akabuatuke pale bungeni.

"Nawaambia sasa watanzania mufahamu, kuna watu wanajibebisha ndani ya chama chetu na kujifanya eti wanamtetea Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania lakini kiuhalisia nawaambie ndugu zangu, hawana dhamira hiyo. Ni kujipendekeza wakidhani huenda watapewa uwaziri.

"Tunakuomba Simae, ufute kauli zako zote ulizozisema na tunakuambia ulimlenga Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Kama hukumulenga Makamu wa Rais, tunakuomba kesho uape, uchukue msahafu wewe muislamu useme, 'Mimi niliongea sikumlenga Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.' Tuone kama utaweza. Tuone kama utaweza. Usituletee masihara.

"Sisi ni wafia chama hiki, hatuwezi kukubali mtu mmoja na kundi lake penginepo wanapika migogoro ndani ya chama chetu kionekane chama chetu kimegawanyika mwanemwane. Leo mnampa maneno mpaka Godbless Lema anasema eti, 'Kifaranga kikipandishwa juu ujue mama yake yuko pembeni.' Mama ni nani? Anamaanisha Rais wa nchi yetu anaweza akamtuma Simae? Anaweza akamtuma Simae? Rais wa nchi yetu ana shida gani? Amiri Jeshi Mkuu, wa majeshi ya ulinzi na usalama. Mwanamama aliyevunja rekodi; Makamu wa Rais wa kwanza ni yeye, Rais wa kwanza ni yeye, Amiri Jeshi Mkuu wa majeshi ya ulinzi na usalama ni yeye. Ana shida gani mpaka amtume huyo jamaa anaitwa Simae?

"Watanzania muwe makini. Sio kila mnaemuona eti anajinasibu na Chama Cha Mapinduzi kwamba eti ni mtu mwenye akili. Tuwe makini, kidumu Chama Cha Mapinduzi." - Cde Kazungu Bakari Kazungu



"
 
20260603_130332.jpg
 
Hatutoki kwenye reli huko CCM hakuna msafi hata Nchimbi huyo hana usafi wowote , CCM ni ile ile.

Sisi tunataka haki ya waliouwawa October 29 tu si vinginevyo na tunapopataka katiba mpya wafungwe wahusika na vidampa wao.
Sahihi sana kwa hiki ulichosema, nashangaa hadi wapinzani wanataka kuingia kwenye mtego wa kumuona Nchimbi ni tofauti na wanaccm wengine. Ni hivi, hakuna mwanaccm yoyote wa kumtetea kwa sasa. Tusipokuwa makini tutauziwa mbuzi kwenye gunia.
 
Nilitegemea wamjibu yule mzanzibari, atleast wamejitahidi kulinda heshima zao kidogo walizonazo.

Watu wasiachwe wajenge tabia ya kuropoka hovyo kama walevi.
Wazanzibari siku hizi wameshajiona wanaweza hata kuwanyea Watanganyika vichwani au vinywani bila soni wala hofu kabisa.Tuendelee hivyohivyo yawezekana ni mipango mizuri ya Mungu kutuelekeza nchi ya ahadi baada ya ufalme kufitinika.
 
Ujumbe wa mh Simai ulikuwa mahususi kwa ajili ya Tundu lissu na si imma the boy
 
Samia amewatumia Sana masheikh na waislamu kumtetea bila kujua anaacha athari ndani ya jamii .....hiyo bado haitoshi amekuja kutumia mbinu ileile ya kijinga Kwa huyu mbunge wake
Wanawake ni shida Sana yupo tayari kutumia mabilioni ya pesa ilimradi aone MTU Fulani anachambwa

Huyu Maza ni wale wanamama wa mwananyamala na kinondoni Moscow
 
Sahihi sana kwa hiki ulichosema, nashangaa hadi wapinzani wanataka kuingia kwenye mtego wa kumuona Nchimbi ni tofauti na wanaccm wengine. Ni hivi, hakuna mwanaccm yoyote wa kumtetea kwa sasa. Tusipokuwa makini tutauziwa mbuzi kwenye gunia.
Mkuu mimi nimeshangaa hadi Lema anaingia mtego huu kumuongelea Nchimbi kuwa anashambuliwa.

Nchimbi ana usafi gani kujitoa na ya October 29?

Katika utengenezaji , usambazaji , kudhibiti ubora wa dawa kuna kitu kinaitwa "product recall"

Ukisikia dawa fulani inaondolewa sokoni sababu haifai kwa matumizi hawaondoi dawa zote bali "batch" husika.

Maana yake batch ya dawa fulani imetumia master formula kutengeneza dawa zote za batch ile kuanzia API, excipients, personnel ,SOP etc.

Hivyo Nchimbi anaangukia katika batch hii ya wauaji hivyo hana usafi ndio maana mimi simtambui Samuya kama rais sababu kaijipa kwa mchakato haramu kadhalika na Nchimbi simtambui kama makamu wa rais sababu kumtambua mmoja utahalalisha wengine njia pekee ya Nchimbi ilikua ni kugomea kuapa kuwa makamu wa rais kwa kupitia damu za watu

Mimi mtego huu siuingii.
 
Wazanzibari siku hizi wameshajiona wanaweza hata kuwanyea Watanganyika vichwani au vinywani bila soni wala hofu kabisa.Tuendelee hivyohivyo yawezekana ni mipango mizuri ya Mungu kutuelekeza nchi ya ahadi baada ya ufalme kufitinika.
Nchimbi ni mtanganyika kama mimi, japo yeye ni CCM mimi Chadema.

Kuja kugombezwa na mgeni ndani ya nyumba yako ni dharau isiyotakiwa kuvumiliwa hata sekunde moja.
 
Haya Ma CCM hata yakigombana vipi ila yakishaenda pale Dodoma, huwa yanaelewana au niseme huwa yanachimbwa beat yanakausha yanabaki kuumia moyoni, na kuunga juhudi za wababe wa chama!

Ni vizuri tukiendelea kuyaacha yapasuane!
 
Back
Top Bottom