Tatizo la Law School si dogo ambalo ati kila Tom, Dick au Harry anaweza kuwa na ufumbuzi au ushauri.
Kwa sampuli hii:
1. Profesa Cyriacus Binamungu (Mzumbe): anasema kuna shida kwa walimu katika taasisi hiyo (LST).
“Wanafunzi wanaandaliwa vizuri (vyuoni) isipokuwa kutakuwa na shida LST, walimu hawazingatii ufundishaji, wanafikiria mishahara, akipokea hajali mwanafunzi kaelewa au la.”
2. Profesa Costa Mahalu, (VC Saut): anasema ni aibu kwa taasisi hiyo kutokana na matokeo hayo, pia inapaswa ijitafakari.
“Haiwezekani wanaofeli mtihani wa uwakili pale LST hawana ujuzi na maarifa katika masomo yao kutoka vyuo walivyosoma. Hapana! Kuna tatizo na lazima utafutwe ufumbuzi,”
Profesa Mahalu anasema matokeo mabaya yanasababishwa na makundi matatu ya walimu wanaowafundisha wanafunzi hao wa uwakili.
(a) Matatizo ya uwezo,
(b) wanaopenda kuogopwa na wanafunzi,
(c) wale wasiotaka mafanikio ya wengine, ambalo ndiyo lililo hatari zaidi.
“Hata hapa Saut niliwakuta walimu wa aina hiyo. Tumefanya kazi kubwa kumaliza tatizo hilo,”
Profesa Mahalu anashauri kulindwa msingi wa kuanzishwa kwa LST ambao ni kutoa elimu kwa vitendo kutoka kwa majaji, mahakimu na mawakili wanaoshughulika na mashauri kila siku mahakamani.
“Maprofesa waliobobea katika nadharia wasipelekwe kuwafundisha wanafunzi pale LST kwa sababu kufanya hivyo ni kukiuka lengo la msingi la kuanzishwa kwa chuo hicho.”
Kabla ya taasisi hiyo, anasema Mahalu mawakili walipata maarifa kwa miezi tisa kutoka kwa mawakili na mahakimu waliopo kazini.
“Taifa lilipata wanasheria na mawakili nguli, nikiwemo mimi, Jaji mkuu mstaafu, Othman Chande na Waziri Mkuu mstaafu Mizengo Pinda mwaka 1974. Wahadhiri wa LST wajitafakari kwa matokeo haya.”
___________
Watu kama hawa walipaswa kuwamo kwenye tume ya Dr. Ndumbaro.
LST kuna matatizo na walimu yasiyokuwa ya kufumbiwa macho. Fika LST kuutambua ukwasi wa walimu hawa wenye kujiita 'fulani the don.'
Kwa hakika muda wa kuyatanzua makando kando yao ni sasa.
Wameyakoroga wenyewe, hawana budi kuyanywa.
Source:
Profesa Shivji asema tatizo ni mfumo ufaulu mtihani Uanasheria