Kadhia ya Law School "Wasomi Nguli" wasikilizwe

Kadhia ya Law School "Wasomi Nguli" wasikilizwe

Sas hyu huyu professor mahalu s amewai kuwa na kashfa ya kuongeza gharama za ofisi ya ubalozi wa Italy ..na kesi kapamban nayo Hadi kuchomokaa ila kusema kweli kuwa wa kili kwa sas Ni dili kubwa mno

Kuna jamaaa namfahamu. Kipindi nasoma olevel yeye alikuwa Aleve fom 5 akiwa six mm Niko fom 5 ,sas baada ya muda chapu kamaliza nakisha kwenda mzumbe namm nikiwa najianda kwenda chuo Cha ija Cha korogwe tanga baadae nikagome kwenda chuo hicho ila mzeee wangu alikuwa na hamu sas mm kuwa wakili au hakimu


Lahaula baada yamiaka Kama mitano nikakutana na yule jamaaa katk eneo fln huko Arusha ambako tulikuwa TUnaenda kucheki kiwanja jamaa dalali akasema jirani yenu huu Ni wakili .bas kdg tu jamaa alitoka na gari ndipo dalali akatumbia kuwa jamaa si yule pale kumbee ndio huyo jmaaa nilisoma nae shule moja sas Ni wakili mkubwa sna huko Arusha anamiliki ma apartment za maana huko Arusha maeneo ya moivaro ..

Uwakili Ni dili Sana na Kaz za dhuluma mno

Mkuu kumbuka kuna baina ya kuwa na tuhuma na tuhuma kuthibitishwa.

Ndiyo maana haijawahi kuacha kuitishwa heshima kwa uamuzi wa mahakama.
 
Huko vyuoni huwa ni chabo tu zinatembea.wakifika huko law school wanabanwa,hatimae pumba na mchele vinajitenga.
Me nashauri law school wakaze buti zaidi . mbona wahasibu kila mwaka wanafeli maelfu kwa maelfu na hakuna anaelialia kwenye media?

Kwa hiyo una shauri course zote wapitie law school kuliko na mitambo ya kutenganisha pumba na mchele mkuu?
 
Kwa ujumla UDSM ni chuo cha kidikteta na udikteta huu unasababishwa na ukabila uliokithiri.

Kuna kabila hapo UDSM huwa hawafeli hata kama ni kialaza.

Kingine ngono. Kuna digrii nyingi za mabinti ni za ngono.

Unakuta binti anabakizwa kuwa tutorial asistant na GPA kubwa ila kichwani boga. Anabebwabebwa tu..

Hebu kila chuo kinachofundizha sheria kiwe na law school hapohapo chuoni.
Wee mburula tunajadili LST na siyo UDSM!
 
Profesa Cyriacus Binamungu (Mzumbe): anasema kuna shida kwa walimu katika taasisi hiyo (LST).

Nguli wa sheria katika chio cha elimu ya juu Prof Cyriacus Binamungu akiwa anatoa lecture

10 June 2022
Third FoL Paper Presentation Series


Dear campus community The Dean, Faculty of Law has the pleasure to invite you all to the Third FoL Paper Presentation Series which will take place today (Friday) 10 June 2022 at the Fanon Lecture Theatre (LT 1) - Main Campus from 1400hrs. The presenters and their corresponding topics are as follows: Presenter 1: Prof Cyriacus Binamungu Topic: 50 Years of the Law of Marriage Act in Tanzania: Examination of Developments and Legal Challenges Presenter 2: Dr. Mwajuma Kadilu Topic: Education and Sustainable Development Goals: Legal Challenges and Prospects for Tanzanian Teenage Mothers

Source: Exaud Paul
 
Kingine ngono. Kuna digrii nyingi za mabinti ni za ngono.

Unakuta binti anabakizwa kuwa tutorial asistant na GPA kubwa ila kichwani boga. Anabebwabebwa tu..
Acha kudhalilisha wanawake. Tukio lq mtu mmoja ama watu 2,3 usilifanye kuwa kanuni ya wanawake wote
 
Kama utaupuuza ukweli kwamba wanafunzi ndiyo wenye shida basi mleta mada una wivu ama chuki binafsi na walimu wa shule ya sheria.

Wanafunzi wanachangia kufeli kwao kwa 75+%. Muda mwingi wanadanga, wanalewa, wanabet, wanawaza ukahaba, n.k.

Hawawezi kuandika sentensi nzuri za kiswahili na hata kiingereza. Unapata wapi ujasiri wa kuwalaumu walimu pekee?
Hivi mtu kasoma hadi kapata degree ya chuo kikuu halafu ndio kaenda law school, aanze kudanga na kustarehe hapo ngwe ya mwisho kabisa ya elimu???!!!! Wanafunzi wa kudanga na starehe huwa hawafikii mbali na GPA zao huwa haziwaruhusu kukanyaga hiyo law school
 
Kingine ngono. Kuna digrii nyingi za mabinti ni za ngono.

Unakuta binti anabakizwa kuwa tutorial asistant na GPA kubwa ila kichwani boga. Anabebwabebwa tu..
Sasa hizo qualifications zilizomfanya awe accepted hapo chuoni amezipata kwa ngono hata ufaulu wake mukautilia mashaka? Pili ina maana hiyo GPA kubwa imepatikana kwa kufaulu course moja au mbili tu?

Someni bwana muache vya bwerere vya mitihani ya kununua haitawafikisha popote.
 
Prof. Josephat Celestine Muhoza - Romans and the Law, Love of wisdom, so what is wisdom ?


What is knowledge? does it benefit you and the community . Philosophy gives you direction.
University degree is supposed to make you universal not local...

The importance of values and beliefs
Education must have a purpose and ground. Education should liberate us. Education for service. Education is not for dominance .... Education without philosophy is like a car without steering wheel or radar ...

Source : African Intellectuals.
 
Kama utaupuuza ukweli kwamba wanafunzi ndiyo wenye shida basi mleta mada una wivu ama chuki binafsi na walimu wa shule ya sheria.

Wanafunzi wanachangia kufeli kwao kwa 75+%. Muda mwingi wanadanga, wanalewa, wanabet, wanawaza ukahaba, n.k.

Hawawezi kuandika sentensi nzuri za kiswahili na hata kiingereza. Unapata wapi ujasiri wa kuwalaumu walimu pekee?
Toa ujingaaa
 
Wanasheria wapumbavu sana sana, Dkt Neema wa SAUT mwanza kachana kila kitu mitaala ya vyuo haikidhi mahitaji ya law school, na pia hao walimu academicians wasihusike kufundisha law school , misingi ya law school ni kufundishwa na practitioners Judges, Magistrates na practicing Advocates. Hao maprofesa wa UDSM na wajinga wengine wasijimilikishe hio Law School of Tanzania.

Watu wanajitafunia watoto warembo wa Sheria kiulaini, na Rushwa ya pesa kumbe nyakati za walimu miungu watu Bado zipo na zinaendelea, so disappointing.

Wanafunzi wajinga sana, narudia tena tumieni vizuri simu janja kila unapohisi kuna changamoto Kwa mhusika au mhusika ni tatizo, record maongezi nyosha sentences record audio, go with hidden cameras ,

Hadi wanasheria wanafanyiwa huo upumbavu Kwa miaka yote hio. Tusiwaonee huruma hawa ni vilaza unawezaje kusomea Sheria halafu uwe na akili za ukilaza kulea matatizo, hio ni dalili kweli madent wa Law School ni vilaza.
 
Tatizo la Law School ni mchanganyiko wa factors nyingi zinazoingiliana. Si busara kuchukua sababu moja au mbili tu na kuhitimisha zipo sababu za kimfumo, mitaala ya LST na vyuo vikuu kutoendana, sababu za kijamii ikiwemo rushwa za ngono na nyinginezo, mfumo wa elimu duni kwa ujumla nchini, uwezo wa walimu, ubabe wa kielimu(superiority & negative mindset) kwa walimu na manyanyaso, sababu za kiuchumi, uhaba wa vitendea kazi kwa elimu ya vitendo, mkazo wa nadharia na kutoa nafasi kidogo mafunzo ya vitendo, maandalizi hafifu ya wanafunzi kwenye vipindi na psychological feeling kuwa chuo hicho ni vigumu kufaulu hii ni kwa walimu na wanafunzi ndicho kinachozunguka akilini lazima wafelishwe. Teaching methodology and approach haimwandai mwanafunzi kufanya mitihani na kufaulu na masuala ya kiutawala yakiwemo LST kusajiri wote wanaoomba kibiashara zaidi bila kufanya mchujo stahiki na upembuzi wa kutosha kuchukua wenye uwezo tu badala ya kuzingatia fedha pekee, mzigo mzito wa masomo kwa muda mfupi, lugha ya kiingereza km mode of communication ni changamoto kwa wanafunzi wetu. etc
 
Mzumbe University
Morogoro, Tanzania

Hapa tunaona 'Passion' hakuna kabisa kwa wanafunzi, wataweza vipi ku 'move' jaji au ku argue na senior counsel au principal state attorney?

26 February 2022
THIS WAS THE MOOT TRIAL HELD AT MZUMBE UNIVERSITY.

BETWEEN JORDAN UNIVERSITY COLLEGE AND MZUMBE UNIVERSITY. THIS WAS DONE BY THE LAW STUDENTS



Source : kwa hisani kubwa ya : TUJUZANE MEDIA
 
Kama utaupuuza ukweli kwamba wanafunzi ndiyo wenye shida basi mleta mada una wivu ama chuki binafsi na walimu wa shule ya sheria.

Wanafunzi wanachangia kufeli kwao kwa 75+%. Muda mwingi wanadanga, wanalewa, wanabet, wanawaza ukahaba, n.k.

Hawawezi kuandika sentensi nzuri za kiswahili na hata kiingereza. Unapata wapi ujasiri wa kuwalaumu walimu pekee?
Huu ujinga mnaobeba vichwani mwenu sijui mlipandikizwa na nani.

Hao maprofesa wanaofundisha vyuo wanavyotoka hao wanafunzi wametoa maoni yao, ajabu nyie mnaendelea kutembea na sababu zenu za kukariri kutoka kwa wajinga wenzenu.

Sijui hiyo research ya kutambua hao wanafunzi ni makahaba, hawasomi, nk mliifanya lini na wapi, na hamjui huu ujinga wenu wa kuropoka kwa kufuata mikumbo unawachafulia sifa zao hao maprofesa waliowafundisha hao wanafunzi kule walipotoka.

Kukosa kwenu maarifa, mnawafanya nao waonekane hawajui, kwenu wanaojua ni hao walimu wa LST peke yao wanaoongoza kwa kufelisha wanafunzi wengi kama vile wao walisomea sayari ya Mars.
 
Mahalu atakuwa anaitaka nafasi ya kuteuliwa kuwa mkuu wa shule ya sheria kama haoni nafasi kubwa ya wanafunzi kuchangia kufeli kwao.
Ni porojo tu zimekujaa kichwani, mwenye mawazo tofauti anaitaka nafasi, kumbe hizo nafasi mnaziona keki ndio maana mnawaumiza wanafunzi kwa kujiona miungu watu.
 
UDSM inakujaje hapa mkuu? Kumbuka LST inachukua wanafunzi wa vyuo vikuu vyote wenye sifa.

Angalizo: Dr. Tulia Ackson, Dr. Asha Rose Migiro kukutajia wachache wameanza kamq Tutorial Assistants faculty of Law UDSM.

NInakazia wengine kina sisi si vibaya kujikita kwenye u Simba na Yanga.
Nimecheka uliponitajia huyo Dr..... hahahaha hahaaaaaaaaaaaa subwoofer.
 
Tatizo la Law School si dogo ambalo ati kila Tom, Dick au Harry anaweza kuwa na ufumbuzi au ushauri.

Kwa sampuli hii:

1. Profesa Cyriacus Binamungu (Mzumbe): anasema kuna shida kwa walimu katika taasisi hiyo (LST).

“Wanafunzi wanaandaliwa vizuri (vyuoni) isipokuwa kutakuwa na shida LST, walimu hawazingatii ufundishaji, wanafikiria mishahara, akipokea hajali mwanafunzi kaelewa au la.”

2. Profesa Costa Mahalu, (VC Saut): anasema ni aibu kwa taasisi hiyo kutokana na matokeo hayo, pia inapaswa ijitafakari.

“Haiwezekani wanaofeli mtihani wa uwakili pale LST hawana ujuzi na maarifa katika masomo yao kutoka vyuo walivyosoma. Hapana! Kuna tatizo na lazima utafutwe ufumbuzi,”

Profesa Mahalu anasema matokeo mabaya yanasababishwa na makundi matatu ya walimu wanaowafundisha wanafunzi hao wa uwakili.

(a) Matatizo ya uwezo,
(b) wanaopenda kuogopwa na wanafunzi,
(c) wale wasiotaka mafanikio ya wengine, ambalo ndiyo lililo hatari zaidi.

“Hata hapa Saut niliwakuta walimu wa aina hiyo. Tumefanya kazi kubwa kumaliza tatizo hilo,”

Profesa Mahalu anashauri kulindwa msingi wa kuanzishwa kwa LST ambao ni kutoa elimu kwa vitendo kutoka kwa majaji, mahakimu na mawakili wanaoshughulika na mashauri kila siku mahakamani.

“Maprofesa waliobobea katika nadharia wasipelekwe kuwafundisha wanafunzi pale LST kwa sababu kufanya hivyo ni kukiuka lengo la msingi la kuanzishwa kwa chuo hicho.”

Kabla ya taasisi hiyo, anasema Mahalu mawakili walipata maarifa kwa miezi tisa kutoka kwa mawakili na mahakimu waliopo kazini.

“Taifa lilipata wanasheria na mawakili nguli, nikiwemo mimi, Jaji mkuu mstaafu, Othman Chande na Waziri Mkuu mstaafu Mizengo Pinda mwaka 1974. Wahadhiri wa LST wajitafakari kwa matokeo haya.”
___________

Watu kama hawa walipaswa kuwamo kwenye tume ya Dr. Ndumbaro.

LST kuna matatizo na walimu yasiyokuwa ya kufumbiwa macho. Fika LST kuutambua ukwasi walimu hawa wenye kujiita 'fulani the don.'

"Pana watu wenye kumudu hata magari 10 ya kifahari mno ya kutembelea tu."

Kwa hakika muda wa kuyatanzua makando kando yao ni sasa.

Wameyakoroga wenyewe, hawana budi kuyanywa.

Source:

Profesa Shivji asema tatizo ni mfumo ufaulu mtihani Uanasheria
For how long has this problem persisted?
2. Only this year has such mass failure?
3. If #2 is yes, why?
4. Does LST recruited all new instructors this year? If the problem is all about instructors.
 
Back
Top Bottom