YA MOHAMMED FAKHI NA KUMBUKUMBU MBOVU ZA VIONGOZI WA SIMBA SC.
Na Nasri Van Man Utd.
Simba wanalalamika kuhusu Muhammed Fakhi kuchezeshwa akiwa na kadi tatu za njano kwenye mechi yao na Kagera sugar . Wanalalamika kuwa hakupasa kucheza kutokana na si sheria mchezaji kucheza akiwa anakadi tatu za njano .. kiufupi tu simba wanataka wapewe point tatu ..
Ila waswahili wanasema ukiwa muongo ukumbuke kuhifadhi na maneno . Tujikumbushe na hii. Msimu wa mwaka juzi simba walipopata kashfa kama hii ya kumchezesha Ajibu akiwa na kadi tatu za njano .. Je TFF waliliongeleaje na walitoa maamuzi gani .?
Tujikumbushe ilikua ni March. 5 2015 ..
Majuzi, Ofisa mkuu wa kitengo cha habari wa klabu ya Yanga SC, Jerry Muro aliweka wazi kuwa Simba imefanya makosa kumchezesha kumchezesha mshambulizi Ibrahimu Ajibu katika mchezo dhidi ya Tanzania Prisons kwa kuwa mchezaji huyo tayari alikuwa na kadi tatu za njano na kwa mujibu wa kanuni zilizo wazi, mchezaji anapopata kadi tatu za njano atakosa mchezo mmoja hivyo Ajibu hakustahili kutumika katika mchezo huo ambao Simba ilishinda mabao 5-0, magoli matatu ‘ Hat-trick’ yakifungwa na mshambulizi huyo kinda.
TFF ilijibu haraka kuwa, kanuni tayari zilikuwa zimeshafiwa marekebisho huku baadadhi ya klabu tu zilipata barua kuhusu marekebisho hayo mapya yaliyofanywa na Bodi ya Ligi. Kanuni za sasa ni nzuri, kwa kuwa zitaruhusu klabu kumchagulia mechi ya ‘ kumiss’ mchezaji ambaye atakuwa na kadi tatu. Simba ni kati ya klabu zilizopata barua ya marekebisho hayo na tayari walishaitumia dhidi ya Abdi Banda wiki mbili zilizopita wakati kiungo mwenye kadi tatu za njano Abdi Banda alipotumika katika mchezo huo ambao Simba walipoteza kwa bao 1-0 katika uwanja wa Kambarage, Shinyanga.
Inawezekana Yanga wasiwe na ‘ hitaji la pointi za Simba kupunguzwa’ lakini kama timu ambayo inaweza kutumia kanuni hiyo Yanga wana hoja ya msingi kwa kuwa hawana taarifa hadi sasa. Bodi ya Ligi tayari wamekiri kuwa Yanga wana hoja ya msingi, kuhoji ni kwanini hawajapata taarifa rasmi ya mabadiliko hayo tangu Januari 8. Lakini katika hilo Bodi inaweza isihusike sana kwa kuwa walitoa maagizo hayo mapema kwa Shirikisho la soka, TFF..
Najiuliza kuwa simba wanacholalamika ni nini wakati sheria ya namna hii kupitia wao TFF waliwahi kuwatetea kuwa imeshabadilishwa..!
Inawezekanaje sheria iliyokufa ije ihukumu tena .. simba wanapasa kukumbuka kwanza hili .
Mi nadhani kwa sasa simba Inatakiwa kupambana ili kupata ubingwa sio kuleta hoja ambazo hazina msingi..