Kadi tatu za njano alizopata Fakhi mchezaji wa Kagera sugar hizi hapa

Kadi tatu za njano alizopata Fakhi mchezaji wa Kagera sugar hizi hapa

Wamechemsha kweli maana kutoka Dec hadi Apr kagera imecheza mechi nne tu?
 
mechi moja ni fa na mbili za ligi kuu mpaka hapo rufaa imefeli
 
Watu mnashindwa kutafuta matokeo uwanjani, mnataka kupata matokeo baada ya mechi.
 
Wa bongo bwana kwani yanga si mlikata rufaa kuhusu mchezaji yule aliyetoka stendi na kuwafunga goli au mumesahau simba ndio kwa nini washindwe kukata rufaa au hawana haki hiyo? Kama ni haki itendeke haki na siyo timu moja ndio isikate rufaa kisa eti walifungwa
 
KADI TATU ZA NJANO ALIZOPATA FAKHI MCHEZAJI WA KAGERA SUGAR

1. Mchezo namba 122 uliopigwa Sokoine tarehe 17 December dhidi ya Mbeya City.

2. Mchezo namba 165 uwanja wa Kaitaba mchezo dhidi ya African Lyon . Ulipigwa tarehe 18 January.

3. Mchezo namba 190 uwanja wa Kaitaba tarehe 4 March , mechi dhidi ya Majimaji.

Mechi hizi ndizo ambazo zimewafanya Simba SC kuikatia rufaa Kagera Sugar kwa kumchezesha mlinzi wao Mohamedi Fakhi katika mechi ya April 2, 2017 Kaitaba ambapo Simba alifungwa goli 2-1.

Kama madai haya yatakuwa kweli kwa ushahidi wa mechi hizo tatu , ina maana Simba watapewa alama tatu za mchezo huo waliopoteza.
Kama ni kweli itakuwa kama ilivyokuwa kwa Simba mchezaji anachagua mechi ya kukosa hivyo hachezi mechi ijayo SIMBA ilikuwa lazima ife kwanza.
 
KADI TATU ZA NJANO ALIZOPATA FAKHI MCHEZAJI WA KAGERA SUGAR

1. Mchezo namba 122 uliopigwa Sokoine tarehe 17 December dhidi ya Mbeya City.

2. Mchezo namba 165 uwanja wa Kaitaba mchezo dhidi ya African Lyon . Ulipigwa tarehe 18 January.

3. Mchezo namba 190 uwanja wa Kaitaba tarehe 4 March , mechi dhidi ya Majimaji.

Mechi hizi ndizo ambazo zimewafanya Simba SC kuikatia rufaa Kagera Sugar kwa kumchezesha mlinzi wao Mohamedi Fakhi katika mechi ya April 2, 2017 Kaitaba ambapo Simba alifungwa goli 2-1.

Kama madai haya yatakuwa kweli kwa ushahidi wa mechi hizo tatu , ina maana Simba watapewa alama tatu za mchezo huo waliopoteza.
 
IPI ya FA apo mkuu? Hakuna ya FA apo mana FA walicheza na mbao fc
Nakumbuka sisi tulivyolalamika kuhusu Ajib tukaambiwa ni hiari ya mchezaji kuchagua mechi gani asicheze so naomba watani na nyie mtulie Fakhi ataamua mwenyewe mechi ipi asicheze kwa Simba ilikuwa lazma acheze alikuwa anawataka sana keshamaliza ss kazi yke ataamua mechi ipi asicheze!
 
YA MOHAMMED FAKHI NA KUMBUKUMBU MBOVU ZA VIONGOZI WA SIMBA SC.

Na Nasri Van Man Utd.

Simba wanalalamika kuhusu Muhammed Fakhi kuchezeshwa akiwa na kadi tatu za njano kwenye mechi yao na Kagera sugar . Wanalalamika kuwa hakupasa kucheza kutokana na si sheria mchezaji kucheza akiwa anakadi tatu za njano .. kiufupi tu simba wanataka wapewe point tatu ..

Ila waswahili wanasema ukiwa muongo ukumbuke kuhifadhi na maneno . Tujikumbushe na hii. Msimu wa mwaka juzi simba walipopata kashfa kama hii ya kumchezesha Ajibu akiwa na kadi tatu za njano .. Je TFF waliliongeleaje na walitoa maamuzi gani .?

Tujikumbushe ilikua ni March. 5 2015 ..

Majuzi, Ofisa mkuu wa kitengo cha habari wa klabu ya Yanga SC, Jerry Muro aliweka wazi kuwa Simba imefanya makosa kumchezesha kumchezesha mshambulizi Ibrahimu Ajibu katika mchezo dhidi ya Tanzania Prisons kwa kuwa mchezaji huyo tayari alikuwa na kadi tatu za njano na kwa mujibu wa kanuni zilizo wazi, mchezaji anapopata kadi tatu za njano atakosa mchezo mmoja hivyo Ajibu hakustahili kutumika katika mchezo huo ambao Simba ilishinda mabao 5-0, magoli matatu ‘ Hat-trick’ yakifungwa na mshambulizi huyo kinda.



TFF ilijibu haraka kuwa, kanuni tayari zilikuwa zimeshafiwa marekebisho huku baadadhi ya klabu tu zilipata barua kuhusu marekebisho hayo mapya yaliyofanywa na Bodi ya Ligi. Kanuni za sasa ni nzuri, kwa kuwa zitaruhusu klabu kumchagulia mechi ya ‘ kumiss’ mchezaji ambaye atakuwa na kadi tatu. Simba ni kati ya klabu zilizopata barua ya marekebisho hayo na tayari walishaitumia dhidi ya Abdi Banda wiki mbili zilizopita wakati kiungo mwenye kadi tatu za njano Abdi Banda alipotumika katika mchezo huo ambao Simba walipoteza kwa bao 1-0 katika uwanja wa Kambarage, Shinyanga.

Inawezekana Yanga wasiwe na ‘ hitaji la pointi za Simba kupunguzwa’ lakini kama timu ambayo inaweza kutumia kanuni hiyo Yanga wana hoja ya msingi kwa kuwa hawana taarifa hadi sasa. Bodi ya Ligi tayari wamekiri kuwa Yanga wana hoja ya msingi, kuhoji ni kwanini hawajapata taarifa rasmi ya mabadiliko hayo tangu Januari 8. Lakini katika hilo Bodi inaweza isihusike sana kwa kuwa walitoa maagizo hayo mapema kwa Shirikisho la soka, TFF..

Najiuliza kuwa simba wanacholalamika ni nini wakati sheria ya namna hii kupitia wao TFF waliwahi kuwatetea kuwa imeshabadilishwa..!

Inawezekanaje sheria iliyokufa ije ihukumu tena .. simba wanapasa kukumbuka kwanza hili .

Mi nadhani kwa sasa simba Inatakiwa kupambana ili kupata ubingwa sio kuleta hoja ambazo hazina msingi..
 
Ni kweli point 3, wamepewa simba? Tff hawajatenda haki kama kweli,hebu tujuzane Mimi nimekosa raha!
 
Back
Top Bottom