Kadi ya kupanda Mwendokasi ni elf tano (5000)

Kadi ya kupanda Mwendokasi ni elf tano (5000)

Mwendokasi wanatujaza km mizigo, waruhusu Co zingine kama tatu au waongeze mabasi! Lile basi refu linashindilia watu mpaka Mia tatu! Huku wafanyakazi wakitufokea mithili ya watoto wa shule! Aise umasikini mbaya, mwakani nitafosi ist hata kwa kukopa.

Kwanza ni aibu na fedheha kuminyana na wamama watu wazima wengine wana misambwanda!
 
Ukweli ni kwamba huu ni ujinga mkubwa. Kama UDART hawawezi kuweka mabasi ya kutosha waruhusu watu binafsi wenye uwezo. Wao wanaweza kuchukua kodi kiasi fulani hii ni win-win situation kwa abiria na Mwendokasi.
 
vp hiyo kadi haina expry date.? kwa nyomi lile kimara na kivukoni labda wenzetu wameona fursa ya ulaji 5000 kamba ndefu hiyo na huduma zenyewe mwendo wa kobe!
 
Ukweli ni kwamba huu ni ujinga mkubwa. Kama UDART hawawezi kuweka mabasi ya kutosha waruhusu watu binafsi wenye uwezo. Wao wanaweza kuchukua kodi kiasi fulani hii ni win-win situation kwa abiria na Mwendokasi.
eti bongo biashara inakufa na kushindwa kujiendesha kisa imezidiwa na wateja yaani barabara yako,ruti uko peke yako abiria wa kumwaga hadi unawakimbia pesa kama zote alafu ruti ya mbagala na g/mboto daladala kibao wanapata faida hawafeli kupeleka hesabu laki mbili kwa bosi hawa Udart wanafeli wapi kwa nyomi lile hadi wanaleta njaa za tsh5000.!
 
Ukweli ni kwamba huu ni ujinga mkubwa. Kama UDART hawawezi kuweka mabasi ya kutosha waruhusu watu binafsi wenye uwezo. Wao wanaweza kuchukua kodi kiasi fulani hii ni win-win situation kwa abiria na Mwendokasi.
Huenda ndio kampuni ya kwanza kushindwa kujiendesha kwa ufanisi kwa sababu ya kuzidiwa na idadi kubwa ya wateja.

Tatizo la huduma nyingi za umma kuwa mbovu ni kwa sababu ya kuwepo kwa tabaka la wenye nacho na wasio nacho kwenye huduma inayotakiwa kutolewa kwa usawa. Kama wakuu wa mikoa na wilaya na wakuu wa taasisi mbalimbali wangekuwa wanatumia usafiri huo kusingekuwa na upumbavu uliopo. Wale wanachotaka ni kuuza tiketi tu huduma bora si kipaumbele kabisa kwa sababu wanajua hakuna mkuu wa mkoa wala wilaya anayepanda udart ndio maana unakuta basi siti zimepasuka, camera zinaning'inia, basi lina vumbi na halisafishwi, watu wanajazana hadi mlangoni.

Hakuna kiongozi wa serikalini anayejua adha ya usafiri wa udart sababu hawatumii usafiri huo hivyo hawafahamu na ndio maana changamoto ya usafiri hup haipati ufumbuzi.
 
Sidhani kama hii ni sawa jamani

Kwani haiwezekani kutoa Kadi bure? Au hata iwe elf moja kama za pantoni?

Kweli ni busara kuuza Kadi Kwa elf tano?

Hiyo Kadi ina mambo gani ya ziada?

Wahusika waangalie hili jambo Kwa hicho la Imani
Watanzania hawaelewi maana ya sustenability. ILi abiria waweze kutunza kadi lazima wazinunue. Ukifanya kadi bure abiria hawatazitunza. Pia fikiria abiria anaepanda bus maramoja tu na kuitelekeza huoni udat watakuwa wanafanya bishara kichaa.

Kabla ya kulalamika unatakiwa uwe unajiuliza mwenyewe maswali. Fikiria udati kilasiku ina abiria wapya. Tena wanaotoka mikoani ambao wala hawataendelea kutumia hiyo kadi tena. Yani wao wawe na kazi ya kugawa kadi kama njugu. Kwa mamilioni ya watu wa DSM watafilisika tu.

Ukinunua utaitunza
 
Back
Top Bottom