Lookmalasin
JF-Expert Member
- Jan 7, 2017
- 1,723
- 2,358
Hilo ndio tatizo kubwa kwa kila sehemu, kila kiongozi, kila mahali. Ubinafsi.Huenda ndio kampuni ya kwanza kushindwa kujiendesha kwa ufanisi kwa sababu ya kuzidiwa na idadi kubwa ya wateja.
Tatizo la huduma nyingi za umma kuwa mbovu ni kwa sababu ya kuwepo kwa tabaka la wenye nacho na wasio nacho kwenye huduma inayotakiwa kutolewa kwa usawa. Kama wakuu wa mikoa na wilaya na wakuu wa taasisi mbalimbali wangekuwa wanatumia usafiri huo kusingekuwa na upumbavu uliopo. Wale wanachotaka ni kuuza tiketi tu huduma bora si kipaumbele kabisa kwa sababu wanajua hakuna mkuu wa mkoa wala wilaya anayepanda udart ndio maana unakuta basi siti zimepasuka, camera zinaning'inia, basi lina vumbi na halisafishwi, watu wanajazana hadi mlangoni.
Hakuna kiongozi wa serikalini anayejua adha ya usafiri wa udart sababu hawatumii usafiri huo hivyo hawafahamu na ndio maana changamoto ya usafiri hup haipati ufumbuzi.
Hawafikirii ningekuwa natumia huu usafiri, hii huduma ningejisikiaje.