Kiukweli hilo ni tatizo tena ni tatizo kubwa sana maeneo ya mijini. Yaani kama una sifa hizi, basi ujue kadi zitakuafuata tu...
1/Unafanya kazi/biashara mahususi.(Una uhakika fulani wa kipato)
2/Unaishi na watu vizuri (Unajitolea vizuri na kushirikiana vyema katika mambo ya kijamii)
3/Unafahamika na watu mbalimbali.
4/Muungwana (Sio mchoyo au sio mnyimi)
Sasa kuacha ghafla tu kuchangia kadi unazopewa huenda kukakuathiri sana kwenye mahusiano yako ya kijamii (Jamii husika itakutafsiri kama wewe ni mtu mwenye chuki binafsi au uliyeanza kubadilika kimaadili)
USHAURI WANGU.
-Usitoe michango ili nawe uje kuchangiwa (kiukweli kwa sasa hali imebadilika sana, watu hawataki kutoa pesa kabisa)
-Chagua pa kuchangia, sio kila mtu wa kumchangia (Angalia aliye karibu na wewe zaidi, mwenye mzigo wa kukufuatilia kukudai au mwenye uhuhitaji mkubwa).
-Anza kutoa mchango mdogo badala ya kutoa pesa nyingi ili kuonyesha ufahari.