Kadi za michango zimenizidia!!

Kadi za michango zimenizidia!!

Kuna mtu aliwahi kudhurika kwa kutowachangia watu wengine michango ya sherehe ??

hio hela si bora ukawasaidie watu wanaokosa hela ya kugaramia matibabu hospitalini.
Kuna ukweli hapa mkuu,bora kuokoa maisha kuliko kuchangia balimi!
 
Aisee hii kitu sometime inakera sana basi wakati mwingine huwezi kukwepa, mie nnazo sijui kama kumi bado za kuambiwa mdomoni labda mshikaji yuko nje ya mkoa nnaoishi,tafrani tupu
Sana dada,kwa hiyo utachangia zote!?
 
Kiukweli hilo ni tatizo tena ni tatizo kubwa sana maeneo ya mijini. Yaani kama una sifa hizi, basi ujue kadi zitakuafuata tu...
1/Unafanya kazi/biashara mahususi.(Una uhakika fulani wa kipato)
2/Unaishi na watu vizuri (Unajitolea vizuri na kushirikiana vyema katika mambo ya kijamii)
3/Unafahamika na watu mbalimbali.
4/Muungwana (Sio mchoyo au sio mnyimi)

Sasa kuacha ghafla tu kuchangia kadi unazopewa huenda kukakuathiri sana kwenye mahusiano yako ya kijamii (Jamii husika itakutafsiri kama wewe ni mtu mwenye chuki binafsi au uliyeanza kubadilika kimaadili)

USHAURI WANGU.
-Usitoe michango ili nawe uje kuchangiwa (kiukweli kwa sasa hali imebadilika sana, watu hawataki kutoa pesa kabisa)

-Chagua pa kuchangia, sio kila mtu wa kumchangia (Angalia aliye karibu na wewe zaidi, mwenye mzigo wa kukufuatilia kukudai au mwenye uhuhitaji mkubwa).

-Anza kutoa mchango mdogo badala ya kutoa pesa nyingi ili kuonyesha ufahari.
 
Asante mkuu kwa hekima hizi!
 
Dawa ni kutojenga mazoea ya kuhudhuria sherehe za wengine, na mwenyewe kutofanya sherehe yoyote au ukifanya usiwachangishe watu, unajiandaa kila kitu unawaalika kula na kunywa tu, hawatakusumbua tena.
 
Back
Top Bottom