Kadinali wa Ujerumani ashauri mapadri wa Katoliki waruhusiwe kuoa

Miss Zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
4,599
Reaction score
9,532
Kadinali mmoja wa Ujerumani ametoa rai kwa Kanisa Katoliki kuondoa kigezo cha useja kwa mapadri wa Kanisa hilo.

Katika mahojiano na gazeti la Ujerumani la Sueddeutsche Zeitung, askofu mkuu Reinhard Marx amesema mapadri wa Katoliki wangeruhusiwa kuoa ikiwa wanapenda kufanya hivyo.

Pia alitaja kigezo cha useja kuwa hatari lakini alikataa kuhusisha na visa vya unyanyasaji wa kijinsia ambavyo vimetikisa Kanisa Katoliki kote ulimwenguni. Marx amejulikana kwa juhudi zake za kusukuma mageuzi ndani ya Kanisa katoliki.

Dayosisi yake iliyoko kusini mwa Ujerumani ilimulikwa katika ripoti iliyochapishwa mwezi uliopita juu ya unyanyasaji wa miongo kadhaa uliofanywa na mapadri.

Ripoti hiyo ilimtuhumu Papa Benedict XVI na Marx mwenyewe kwa kushindwa kuchukua hatua dhidi ya wahusika wa unyanyasaji.

Matamshi hayo yanatolewa kuelekea mkutano mpya unaolenga kulifanya Kanisa hilo liwe la kisasa ifikapo 2023.

DW
 
Wazo zuri Cardinal. Itapunguza kashfa za watawa kuhusishwa na unyanyasaji wa kingono, michepuko pamoja na mahusiano na wake za watu kwa wale inaowawia vigumu kujizuia.
 
Kadinali mmoja wa Ujerumani ametoa rai kwa Kanisa Katoliki kuondoa kigezo cha useja kwa mapadri wa Kanisa hilo.

Katika mahojiano na gazeti la Ujerumani la Sueddeutsche Zeitung, askofu mkuu Reinhard Marx amesema mapadri wa Katoliki wangeruhusiwa kuoa ikiwa wanapenda kufanya hivyo.

Pia alitaja kigezo cha useja kuwa hatari lakini alikataa kuhusisha na visa vya unyanyasaji wa kijinsia ambavyo vimetikisa Kanisa Katoliki kote ulimwenguni. Marx amejulikana kwa juhudi zake za kusukuma mageuzi ndani ya Kanisa katoliki.

Dayosisi yake iliyoko kusini mwa Ujerumani ilimulikwa katika ripoti iliyochapishwa mwezi uliopita juu ya unyanyasaji wa miongo kadhaa uliofanywa na mapadri.

Ripoti hiyo ilimtuhumu Papa Benedict XVI na Marx mwenyewe kwa kushindwa kuchukua hatua dhidi ya wahusika wa unyanyasaji.

Matamshi hayo yanatolewa kuelekea mkutano mpya unaolenga kulifanya Kanisa hilo liwe la kisasa ifikapo 2023.

DW

Wanajinyima mbususu kwa makusudi kabisa.😱😨 huku pembeni wakiwa na michepuko au kuwanyanyasa ma Nuns nk,
 
Kadinali mmoja wa Ujerumani ametoa rai kwa Kanisa Katoliki kuondoa kigezo cha useja kwa mapadri wa Kanisa hilo.

Katika mahojiano na gazeti la Ujerumani la Sueddeutsche Zeitung, askofu mkuu Reinhard Marx amesema mapadri wa Katoliki wangeruhusiwa kuoa ikiwa wanapenda kufanya hivyo.

Pia alitaja kigezo cha useja kuwa hatari lakini alikataa kuhusisha na visa vya unyanyasaji wa kijinsia ambavyo vimetikisa Kanisa Katoliki kote ulimwenguni. Marx amejulikana kwa juhudi zake za kusukuma mageuzi ndani ya Kanisa katoliki.

Dayosisi yake iliyoko kusini mwa Ujerumani ilimulikwa katika ripoti iliyochapishwa mwezi uliopita juu ya unyanyasaji wa miongo kadhaa uliofanywa na mapadri.

Ripoti hiyo ilimtuhumu Papa Benedict XVI na Marx mwenyewe kwa kushindwa kuchukua hatua dhidi ya wahusika wa unyanyasaji.

Matamshi hayo yanatolewa kuelekea mkutano mpya unaolenga kulifanya Kanisa hilo liwe la kisasa ifikapo 2023.

DW
tatizo hamsomi kitabu vzr, hakuna mahala MUNGU anazuia mtu kuoa mke halali, ndio maana inakuwa vigumu kuthibiti jambo hili kwani ni maumbile yetu aliyotuumba nayo MUNGU.
 
Kwani dhambi ni uzinzi tu na uasherati?

Mbona hata ulevi nayo ni dhambi??

Ila dhambi kubwa ni kutomwamini Yesu Kristo kuwa ndiye Bwana na Mwokozi wa maisha yako

Hata hivyo haya ya ujenzi, uasherati, ufisadi, uchawi, ugomvi, uadui na mambo mengine yanayofanan na hayo yanatajwa kama matendo ya mwili tu ambayo ukiyatenda huwezi kuuridhi Ufalme wa Mungu
 
Back
Top Bottom