Kadiria Kodi kabla ya 31-March, epuka penati isiyo ya lazima ya Biashara au Kampuni yako

Kadiria Kodi kabla ya 31-March, epuka penati isiyo ya lazima ya Biashara au Kampuni yako

klinbritetz

Senior Member
Joined
Sep 23, 2020
Posts
160
Reaction score
125
Habari, Mtanzania mwana JF,
Makadiro ya Kodi ni Kwa kila mlipa kodi.
Huwa yanafanyika muda wowote kuanzia tarehe 1,January hadi tarehe 31,March kila mwaka
Kwa Yeyote atakae chelewa kufanya makadirio, kwa sasa, siku moja baada ya tarehe 31, March kunachaji(penati) ya Tsh 225,000 kwa KILA mwezi ulio pitiliza Namna ya kufanya makadirio:
  • Hufanyikwa kwa njia ya Mtandao kupitia websiteya TRA (tra.go.tz).
  • Kila mlipa Kodo aliye sajiliwa huingi kaktika mfumo na kujikadiria mwenyewe.
Angalizo, ni kwamba: haijalishi kampuni imefanya bisahara ama haikufanya biashara, ni-lazima kufanya makadirio, kinyume na hapo itapata penati. Kwahiyo biashara au kampuni ambayo haitegemei kuingiza chochote kwa maana ya mauzo, bado itajikadiria SIFURI.

Makadirio ni kusema kwamba kampuni ama bishara inategemea kupata faida kiasi gani kwa mwaka wa fedha kwa mwaka husika ( ni kwasababu, hajafika mwisho wa mwaka bado, hivyo hajui kinagaubaga atapata faida kiasi gani)
Ni vema tujue kwamba baada ya kukadiria, mlipa kdoi anaanza kulipa alichokadiria (isipokuwa kwa makadirio ambayo ni SIFURI)
JINSI YA KULIPA MAKADIRIO
  • Kuna uchaguzi wa kulipa kila baada ya mizei mitatu, ingawa sio lazima. Mlipa kodi aweza lipa makadiro yote kwa awamu moja tu, ama awamu mbili, kwa kadiri apendavyo.
  • Control namba hutumika kulipia malipo ya serikali kwa sasa
Ipo tofauti ya MAKADIRIO na RITANI ya mwaka huu wa biashara. (wakati mwingine nitaongelea hilio zaidi, kwani leo nimejikita kusema kuhusu MAKADIRIO)

kwaheri kwa leo,
HAKIKISHA UMEFANYA YAKUPASAYO, HASA KATIKA AUALA ZIMA LAMAKADIRIO; KABLA HAYAJAKUPATA YA KUKUPATA,
PIA NI VEMA UFANYE MAPEMAKUTOKANA NA
1. Changamoto ya Mtandao siku za mwisho
2. Kumekuwa na mabadiliko karibini TRA(e-filing) kwahiyo kunachangamoto za kureseti password kwa walipa kodi wengi
Mungu atubariki Tanzania, Mungu atubariki Afrika, Mungu atubariki Mataifa Yote
 
Vipi kuhusu vitambulisho vya wajasiliamali bado vinatambulika na TRA au
 
Shukrani sana. Vipi kwa kampuni iliyosajiliwa Brela na bado haijapata Tin wana kuanza biashara hii nayo inahusika kwenye ukadiriaji?
 
NJE YA MADA LAKINI NDANI YA TRA:
Hivi mkuu ni utaratibu gani unaotumika sikuhizi mtu kujiandalia TIN online? maana naona mfumo wa awali haufanyi kazi!
 
NJE YA MADA LAKINI NDANI YA TRA:
Hivi mkuu ni utaratibu gani unaotumika sikuhizi mtu kujiandalia TIN online? maana naona mfumo wa awali haufanyi kazi!
Wamebadilisha kidogo ila still inafanya kazi nimeitumia mwezi ulopita ilikua sawa. ngoja nikutafutie link
 
Shukrani sana. Vipi kwa kampuni iliyosajiliwa Brela na bado haijapata Tin wana kuanza biashara hii nayo inahusika kwenye ukadiriaji?
KAMPUNI ikisajiliwa tu, inasoma TRA, moja kwa moja (mfumo wa sasa) hivyo unapewa takribani miezi 3, uwe umeprinti TIN na umefanya makadirio. Kutofanya hivyo penati inaaanza 225,000 kila mwezi
 
Nitafutie nitashukuru sana mkuu naisubiria hiyo link
link ni ya TRA kuomba TIN
hakikisha una namba yako ya NIDA
pia uwe na nmba ya simu, anuani ya makazi


1679900668795.png



1679900830282.png
 
Back
Top Bottom