Kadogosa: Kuna njama zinafanywa Kuhujumu treni ya SGR na hazijaanza Leo na tumeshawabaini Wanaotuhujumu!

Kadogosa: Kuna njama zinafanywa Kuhujumu treni ya SGR na hazijaanza Leo na tumeshawabaini Wanaotuhujumu!

Kufuatia changamoto za hapa na pale zinazoipata TREN ya SGR boss wa TRC Masanja Kadogosa amesema Kuna njama zinafanywa Kuhujumu mradi huo

Njama hizi hazijaanza Leo ni za muda mrefu na tayari wameshawabaini miongoni mwa wanaowahujumu na watawashughulikia ipasavyo

Source Mwananchi

Mlale unono 😃
Hakuna wengine zaidi ya wamiliki wa mabasi yaendayo hizo sehemu ambazo SGR inaenda.....adhabu pekee kwao ni kuwafirisi tu na kuwaua baaaaasi kwani wanahujumu uchumi na maendeleo ya nchi.
 
Kama tumeshindwa kusimamia vilivyopo tunakazi gani
Ikulu ni issue nyingine ndugu. Tatizo letu nadhani linasababishwa na mambo mengi kama vile uvivu, tamaa (hasa za kutaka maendeleo ya harakaharaka), kupenda vitu (mambo) makubwa kuliko uwezo wetu, wizi, uongo, utapeli, kupuuzia mambo (kutojali) na mengineyo
 
Unakuta mhujumu ni MTU mkubwa ndani ya chama tawala na mchangiaji mkuu wa Hali na Mali wa shughuli za chama, na ana ukwasi unaowazidi akina Kadogosa 19!

Nje ya mada, jina halisi la Abood ni Nani?
 
Kufuatia changamoto za hapa na pale zinazoipata TREN ya SGR boss wa TRC Masanja Kadogosa amesema Kuna njama zinafanywa Kuhujumu mradi huo

Njama hizi hazijaanza Leo ni za muda mrefu na tayari wameshawabaini miongoni mwa wanaowahujumu na watawashughulikia ipasavyo

Source Mwananchi

Mlale unono 😃
Tatizo kubwa ni viongozi wa CCM machawa wenye kusifia na hawana akili za uongozi

Pili maisha wa waTanzania ni ya kimasikini mno na hakuna elimu inatolewa uenye kuwaelewesha nini maana ya mradi au kitu fulani kwao.

Watu wako mtaani 7/24 kusaka maisha na ndio maana Lori la mafuta likianguka utakuta watu kibao mama baba mtoto na madumu ya kuteka mafuta!!!

Usishangae nako huku wanajipanga kuibianabiria na kunyofoa mavyuma itapoangukia au kukwama!!
 
Yule Kadogosa ni mjinga kabisa, na ameshahisi anakwenda kufukuzwa, wote tunajua na tunaona uwezo duni wa watumishi wa umma kuweza kuendesha miradi. Mchawi mkuu wa TRC ni TRC wenyewe wakishirikiana na CCM na kwa hakika SGR itakufa kama inavyokufa mwendokasi.
Shida yaweza isiwe Kadogosa, shida ni serikali na CCM nzima. Ina maana hii nchi kila mkurugenzi wa shirika huwa ni kichaa?

Si ni hawahawa wana akili nzuri tu kwenye familia, kanisani/msikitini/kilingeni, mtaani, shuleni walikuwa sawa, vyuoni walikuwa vizuri sana, wengine walichaguliwa kusoma nje, wengine walikuwa na careers nzuri mashirika ya kimataifa?

Sasa inakuwaje ghafla wakiwa wakurugenzi wa TANESCO, TRC, TTCL, Posta, Bandari wanakuwa wehu/mbumbumbu/wendawazimu/vilaza. Na wakibadilishwa wanakuja wengine nao ni wehu na waliotoka nao wehu.

Kwa mfano kama wanaohujumu reli ni 'mjumbe' mwenye asili ya Kiasia pale Morogoro na ana cheo bungeni na ana urafiki na awamu ya nne. Mhujumu mwingine labda ni baba 'Esther' na anakaa baraza kuu. Mwingine ni haohao wezi na wapo connected na serikali kuu na marafiki zao. Huyo Kadogosa mwenyewe kawekwa na wao ni nani awazidi nguvu. Siasa zinaingilia maslahi ya kitaifa.
 
Kufuatia changamoto za hapa na pale zinazoipata TREN ya SGR boss wa TRC Masanja Kadogosa amesema Kuna njama zinafanywa Kuhujumu mradi huo

Njama hizi hazijaanza Leo ni za muda mrefu na tayari wameshawabaini miongoni mwa wanaowahujumu na watawashughulikia ipasavyo

Source Mwananchi

Mlale unono 😃
Visingizio vimeanza, watuhumiwa wa mwanzo walikuwa msanii wa sarakasi mr. Nyani akishirikiana na msomi Bundi.
 
Back
Top Bottom