Kadogosa: Nauli ya Treni ya Mchongoko Dar - Dodoma itakuwa tsh 100,000 - 120,000

Kadogosa: Nauli ya Treni ya Mchongoko Dar - Dodoma itakuwa tsh 100,000 - 120,000

Mkurugenzi wa TRC Kadogosa amesema nauli ya Treni ya Mchongoko( Mjusi) itakuwa Kati ya tsh 100,000 - 120,000

Source: Swahili Times

Mlale Unono 😃😃
=========

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania (TRC), Masanja Kadogosa amesema bei za treni za mchongoko zitakuwa Tsh. 100,000 hadi 120,000 kutoka Dar es Salaam hadi Dodoma ambapo treni hizo zitakuwa ni express ambazo hazitosimama kila kituo bali kutoka Dar es salaam zitasimama Morogoro kisha Dodoma .

Akiongea Jijini Dar es salama leo June 12,2024, Kadogosa amesema “LATRA wametangaza nauli za daraja za kawaida lakini tutakuwa na treni za aina tatu, treni za kawaida ambazo zinasimama kote, tutakuwa na treni za express ambayo ikitoka hapa inasimama Morogoro, Morogoro - Dodoma lakini pia tutakuwa na treni nyingine ambayo ni high class zaidi zile za mchongoko tumeshaanza kuifanyia majaribio lakini June 16,2024 tutapokea nyingine mbili”

“Mule ndani kuna class mbili economy na business lakini ile nyingine kuna business lakini pia kuna Royal business kuna sehemu wanakaa Watu 48 tu na nyingine wanakaa chini ya hao Watu, business tutaenda kwa Tsh. elfu 70, katika ile ya mchongoko Royal tutaenda kwa Tsh. 120000 na business ya kawaida laki 1 na itakuwa express”

“Tunafanya hivyo Ndugu Waandishi wa Habari naomba hili mliweke vizuri tunajaribu ku-accomodate Watu wote, kuna zile ambazo mmetangaziwa, najua Watu watalalamika lakini hatuwezi kuwa na mentality ileile”

Itakumbukwa hivi karibuni Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA) ilitangaza maamuzi ya Bodi ya Wakurugenzi ya LATRA kuhusu nauli za abiria wa daraja la kawaida kwa Treni ya Reli ya Kisasa (SGR) kutoka Dar es Salaam hadi Makutupora baada ya kufanyia kazi maombi ya Shirika la Reli Tanzania (TRC) na maoni ya Wadau wengine ambapo Dar es salaam hadi Morogoro (KM 192) nauli ni Tsh. 13000 na Dar es salaam hadi Dodoma (KM 444) nauli ni Tsh. 31000.
#MillardAyoUPDATES

Pia Soma: Hizi hapa Nauli Mpya za SGR: Dar - Moro Tsh. 13,000, Dar - Dodoma Tsh. 31,000
Ndege dodoma hadi dar bei gani
 
Mpango wa kubinafsisha huu. Siku chache baadae shirika limeshindwa kujiendesha.
Zile kauli za mbalawa zitakuja kutimia muda si mrefu.
 
Linachukua siku ngapi kufika mwisho wa safari? Kama linaenda haraka, lazima tulipie maana hakuna cha bure bure
 
Nina experience na India wao treni ya Gharama kubwa kabisa kwa umbali kama wa Dodoma to Dar (Nimechukua mfano wa Mumbai to Vadodara almost 450Km) nauli zao ni inclusive yani kila mtu atapanda treni ya uwezo wake; kuna nauli za thamani ya kuanzia chini ya Tsh10,000/= mpaka 40,000/= kwa treni ya kawaida(ya umeme) muda wa safari ni masaa 6.

Treni ya mchongoko gharama ya Juu kabisa ni kama 75,000/= ya kitanzania na inatumia masaa 4.
 
Attachments

  • Screenshot_20240614_170310_PhonePe.png
    Screenshot_20240614_170310_PhonePe.png
    94.5 KB · Views: 5
  • Screenshot_20240614_170400_PhonePe.png
    Screenshot_20240614_170400_PhonePe.png
    88.2 KB · Views: 4
Uzuri wa technology kudanganya ni kazi sana. Tokyo-Kyoto ni ¥16,000 ambayo ni $100 ambayo ni Tzs 260,000. Mtu anaesema treni ni rahisi huko majuu hajawahi kusafiri au yuko huko hajawahi kupanda treni.
Miaka 10 nyuma London-Manchester ilikuwa £100-120 wakati bus ilikuwa £15 tu.
View attachment 3016979
Hahaha jf kila mtu mropokaji mkuu ndio niko hapa namsubiri anitajie hiyo nauli nafuu ya treni from Tokyo to Osaka, tena akakazia kabisa eti popote duniani treni ndio usafiri nafuu kwahiyo acha yeye atuelezee, maana inaonekana mwenzetu ni Global citizen sisi wengine ni washamba tu wa vijijini 😃😃
 
Kwa akili yako pesa ya Japan inafanana thamani na pesa ya Tanzania?
Unawezaje kufananisha matumizi ya pesa ya Japan kwa matumizi yao ya kila siku kwa kulinganisha na thamani ya pesa ya Tanzania .

Unakuta mtu anafananisha mtumizi ya US Dollar kwa matumizi ya huko unafananisha na Tanzania.

Halafu tena unaonesha speed ya train ya zaidi ya 380km/hr kulinganisha gharama na train ambayo hata haijakaribia speed ya 160km/hr kama walivyokuwa wanaamini .

Uchambuzi wa Hovyo sana huu..

Kulingana na speed ya hovyo hiyo gharama haziendani kabisa labda kama wanaweka gharama kurudisha pesa za mkopo.

Kwa umeme wao wa route moja wa 360,000 Tsh
Sasa mbona unatwist mada tena, wewe ulisema duniani kote treni ndio usafiri nafuu, bila shaka ulilinganisha na usafiri wa aina nyingine kama ndege, basi na meli, sasa hayo mambo ya thamani na matumizi ya hizo pesa yametoka wapi tena hapo
 
Nadhani SGR wa-focus zaidi mizigo kuliko abiria wapunguze malori barabarani; sio kuyapunguza kwa lazima bali kwa unafuu wa bei, muda, rushwa za barabarani, n.k.

Wakijielekeza usafirishaji abiria inanipa shaka itakuwa kama the so called "mwendokasi" ambao ndani ya muda mfupi umekosa kabisa mwelekeo.

Upo sahihi
 
Back
Top Bottom