Kadogosa: Tumetumia umeme wa 336,000 kwenda na kurudi Dar - Morogoro

Yaan Mimi kichwani kwangu nilikuwa nafikiria ...train ya umeme itakuwa na speed!! Labda 30min tuu mpaka Moro...
Kumbe inachukua muda hivyo.
Duh hata mimi nilidhani Dar Moro itakua Lisaa limoja tu kumbe I was wrong. Issue ni kwamba inatumia umeme tu ila spidi na distance covered ni kama reli ya Tazara tu!!
 
Waswahili kiboko
Yaani mtu anashangaa au anakataa hiyo gharama wala sielewi
Halafu nasubiri nisome gharama halisi anazozikataa hizo sioni
Sasa na mimi mwingine hapa siongezi bei bali nasema gharama ni buku tu kwenda na kurudi

Mswahili mpe picha mengine tuachie wenyewe tupigane kwa keyboard
 
Itakuwa inakwenda kubeba madini ya nickel..? Kwenda bandarini..!
Madini haya yanayotumika kutengeneza battery za gari za umeme..?
 
Kwa ujumla nishati ya umeme inayotumika kwa treni za umeme inategemea mambo kadhaa. Moja, ni uzito wa treni yenyewe, yaani uzito kulingana na idadi ya mabehewa na uzito wa watu na mizigo.

Pili, idadi ya stops treni inayofanya. Yaani, nishati inayohitajika kuanza kusukuma treni katika mwendo mdogo ni kubwa kuliko ile inayohitajika kumaintain mwendo kasi mkubwa (cruising speed). Ukiwa na stops nyingi consumption ya umeme katika kuanzisha mwendo itakuwa kubwa.

Tatu, hali ya milima au tambarare. Ni wazi treni hii ya majaribio ilikuwa na mabehewa machache, na kiwango kilichotajwa cha matumizi ya umeme hakiwezi kuwa ndicho cha treni ya abiria iliyosheheni.
 
Atupe maspecifikesheni ya hio treni tumkalukuletie hio gharama tuone kama kweli imefikia

Electric train 1
Economy: 1.6 kWh per 100 passenger-km (full), 0.016 kWh/p.km
Its not clear if this energy consumption is average or max power.

Economy: 4.4 kWh per 100 passenger-km (full), 0.044 kWh/p.km

High speed intercity train
Electric Economy: 3 kWh per 100 passenger-km (full), 0.03 kWh/p.km
 
Waongeze mzigo plus kupunguza vituo ili kupunguza muda wa kukaa barabarani pamoja na umeme unaotumika kuanzisha mwendo ambao huliwa zaidi.

Nadhani engineers plus wachumi wa biashara ya treni watakaa kuangalia best alternative way ya kupunguza gharama kwa abiria by substituting to the cargo na factors nyingine.

All in all huwezi kufananisha basi au lorry na treni. Tutapunguza foleni ya dar mpaka chalinze kwa asilimia kubwa ambayo imekuwa ni kero kubwa kuanzia kibaha, mlandizi, vigwaza nk.
 
Kwa rate ipi? Lengo ni kushusha bei ya umeme.
 
Lengo ni kushusha bei ya umeme toka NHPP
 
Umeme wa laki 3+, sawa sio kesi, kwa idadi ya abiria inayobeba treni, behewa moja kule kajamba nani ni kama watu 60 hivi(sina hakika ni makadirio) hawa wana bei zake, bado 2nd class, bado 1st class kila daraja na nauli yake, still si shida kabisa, watwambie tren ya mafuta ilikuwa inatumia diesel kiasi gani mpaka moro ili tuweze linganisha.
 
Hata na mimi siamini hii.

Kama ni kweli basi nauli isizidi Buku 5.
Wapinga vision ya magufuli ni wajinga sana .... Magufuli alikuwa jembe siyo huyu zuzu tuliyenaye sasa na mazuzu wa Chadema walio mpinga JPM kwenye kila kitu kuanzia treni hadi bwawa la umeme ... JPM alipanga kuwa bwawa la umeme likikamilika basi bei ya umeme iwe sh 1000 unit 5 kisha apige marufuku mikaa na kupambana na mafisadi wa gesi waliokuwa wanahujumu nchi kwa kuweka bei ya gesi juu mara 2 ya bei iliyo stahili kuuzwa nchini....kitendo cha kushusha bei ya umeme kwa kiwango hicho kinge amsha miji na vijiji kiuchumi na miji isinge lala maana umeme ungependezesha miji usiku siyo sasa hivi hadi jiji la dar magorofa yanazimwa umeme usiku na kuwa giza na kubakisha kitaa kimoja mlangoni
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…